Video
mpya ya staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz imetazamwa na watu
zaidi ya laki nane na tisini kwa muda wa wiki moja tangu itoke Desemba
11, mwaka huu.
Mkali huyo wa Bongo Fleva anatarajia kuangusha bonge moja la shoo ndani
ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar siku ya Krismasi,
keshokutwa.
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Akizungumzia maandalizi ya shoo hiyo, Diamond alisema itakuwa ya tofauti. Kila atakayelipia fedha yake ( kawaida shilingi 15,000 na V.I.P shilingi 30,000) hatojutia.
"Tukutane pale Dar Live, tuimbe na kucheza nyimbo zote za Diamond kuanzia
Kamwambie, Lala Salama, Moyo Wangu, Mbagala, Nimpende Nani, Nitarejea,
Ukimuona, Nataka Kulewa, Kesho, Nasema Nao, Mawazo, Number One, Nana,
Nitampata Wapi, Kizaizai, MdogoMdogo, BamBam na Utanipenda ambao ndiyo
habari ya mjini kwa sasa," alisema Diamond.