Saturday, August 9, 2014

 Mkurugenzi
Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga a.k.a Joe sambamba na
Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time
Promotions ,Bi Juhayna Kusaga ambao ndio waandaaji wa Tamasha la
Serengeti Fiesta 2014 wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia
ya Serengeti (SBL),Bwa.Ephraim Mafuru  ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo wakiwa ndani ya hafla ya Meet&Great ya Wasanii
mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya (watakaoshiriki tamasha la fiesta)
na wadau wengine ndani ya Ufukwe wa Club ya Jembe ni Jembe,ilioko nje ya
mji wa Jiji la Mwanza.
Tamasha
la Serengeti Fiesta linatarajiwa kuzinduliwa leo ndani ya uwanja wa CCM
Kirumba,huku Wasanii mbalimbali wakiwa wamekwishawasili tayari kwa
onesho hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na Wakazi wa jiji hilo la
Miamba.
 Baadhi
ya Wasanii bongofleva na Wadau wengine mbalimbali wa muziki wakiwa
wamujumuika kwa pamoja kwenye hafla ya meet&great iliyofanyika usiku
wa kumkia leo kwenye kiota cha maraha cha Jembe ni Jembe,jijini Mwanza.
Mwenyekiti
wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,pichani kulia Sebastian Maganga
akiwa na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM,kwenye hafla hiyo ya
Meet&Great.Pichani shoto ni B Dozen,Nikson pamoja na Millard Ayo.
Baadhi
ya Wasanii watakaoshiriki tamasha la Fiesta wakiwa wamejichanganya na
wadau wengine wakibadilishana mawazo na kufahamiana pia.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog