Sunday, October 6, 2013


Mama lulu atoboa siri za kanumba, aelezea mengine mengi zaidi!
Mama wa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila kwa mara ya kwanza amemfungukia marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012. Mahojiano hayo yamefanywa hivi karibuni na gazeti la Risasi linalotolewa na kampuni ya GPL
Ifuatayo ni habari hii kama ilivyoripotiwa na mwandishi wa gazeti hilo.

Katika mahojiano rasmi na Risasi Jumamosi, juzi jijini Dar, Mama Lulu aliweka wazi kila kitu kuhusu madai mbalimbali ya yeye na mama Kanumba, Lulu na marehemu Kanumba.
Mambo yaliyoelekezwa ayajibu mwanamama huyo ni pamoja na madai kwamba alishapokea barua ya posa ya Kanumba kutaka kumuoa Lulu, yeye na mama Kanumba kugombana hivi karibuni na Lulu kumjali zaidi mama Kanumba kuliko yeye.
Awali, mwanamke huyo alisema miongoni mwa watu waliofiwa na Kanumba yeye yupo mstari wa mbele kwani uchungu alioupata siku ya tukio mpaka leo haujamtoka.
Mahojiano kamili yalikuwa kama ifuatavyo:
Risasi: Mama kuna madai kadhaa ambayo ni vyema uyajibu.
Mama Lulu: (Kwa ukali kidogo) maswali gani? Mimi sitaki waandishi, nilishasema! Kama ni kuhusu Lulu muulizeni mwenyewe.
Ilibidi waandishi watumie kazi ya ziada ili mama huyo aweze kuzungumza.
Risasi: Ni mambo ya kawaida tu mama, wewe ndiyo unafaa kujibu, tafadhali tusikilize.
Mama Lulu: Haya, ulizeni.

ALIUJUA UHUSIANO WA KANUMBA NA LULU?
Risasi: Kuna madai kwamba uliujua uhusiano wa kimapenzi kati ya Lulu na Kanumba,  lakini mama Kanumba alikuwa hajui kinachoendelea, ni kweli?
Mama Lulu: Kwanza katika maisha yangu hakuna siku niliyowahi kupata mshtuko kama niliposikia Kanumba amefariki dunia na mwanangu Lulu kahusishwa na kifo kile, nilishtuka sana.
“Ilikuwa mara yangu ya kwanza kujua kumbe Kanumba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanangu Lulu, lakini kabla ya hapo sikuwa najua lolote.
ALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
“Ninachoweza kukiweka wazi ni kwamba, nilikutana na Kanumba nikamkabidhi mwanangu kwa moyo mweupe amlee kisanii kwa sababu nilijua anaweza, kumbe na wao wakaanzisha uhusiano huo kwa siri.
KWA NINI ALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
 “Mimi na Kanumba tulikuwa tumezoeana sana. Alinipa heshima zote kama mama yake na alikuwa kijana mwenye aibu kwangu kutokana na heshima, haikuwa rahisi kuangaliana machoni na ndiyo maana niliamua kumpa Lulu amkuze kisanii.
ALIPOKEA BARUA YA POSA YA KANUMBA?
“Si kweli, sijawahi kuona wala kupokea barua ya posa ya Kanumba kumchumbia Lulu.
KAMA KANUMBA ANGETAKA KUMUOA LULU?
“Lakini nataka kusema kwamba kama Kanumba angekuwa hai na angetaka kumuoa Lulu ningefurahi sana kwani naamini mpaka sasa wangekuwa wamepata mtoto mzuri na sisi wazazi tukaitwa bibi.”
MADAI YA KUGOMBANA NA MAMA KANUMBA?
Risasi: Kuna madai kwamba wewe na mama Kanumba kwa sasa ni paka na panya, na sababu kubwa ni Lulu kumjali zaidi mwanamke huyo kuliko wewe, ni kweli habari hizi?
Mama Lulu: Mimi na mama Kanumba hatuwezi kugombana hata siku moja. Kwanza Lulu nimempa jukumu kwamba kwa sababu wote ni mama zake, akinunua nyama kilo tano kwa ajili yangu na kwa mama Kanumba apeleke tano.
“Akinunua vocha ya elfu tano kwangu na mama Kanumba amtumie kama hiyohiyo. Kwa hiyo hakuna ugomvi.”
Risasi: Je, Lulu akimzidishia mama Kanumba wewe hutajisikia vibaya?
Mama Lulu: Siwezi kujisikia vibaya ingawa mimi kwa sababu naishi naye ni lazima nitapata zaidi, lakini akimsaidia naona ni sawa tu.

ALIKUWA AKIMUOGOPA MAMA KANUMBA?
Mwandishi: Ilikuwaje ukakutana na mama Kanumba kwa mara ya kwanza?
Mama Lulu: Lulu ndiye aliyekuwa akinishawishi kila mara niende nikaonane na mama Kanumba ingawa wakati mwanangu yuko jela kiukweli nilikuwa namuogopa sana.
“Unajua yule aliyepotea (Kanumba) ni mtoto kama wangu, lakini alipotoka tulikwenda nyumbani kwake na tunamshukuru alitupokea vizuri. Awali kabla ya kifo cha Kanumba sikuwahi kufahamiana naye.
Risasi: Ukiambiwa uongee na Watanzania utataka kuwaambia nini?
Mama Lulu: Cha kuwaambia ni kwamba, mimi na mama Kanumba si marafiki bali ni mtu na dada yake. Nawaomba wawaombee mama Kanumba na Lulu mwenyewe ili waendelee kupatana na kufanya kazi za sanaa pamoja kama walivyoanza.
Risasi: Tunashukuru sana mama.
Mama Lulu: Karibuni sana, mimi huwa naogopa sana magazeti, sipendi sana kuongea na waandishi wa habari.
KUMBUKUMBU YA LULU
Katika mahojiano na kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Lulu alisema: “Katika maisha yangu sitakaa nimsahau Kanumba kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mpenzi. Kamwe sitamsahau.”

Jumamosi 5 Oktoba
14:45 Manchester City 3 v Everton 1
17:00 Cardiff City 1  v 2 Newcastle United
17:00 Fulham 1 v 0 Stoke City
17:00 Hull City 0 v 0 Aston Villa
17:00 Liverpool 3 v 1 Crystal Palace
19:30 Sunderland 1 v 2 Manchester United
Jumapili 6 Oktoba
15:30 Norwich City v Chelsea
15:30 Southampton v Swansea City
18:00 West Bromwich Albion v Arsenal
18:00 Tottenham Hotspur v West Ham United
LA LIGA
Jumamosi Oktoba 5
Elche CF 2 RCD Espanyol 1
Rayo Vallecano 1 Real Sociedad 0
Levante 2 Real Madrid CF 3
FC Barcelona 4 Real Valladolid 1
Jumapili Oktoba 6
13:00 Atletico de Madrid v Celta de Vigo
18:00 Sevilla FC v UD Almeria
20:00 Getafe CF v Real Betis
22:00 Athletic de Bilbao v Valencia
SERIE A
Jumamosi Oktoba 5
Chievo Verona 0 Atalanta 1
Inter Milan 0 AS Roma 3
Jumapili Oktoba 6
13:30 Parma v Sassuolo
16:00 Bologna v Hellas Verona
16:00 Udinese v Cagliari
16:00 Sampdoria v Torino FC
16:00 Napoli v Livorno
16:00 Catania v Genoa
21:45 Juventus v AC Milan
21:45 SS Lazio v Fiorentina
Watu zaidi ya 60 waliokuwa wakisafiri wamenusurika kifo huku wengine wakijeruhiwa baada ya basi la Mtei Express Coach kuyagonga magari matatu katika eneo la kijiji cha Mawemairo Wilayani Babati Mkoani Manyara kilichopo katika barabara kuu inayotoka mjini babati kuelekea mkoani Arusha.
 
Ajali hiyo imelihusisha bus hilo lenye namba za usajili T 729 bes wakati lilipokuwa likitokea mjini Babati kuelekea mkoani Arusha na kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa wakisafiri wamesema lilipofika katika eneo hilo,dereva wa basi hilo alishindishwa kulimudu wakati alipopewa ishara na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya serikali ya china(Chico) kusubiri lori lililokuwa likishusha matofali kwa ajili ya ukarabati wa karavati na hatimaye kuyagonga magari yaliyokuwa yakisubiri lori hilo.
 
Nae mganga mfawidhi katika hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati Bw Mosses Mollel amesema amepokea majeruhi wanane na mpaka sasa amebaki majeruhi mmoja huku wengine wakiwa wamepata ruksa baada ya kupatiwa matibabu.

 Bw Salumu ally meneja mahusiano ya nje vodacom akifungua bonanza la waandishi wa habari mkoa wa kagera katika viwanja vya gymkana bukoba mjini,bonanza  hilo limejumuisha waandisi wa habari wa magazeti,redio,television,na wapiga picha. bw salumu alieleza huduma mbalimbali zinazotolewa a vodacom na kueleza kuwa wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na vyombo vya habari nakatika mafanikio waliyoyapata ya kuwa na wateja wengi kuliko mtandao wowote na kutengeneza faida kuliko mtandao wowote.pia alieleza mchango wa vodacom katika jamii ni pamoja na vodacom kuamua kupambana na taizo la ugonjwa wa vistura unaowasumbua akina mama kwa kugharamikia matibabu yao,katika elimu wamekuwa akijenga vyumba vya madarasa nk, pia akaeleza namna walivyoamua kudhamini bonanza na kutoa zawadi na kupata chakula na vinywaji kwa pamoja,zaidi ya shilingi milioni tano zimetumika katika bonanza la waandishi wa habari mkoa wa kagera.
 Hiki ni kikosi cha timu ya electronic(television,redio na
 picha)katika picha ya pamoja kilicho toa
 fundisho na onyo kali la kufunga goli  2-1 timu ya printing
                        hiki ni kikosi cha printing kilichosalimu
 amri kwakufungwa na electronic 2-1
 kabla ya mpambano keptan wa timu
 ya electronic kulia jamal kalumuna jamco akisalimiana
 na kaptan wa printing kibuka
                                                              printing wakishangilia bao lao
 kaptan wa electronic jamco akishangilia bao
 alilofunga kitaalamu na kumuacha golikipa 
wa printing bw karunde akishangaa kilichotokea
                                                         matukio yakichukuliwa
                                                         kipindi cha mapumziko
 mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari 
mkoa wa kagera ndugu rwekamwa akitoa
 neno la shukrani kwa wadhamini
 meneja wa vodacom kanda ya ziwa ni koka akieleza 
huduma mbalibali, ufanisi wa kazi na 
wajibu wafanyakazi wa vodcom na kumjali mteja.
                                                    ukafika wakati wa kufukuza kuku
                                                         ilikuwa bonge la burudani
                                                               kuku akikata mbuga
                                hatimae mwandishi wa kasbante redio akaibuka kidedea
                                                      wababa nao wakamfukuza kuku
                                         pamoja na unene asikwambie mtu speed ya hatari
                                                   joas kaijage akaibuka kidedea
                                                                    ilikuwa poa asikwambie mtu
                                   vipaji,vya watoto wimbo wa diamond palikwa apatoshi
                                                             kijana bahati akaibuka mshindi
                                           kijana akapewa zawadi kutoka vodacom
                                                                 wazee katika kusakata twist
                                                ponsian kaiza wa star tv akaibuka kidedea zawadi 20'000
                                          wakaingia waandishi wa kike katika taarabu
                                                  hapa picha inakua hivi live inakuaje
                                                wakaingia waandishi wa kiume bolingo si mchezo
                                         kijana wa kwanza kulia tofau saidi akaibuka kidedea 20,000
                                          mabalozi wa vodacom nao wakatoa burudani
                               ikavutwa kamba timu ya electronic ikashinda zawadi laki moja
                                                                      shangwe
 katibu wa chama cha waandishi wa habari
 mkoa wa kagera akitoa neno la shukrani kwa vodacom
 zawadi tofau wa kasibante redio alijinyakulia
 kitita cha 80,000 kwa kukimbia,na muziki
                            jane rwomile zawadi ya kucheza taarabu 20,000
                                       jamco l50'000 kwa ajili ya washindi timu ya electronic
                        kibuka 75.000 kwa ajili ya timu ya printing washindi wa pili
 picha ya pamoja waandishi wa habari magazeti,redio, 
television,bloggers wakiwa na viongozi wa vodacom

       
 ni kupongezana viwanja vya bukoba club baada ya bonanza

waliotembelea blog