Saturday, August 9, 2014


Majembe ya kazi: Manahodha wa Barcelona kutoka kushoto Sergio Busquets, Lionel Messi, Xavi na Andres Iniesta

KIUNGO mkongwe, Xavi Hernandez ameteuliwa kuwa Nahodha mpya wa wazee wa Katalunya, FC Barcelona kuanzia msimu ujao.
Kitambaa cha unahodha wa Barca kimeachwa wazi na beki Carles Puyol aliyestaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita na kura zikapigwa kumpata atakayerithi mikoba yake.

Nyota huyo wa Hispania, alishinda kura zilizopigwa na kutangazwa rasmi jana kuwa Nahodha Mkuu, akifuatiwa na Andres Iniesta, Lionel Messi na Sergio Busquets, ambao watakuwa Manahodha Wasaidizi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog