MUONEKANO WA BASI LA BUKOBA EXPRESS T 315 BLC
BAADA YA KUANGUKA ,BASI LILIKUWA LINATOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA BUKOBA
MUDA MCHACHE BAADA YA KUANZA SAFARI ALFAJIRI YA LEO KUTOKA LILIPOKUWA
LIMELALA,TAYAR KUANZA SAFARI YA KUELEKEA BUKOBA,WATU WOTE WAMENUSURIKA KIFO NA WENGINE KADHAA WAMEPATA MAJERAHA !!!
Sanamu kubwa zaidi duniani ya
Nelson Mandela imezinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria
siku moja baada ya rais huyo wa zamani kuzikwa.
Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba ina urefu
wa mita tisa na ina uzani wa tani nne unusu. Ilizinduliwa katika bustani
la majengo ya bunge na inaonyesha Nelson Mandela akihimiza umoja na
maridhiano.
Sanamu hiyo yenye mikono ya Mandela ikiwa wazi ilinuiwa kuonyesha Mandela alivyoliungaisha taifa zima kwa mapenzi yake.
Bwana Mandela lipewa mazishi ya kitaifa nyumbani alikozaliwa katika kijiji cha Qunu Jumapili
Familia ya Madiba , viongozi wa ANC , viongozi
wa Afrika na maafisa wengine wakuu walihudhuria mazishi hayo katika
kijiji cha Qunu mkoani Cape Mashariki.
Kifo cha Mandela kilifuatwa na maombolezi ya
siku kumi na sherehe za kukumbuka maisha ya Mandela aliyefariki akiwa na
umri wa miaka 95.
Bendera ya nchi hiyo ilirejeshwa kupepea katika urefu wake wa kaiwada.
Mandela anakumbukwa kwa juhudi zake za
kupatanisha wananchi na kupigia debe msamaha miongoni mwa watu na ndio
maana leo ikawa siku iliyotengwa kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu hiyo.
Wakati wa utawala wa wazungu, terehe 16 Disemba
ilijulikana kama siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Afrikaners walioshinda
vita dhidi ya jeshi la Zulu mwaka 1883.
Zaidi ya karne moja baadaye mwaka 1961, Mandela alizindua jeshi lake la Umkhonto we Sizwe kupigana dhidi ya utawala wa wazungu.