Agnes Gerald ‘Masogange’.
Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
Sharifa Mahamoud (27
Melisa Edward
Saada Ally Kilongo (26),
MTANDAO wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia
madai ya kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji
‘punda’ wa biashara hiyo haramu, Hivi
karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’
amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na
hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda
kortini mara moja Ijumaa iliyopita.
Wakati Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini
kwa sasa ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed
’Z-Anto’, Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano
kwa sakata la ‘unga’.
HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita, habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa
Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na hatia ya
kukutwa na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi
kufa au la! Sheria za hukumu hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi
kufa.
UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.
Kwenye makazi ya mama yake, Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo
amehama baada ya kufunga ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan.
IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo
ambapo lilifanikiwa kumpata ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya
naye mazungumzo kama ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda: Kuna manenomaneno kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China
baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu: Kwanza kabisa Binti Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong
Kong, kwa sheria za kule mtu akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’
anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana
EMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana anayejulikana
kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu wa Kanumba’ yeye
bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma za kukutwa na
madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Mdada huyo mkazi wa
Mbezi Beach, Dar aliwahi kutoka kwenye Gazeti la Ijumaa la Desemba 9,
2011 ukurasa wa mbele kwa kichwa cha habari kisemacho: SAA 7 USIKU
KANUMBA AGANDANA NA DEMU.
Demu huyo ambaye wakati
huo alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar
(alimaliza mwaka jana), picha yake akiwa na marehemu Kanumba ilipigwa
Desemba 2, 2011 ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo kulirindima
Tamasha la Usiku wa Kiafrika lililopambwa na mkali wa dansi kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa’.
MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu
Bongo, Sharifa Mahamoud (27) naye anashikiliwa katika gereza moja nchini
Misri wakati kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima
nchini humo.
BALOZI WA TANZANIA -MISRI AZUNGUMZA
Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mohammed Haji, Mei 18,
mwaka huu, Sharifa na nduguye, Abdallah Salum (28), wote wakazi wa
Magomeni, Dar, walinaswa na unga jijini Cairo wakitokea Dar.
Mei 26, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. Madawa waliokutwa nayo ni heroine kilo saba (gharama ya fedha haikutajwa).
Kwa sheria za Misri, kosa la kukutwa na madawa ya kulevya ni kunyongwa
hadi kufa. Lakini kwa mujibu wa Balozi Salum, hana kumbukumbu za raia wa
kigeni aliyewahi kuhukumiwa kunyongwa nchini humo kwa kosa hilo.
Balozi alisema: “Endapo watapatikana na hatia kwamba kweli dawa hizo
zilikuwa zao, hili litakuwa doa la kwanza kwa nchi yetu (Tanzania) hapa
Misri.
Kwa mujibu wa Sharifa wakati akihojiwa na TV ya Misri, alishangaa kuona
begi lake likiwa na madawa ya kulevya baada ya kukamatwa na kwamba
aliingia nchini humo kumtafuta binamu yake.