Monday, December 16, 2013


Mazishi ya Nelson Mandela yanaendelea katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa wa Afrika mwendazake Nelson Mandela.

 
Takriban watu 4,500 wakiwemo wageni wa kimataifa wanahudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.
 
Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.




 Rais Jakaya Kikwete ni mmoja wa viongozi mbalimbali wanaoshiriki kwenye mazishi ya hayati Mzee Nelson Mandela yanayofanyika leo kijijini kwao Qunu, nchini Afrika Kusini.


Watu wengi maarufu Duniani wapo eneo hili hivi sasa kuhudhuria mazishi ya Mzee Nelson Mandela yanayoendelea hivi sasa katika kijiji cha Qunu,baadhi yao ni Oprah Wilfrey,Forest Whitaker,Richard Branson,Idris Ebra na wengine wengi.


Mwili wa Mzee Mandela ukiwasili ukumbini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog