Friday, July 8, 2016


Nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari akiwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. 
Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimpokea kwa shangwe nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akimkabidhi taji la maua nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari mara baada ya kuwasili ndani ya uwanja cha ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutokea katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Paris nchini Ufaransa. Pembeni ni Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko. 
 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na nyota wa soka aliyefanya vizuri michezo ya Shule za Sekondari (UMISETTA) Mussa Bakari (katikati) pamoja na Pamela Lugenge (kulia) mmoja wa Afisa Masoko.



Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja. 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezindua mashindano ya magari ya hapa nchini  ya 2016 na kuwataka watazania kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mchezo huo ambapo amewataka kuacha kujiweka nyuma na kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila siku. Hayo ameyasema wakati akizindua mashindano hayo ya magari yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho wilaya ya Bagamoyo ikihusisha magari 25.

Nape amesema kuwa wanachotaka kuona ni kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano hayo na zaidi wanataka kuona wanazidi kuwavutia wageni kwenye mashindano hayo ili kuongeza utalii wandani na kuongeza pato kwa serikali pale watakapoamua kutembelea mbuga za wanyama. 

“Nawataka watanzania kuzidi kufanya vizuri kwenye mashindano na zaidi wawavutie wageni kwani watakapokuja kwa wingi wataongeza pato la taifa pale watakapotembelea hifadhi za taifa,”amesema. 

Naye  Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa mwaka jana waliweza kuondoa kauli ya kichwa cha mwendawazimu na walilitekeleza kama walivyomuahidi Raisi mstaafu wa awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi na mwaka huu watazidi kufanya vizuri na watabakisha ushindi nyumbani. Mashindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati  ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni  17.

Magari hayo  17  ya Tanzania ambapo  Dar es Salaam  magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza na yatakuwa kwa muda wa siku mbili.


Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka kandarasi mpya ya miaka sita na mmiliki wa klabu hiyo akisema ingekuwa makosa kutompatia kandarasi ndefu.
Klopp alijiunga na Liverpool mnamo mwezi Oktoba ,baada ya kukubali mkataba wa pauni milioni 15 ambao umeongezwa hadi mwaka 2022.
''Uongozi wake utakuwa muhimu katika kufanikisha malengo yetu'',  alisema mmiliki wa Liverpool.

Klopp aliifikisha Liverpool katika fainali ya League Cup pamoja na fainali ya Europa League msimu uliopita.

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 49 aliisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji mawili ya Bundesliga pamoja na kucheza fainali ya vilabu bingwa Ulaya 2013.


Pep Guardiola held his first news conference since taking over as Manchester City manager, on FridayPepMkufunzi mpya wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa alienda nchini Uingereza kuthibitisha kuwa inawezekana kucheza mchezo mzuri katika ligi ya Uingereza.
Gurdiola mwenye umri wa miaka 45 ambaye ametia kandarasi ya miaka mitatu ,amesema kuwa alipendelea kusalia kuifunza Bayern Munich,lakini alitaka mtihani mwengine katika ukufunzi wake.

Raia huyo wa Uhispania amekiri kwamba alikuwa na kila alichohitaji wakati alipokuwa Barcelona ,lakini akakana kuwa huenda anakabiliwa na kibarua kigumu katika klabu ya Manchester City.
''Niko hapa kuthibitisha kuwa ninaweza kuchezesha soka nzuri vilevile nimekuwa nikicheza'',alisema.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuanzisha mtindo mzuri wa tiki-taka kama ule wa Barcelona, alisema Guardiola:''Hiyo ndio sababu niko hapa''.
Aliongezea:''Sijawahi kucheza wakati wa siku kuu ya Boxing Dei.Sijawahi kuwa katika uwanja wakati ambapo kuna upepo mkali na baridi na uwanja sio mzuri.Ni lengo langu. Nataka kuwathibitishia'


Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mecky Maxime ametua Kagera Sugar. Maxime ambaye alikuwa akiinoa Mtibwa Sugar, sasa amesaini mkataba wa kuinoa Kagera Sugar. Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein amesema Maxime ndiye kocha mkuu akichukua nafasi ya Adolf Rishard.
Awali, kulikuwa na taarifa za kuondoka kwa Maxime kwenda Kagera, lakini uongozi wa Mtibwa Sugar ulilikataa hilo. Kuna tarifa Mtibwa Sugar inatarajia kumrejesha Salum Mayanga ambaye sasa anainoa Prisons.

waliotembelea blog