Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi
wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza.
Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao
na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama
alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi
wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja
hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?
Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani. Kwa mujibu wa
Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli
kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.
0 maoni:
Post a Comment