Saturday, August 9, 2014

Record holder: Drogba scored 65 goals in his 104 caps for Ivory Coast, more than any other playerDrogba alisaidia Nchi yake katika upatanishi baada ya mgogoro wa kisiasa
Mchezaji soka maarufu wa Ivory Coast Didier Drogba, ametangaza kustaafu kutoka katika soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alichezea Ivory Coast zaidi ya mara miamoja.
Alishiriki kombe la dunia mara tatu na mashindano ya kombe la Afrika mara 2
Amesema kuwa anajivunia kusaidia nchi yake kufika katika nafasi hiyo kimataifa.
Drogba alipigia debe kumalizika kwa mgogoro wa kisiasa na pia kuhimiza pande zilizozozana kupatana.
ACN: Didier Drogba and the Ivory Coast finished runners-up in the 2012 African Cup of NationsDidier Drogba

01
Meneja Bidhaa wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo wakati uzinduzi wa  tamasha la muziki la mwaka huu la Serengeti Fiesta litakaloanza kutimua vumbi kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapo. Kulia ni Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Sebastian Maganga . Fiesta ya mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la leo ni, Diamond Platinum, Ommy  Dimpos, Linah, Chenge, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Mwana FA, Young Killer, Ben Pol, Christian Bella, Roma, Ney wa Mitego, Mkubwa na wanae, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee.02
Mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika matamasha ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta, Vanessa Mdee akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la muziki la mwaka huu la Serengeti Fiesta litakaloanza kutimua vumbi kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapo. Kushoto kwake ni Meneja wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Sebastian Maganga . Fiesta ya mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la leo ni, Diamond Platinum, Ommy Dimpos, Linah, Chenge, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mr. Blue, Mwana FA, Young Killer, Ben Pol, Christian Bella, Roma, Ney wa Mitego, Mkubwa na wanae, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee.
03
Mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika matamasha ya mwaka huu ya Serengeti Fiesta, Mr Blue akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa uzinduzi wa  tamasha la muziki la mwaka huu la Serengeti Fiesta litakaloanza kutimua vumbi kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapo. Fiesta ya mwaka huu inadhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la leo ni, Diamond Platinum, Ommy  Dimpos, Linah, Chenge, Temba, Shilole, Ally Kiba, Mwana FA, Young Killer, Ben Pol, Christian Bella, Roma, Ney wa Mitego, Mkubwa na wanae, Barnaba, Belle 9, Rachel na Madee.
 





Majembe ya kazi: Manahodha wa Barcelona kutoka kushoto Sergio Busquets, Lionel Messi, Xavi na Andres Iniesta

KIUNGO mkongwe, Xavi Hernandez ameteuliwa kuwa Nahodha mpya wa wazee wa Katalunya, FC Barcelona kuanzia msimu ujao.
Kitambaa cha unahodha wa Barca kimeachwa wazi na beki Carles Puyol aliyestaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita na kura zikapigwa kumpata atakayerithi mikoba yake.

Nyota huyo wa Hispania, alishinda kura zilizopigwa na kutangazwa rasmi jana kuwa Nahodha Mkuu, akifuatiwa na Andres Iniesta, Lionel Messi na Sergio Busquets, ambao watakuwa Manahodha Wasaidizi.


Hard year: Phil Neville said last season was a disaster for Manchester United under David Moyes
Mwaka mgumu: Phil Neville alisema msimu uliopita ulikuwa wa majanga kwa Manchester United chini ya David Moyes.

Imechapishwa Agosti 9, 2014, saa 1:50 asubuhi

PHIL Neville amekiri kuwa kumteua David Moyes kuifundisha Manchester United lilikuwa janga kubwa.
Neville, ambaye aliteuliwa na Moyes kuwa kocha msaidizi namba moja msimu uliopita alisema: 'Wote tulitakiwa kuwajibika, sio David Moyes tu. Niliwajibika na wengine waliohusika walitakiwa.
'Mwaka uliopita ulikuwa ni janga kwelikweli, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.'
Terrible time: Moyes guided United to seventh in the league despite joining the club as they were champions
Muda wa majanga: Moyes alimaliza katika nafasi ya 7 licha ya kupewa klabu ikiwa ni bingwa mtetezi.

Lakini Neville anaamini, United inaweza kurudi vizuri kutoka kwenye nafasi mbaya zaidi waliyomaliza ikiwa imepita miaka 24: 'Nadhani tunaenda kushinda kombe,' alisema. 'Nafasi ya pili sio nzuri kabisa kwa Manchester United.
'Tumepata nafasi nzuri mwaka huu kwasababu hatuna michuano ya Ulaya.
'Ni kuwaunganisha pamoja na wachezaji wote wanaonekana kuwa tayari kushinda ligi tena baada ya kutoka kwenye maandalizi ya msimu'.

Bondia Thomasi Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Maugo alishinda kwa point 
Bondia Said Memba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Khalid Chokoraa wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Chokoraa alishinda kwa point picha na 
Bondia Khalid Chokora kushoto akilusha konde kwa saidi Memba wakati wa mpambano wao chokoraa alishinda kwa point
Bondia Thomas Mashali kulia akimrushia konde la mkono wa kulia bondia Mada Maugo wakati wa mpambano wao uliofanyika juzi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Maugo alishinda kwa point mpambano huo
Mabondia Mada Maugo kushoto na Thomas Mashali wakipambana ulingoni

 
TAMASHA la Usiku wa Matumaini, Dar (Dar Night of Hope 2014) lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar lilikuwa ni full msisimko kutokana na matukio mbalimbali yaliyofanyika.
Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makamu wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana Makamu wa rais Mh.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Miongoni mwa matukio yaliyosisimua kwenye tamasha hilo ni pale mechi za mpira wa miguu zilipokuwa zikichukua nafasi.

Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Wakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Mwanamuziki H-Baba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
Wengi walikuwa wakishangilia wakidai ni siku nyingi hawajamuoana uwanjani, huku wengine wakishangilia kwa kuimba wimbo wake mpya wa Mwana.
 
Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa ‘Cloud 112′.
Kama hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba kufunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo Fleva waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye tamasha hilo.
 
Nyomi iliyokusanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwa ajili ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKU
Licha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.
 
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
 
Bondia Mada Maugo amemshushia kichapo bondia Thomas Mashali katika mpambano wao kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
WABUNGE SIMBA VS YANGA
Wakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
 
Yanga wakishangilia bao lao.
Matukio mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti na kutoa burudani baab’kubwa.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!
 
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba

 
Mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ghalib Bilal akitoa hotuba.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014, Eric Shigongo naye akitoa neno la matumaini kwa maelfu ya Watanzania waliofurika Uwanja wa Taifa, Dar.
Mgeni rasmi Dk. Ghalib Bilal akikakua timu ya wabunge wa Simba.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wabunge wa Yanga.
Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongea jambo na refa wa mchezo wa mechi ya wabunge akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global, Eric Shigongo.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mohamed Ghalib Bilal amelipongeza wazo la Tamasha la Usiku wa Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers, jana kuwa ni zuri.
Alimpongeza Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwa kuandaa tamasha hilo kwani linaunganisha Watanzania wote.

 Mkurugenzi
Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga a.k.a Joe sambamba na
Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time
Promotions ,Bi Juhayna Kusaga ambao ndio waandaaji wa Tamasha la
Serengeti Fiesta 2014 wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia
ya Serengeti (SBL),Bwa.Ephraim Mafuru  ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo wakiwa ndani ya hafla ya Meet&Great ya Wasanii
mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya (watakaoshiriki tamasha la fiesta)
na wadau wengine ndani ya Ufukwe wa Club ya Jembe ni Jembe,ilioko nje ya
mji wa Jiji la Mwanza.
Tamasha
la Serengeti Fiesta linatarajiwa kuzinduliwa leo ndani ya uwanja wa CCM
Kirumba,huku Wasanii mbalimbali wakiwa wamekwishawasili tayari kwa
onesho hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na Wakazi wa jiji hilo la
Miamba.
 Baadhi
ya Wasanii bongofleva na Wadau wengine mbalimbali wa muziki wakiwa
wamujumuika kwa pamoja kwenye hafla ya meet&great iliyofanyika usiku
wa kumkia leo kwenye kiota cha maraha cha Jembe ni Jembe,jijini Mwanza.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,pichani kulia Sebastian Maganga
akiwa na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM,kwenye hafla hiyo ya
Meet&Great.Pichani shoto ni B Dozen,Nikson pamoja na Millard Ayo.
Baadhi
ya Wasanii watakaoshiriki tamasha la Fiesta wakiwa wamejichanganya na
wadau wengine wakibadilishana mawazo na kufahamiana pia.

 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye ni shabiki wa Yanga, Ridhiwan Kikwete akivua jezi yake kwa ajili ya mashabiki mara baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3-2 dhidi ya Simba leo.
 
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akishangilia na shabiki wake baada ya ushindi wa Yanga.
 
Mwigulu Nchemba akiwarushia skafu yake mashabiki wa Yanga.
 
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.
 
Hekaheka wakati wa mtanange huo.
 
Mashabiki wakifuatilia mtanange huo.
 
Timu zikiingia uwanjani.
 
Ridhiwan akiwapa hi mashabiki.
 
Waamuzi wakiingia uwanjani.
 
Kikosi cha Yanga kilichokwaana na Simba na kuibuka na ushindi wa 3-2.
 
Kikosi cha Simba kilichopigwa 3-2 na Yanga.
 
Mwamuzi Othman Kazi akiongea na manahodha wa Yanga na Simba (Wabunge).
Mechi ya wabunge mashabiki wa Simba na Yanga iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 imemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2. Wafungaji Simba: Maji Marefu na Yusuf Gogo. Yanga: Idrissa Kitwana, Ahmed Ngwali na Mark Tanda.

waliotembelea blog