TAMASHA
la Usiku wa Matumaini, Dar (Dar Night of Hope 2014) lililofanyika jana
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar lilikuwa ni full msisimko kutokana na
matukio mbalimbali yaliyofanyika.
Staa
kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha
la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makamu
wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana Makamu wa rais
Mh.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Miongoni mwa matukio
yaliyosisimua kwenye tamasha hilo ni pale mechi za mpira wa miguu
zilipokuwa zikichukua nafasi.
Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Wakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati
ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh
Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.
Wengi walikuwa wakishangilia
wakidai ni siku nyingi hawajamuoana uwanjani, huku wengine wakishangilia
kwa kuimba wimbo wake mpya wa Mwana.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa ‘Cloud 112′.
Kama
hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba kufunga
bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo Fleva
waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye
tamasha hilo.
Nyomi iliyokusanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwa ajili ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKU
Licha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha
kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa
washindi.
Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
Bondia
Mada Maugo amemshushia kichapo bondia Thomas Mashali katika mpambano
wao kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
WABUNGE SIMBA VS YANGA
Wakati wa mechi ya wabunge,
vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge
walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku
ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua
nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea
kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.
Yanga wakishangilia bao lao.
Matukio
mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma
Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti
na kutoa burudani baab’kubwa.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!
Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba
0 maoni:
Post a Comment