Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa amezidisha uvumi wa kuwa huenda akahama timu hiyo kufuatia majibu ya swali aliloulizwa na jibu alilotoa.
Zlatan amekuwa akihusishwa kuhama PSG msimu huu kwa muda mrefu licha ya yeye kutotoa jibu la kukanusha wala kukubali kuhusiana na uvumi huo... Zlatan ambaye amejiunga PSG toka mwaka 2012 akitokea katika klabu ya AC Milan ya Italia amekuwa akihusishwa kurudi AC Milan
ambayo imedhamiria kurejesha makali yake kwani msimu uliopita
haikufanya vizuri na ilimaliza katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Seriea A.
Baada ya mechi ya michuano ya International Champions Cup ambapo PSG ilishinda kwa goli 4-2 dhidi ya klabu ya Fiorentina ya Italia Zlatan aliulizwa swali kuhusu hatma yake.“Nitabakia Paris? Maamuzi yote yapo mikononi mwa Mino Raiola”>>>> Zlatan
Mino Raiola ni wakala wa Zlatan Ibrahimovic ambaye anashughulikia masuala yake yote ya uhamisho kutoka klabu mmoja kwenda nyingine au wakata anaposaini mkataba mpya.
0 maoni:
Post a Comment