Tuesday, August 5, 2014



Washiriki wa shindano la Redd’s miss Kinondoni 2014 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye Hotel ya Picolo jijini Dar es Salaam, Jumla ya warembo 20 wapo mazoezini kujiandaa na shindano litakalofanyika ijumaa 15/08/2014 katika Fukwe za Escape One kwa kiingilio cha 10,000 na 30,000 kwa VIP.
Wanyange 20 kuchuana jukwaani kutafuta mshindi
Warembo wakiwa kwenye picha ya pamoja
Fainali wiki ijayo Agost 15



BENDI mpya inayotamba kwa sasa hapa nchini na ambayo imechukuwa tuzo mbalimbali za muziki hapa nchini (MASHUJAA BAND) Alhamisi 14 inatarajia kushuka hapa Mjini Bukoba katika ukumbi wa LINA'S NIGHT CLUB kuwapa burudani wakazi wa Mji huu na vitongoji vyake.
Akiongea na Mwaandishi wa Bukobasports.com Mc Jerry kwa jina maarufu hapa Bukoba amesema Bendi hiyo itatua hapa Mjini kwa ajili Burudani ya Nguvu na pia alifafanua kuwa Tangu Bendi hii ianzishwe ni Onesho lao la kwanza hapa Bukoba hivyo anawataka Wakazi kuingia kwa wingi kushuhudia Bendi hiyo ikifanya mambo yake live Jukwaani.
Alisema kuwa bendi nzima ya Mashujaa inatarajiwa kutia timu mjini hapa wakiwa na wanamuziki wake wote ambapo aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni pamoja na Chaz Baba.
Alifafanua zaidi kuwa Bendi hii imedhamiria ‘kufunika’ katika onyesho hilo na wamejipanga kufunika bendi zote ambazo zimeshawahi kufanya onyesho katika Mji huu wa Bukoba
kwani bendi hii ina historia nzuri katika muziki wa Tanzania haswa katika maonyesho yao mbalimbali ambayo wameshayafanya hapanchini.
Aidha Mc Jerry alisema kuwa ameamua kuwaletea wakazi hawa wa Mji wa Bukoba


bendi hii kwani bendi hii imekuwa inafanya vyema katika tasnia hii ya muziki wa dansi ambapo alifafanua kuwa kwa mwaka huu bendi hii ya Mashujaa inashikilia tuzo tano za muziki hapa nchini.

Alitaja kiingilio cha shindano hili ni shilingi10000 kwa kila mmoja huku akiwasihi wakazi wa mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwaa kwa kuimba pamoja na kucheza.


Mashindano ya Jumuiya ya Madola yamemaliza katika mji wa Glasgow nchini Scotland huku mji huo ukimiminiwa sifa kem kem na Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Mashindano ya Jumuiya ya Madola Mike Hooper kwa kuandaa mashindano hayo.

Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua medali za dhahabu 19.
Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.


Mashindano ya Jumuiya ya Madola yamemaliza katika mji wa Glasgow nchini Scotland huku mji huo ukimiminiwa sifa kem kem na Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Mashindano ya Jumuiya ya Madola Mike Hooper kwa kuandaa mashindano hayo.

Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua medali za dhahabu 19.
Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.


Wayne Rooney (kushoto) akiwa amebeba Kombe na mwenzie baada ya kuifunga Timu ya Liverpool bao 3-1 usiku wa kuamkia leo
Kipndi cha pili Dakika ya 55 Wayne Rooney aliwasawazishia bao kwa kufanya 1-1 na baadae katika dakika ya 57 Juan Mata liwapachikia bao la kuongoza na kufanya 2-1 dhidi ya Majogoo
Liverpool.

Dakika ya lala salama ya 88, Jesse Lingard anaongeza bao la tatu na kufanya 3-1 dhidi ya majogoo Liverpool. Bao hilo la Jesse lilihitisha ungwe hiyo ya pili United wakiibuka na ushindi na kujinyakulia kombe la kwanza chini ya uongozi mpya wa Kocha Lous Van Gaal.Fainali hii ni ya kipekee sana!!!Nyimbo za Mataifa yao ziliimbwa kabla ya mtanange kuanza...
View image on TwitterTayari mtanange kuanza...Kikosi cha LiverpoolSteven Gerard akimfunga kipa wa United kwa mkwaju wa penati.

Gerrard mapema aliwapachikia Liverpool bao kwa mkwaju wa penati na hapa alikuwa akipongezwa na  Henderson na Lambert 
 Rooney akisawazisha bao na kufanya 1-1 baada ya kupata krosi safi kutoka kwa  Hernandez's scross

Kutangulia siyo kufika: Rooney akiwawasha Liverpool

Mtajiju: Rooney  akishangilia bao lake huko Miami baada ya kusawazisha

Juan Mata hakuchelewesha mambo ndani ya dakika 2 alitupia bao katika dakika ya 57 kipindi cha pili.

 Mata akipongezwa na Wanaunited wenzake!

 Gerrard akitupia

Wachezaji wa  United wakijiuliza kwa nini!! baada ya kufungwa penati!!

Rooney

Kocha Van Gaal
Rooney chupucupu afunge bao hapa kwenye frii kiki

Hernandez mbele ya  SkrtelShaw

 Ander Herrera akimwangaisha  Jordan Henderson

Juan Mata tena na Martin Skrtel

Antonio Valencia

 Ashley Young akichuana na Glen Johnson

Ashley Young na Glen JohnsonLuke Shaw wa Man United akiendesha..
Raheem Sterling akichuana na Phil Jones
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED:
De Gea, Evans (Blackett 46), Smalling, Jones, Valencia (Shaw 9), Herrera (Lingard 78), Fletcher (Cleverley 46), Young, Mata (Kagawa 68), Rooney [captain], Hernandez (Nani 68).
Subs: Lindegaard, Amos, Johnstone, M Keane, James, Zaha, W Keane.
Goals: Rooney (55), Mata (57), Lingard (88)
Booking: Shaw (52).


LIVERPOOL: Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho (Toure 74), Gerrard [captain] (Lucas 62), Allen (Ibe 62), Henderson, Coutinho (Peterson 77), Lambert (Can 62), Sterling.
Subs: Jones, Coates, Coady, Phillips, Robinson, Suso.
Goal: Gerrard (14, pen)
Attendance: 51,104


Julio Grondora enzi za uhai wake

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.

Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).

Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.

Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.


Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.


Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo


BAADA ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amezugumza na MPENJA BLOG mchana huu na kueleza kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.
“Tunachosema ni kwamba klabu inapokuwa bingwa sio kwamba kuna kanuni zinailazimisha kucheza mashindano. Kwahiyo ikiona kwamba haijajipanga kwa mashindano, bado ina haki ya kutuandikia sisi kuwa hawapo tayari kushiriki mashindano na tunatafuta timu nyingine inayokwenda kwenye mashindano,” alifafanua Wambura.
Hata hivyo, Shirikisho la soka Tanzania limeichagua Azam fc kwenda kushiriki mashindano hayo na tayari limeshawaandikia barua baada ya mawasiliano ya pande zote kwenda barabara.
“Ni kweli , CECAFA waliwapa Yanga muda wa kuthibitisha kikosi chao, lakini muda umekwisha, maana yake sasa CECAFA wamefanya uamuzi wa kuwatoa katika michuano ya Kagame kwa uamuzi wa kupeleka kikosi cha pili au mchanganyiko kinyume na kanuni za mashindano. Na hii ililenga kupunguza hadhi ya mashindano,” alisema Wambura.
“Kwahiyo CECAFA wakaiondoa Yanga na badala yake sisi tukawaomba watupe hiyo nafasi kwa kutafuta timu nyingine ambayo itatuwakilisha kwa maana ya Tanzania bara, tukasema lazima tuwe na uwakilishi kwenye mashindano hayo na tumewapa nafasi Azam.”
“Tumeshawaandikia barua baada ya kuzungumza nao na ndio watatuwakilisha kwenye mashindano yanayotarajia kuanza Agosti 8
“Cha msingi cha kuelewa ni kwamba kila mashindano yana kanuni zake na taratibu zake. Kila mashindano lazima uwe na sifa ya kushiriki, ukishakuwa na sifa, unatakiwa kufuata kanuni kama zinavyoelezeka”
Aidha, Wambura alisema TFF hawahusiki kwa lolote kuhusu maamuzi hayo kwasababu wao sio sehemu ya waandaaji wa mashindano.

“Sisi kama TFF hatupo kwenye hayo mashindano na waliohusika kuwatoa Yanga ni waandaji wa mashindano, kwahiyo sisi hatuna lingine la kufanya isipokuwa kuwakumbusha watu kuwa wanapokwenda kucheza mashindano wazingatie kanuni na wasitunge kanuni zao, wanatakiwa kufuata kanuni za waandaaji”.

Teaming up: Cristiano Ronaldo and James Rodriguez give the thumbs up at Real Madrid training 
Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini Hispania.
Rodriguez  alijiunga na mabingwa hao wa Ulaya kutokea klabu ya Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya kuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu na kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa mashindano.
Baada ya mapumziko akitokea kombe la dunia kuiwakilisha Colombia, nyota huyo aliripoti katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Valdebebas HQ ambapo aliungana na wenzake.
Close ball control: Ronaldo works with the football during training at Valdebebas
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Keep it up: Real stars (from left) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez and Raphael Varane during the session
Ona kitu hicho: Nyota wa Real  (kutoka kushoto) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez na Raphael Varane wakati wa mazoezi ya Real Madrid

waliotembelea blog