Tuesday, August 5, 2014


Jan Poulsen alirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars mwaka 2010



TAIFA Stars imekuwa timu ya ‘Tia maji Tia maji’ kwa miaka mingi, lakini kwasasa kuna haja ya kuanza upya kuijenga timu hii.
Kumbukumbu: mwaka 1980 Stars ilishiriki fainali za mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Nigeria.
Kuanzia hapo mpaka leo hii, imekuwa ndoto ya mchana kwasababu ya mipango mibovu katika soka la Tanzania.
Mwaka 2009, Stars ilishiriki mashindano mengine makubwa ya mataifa ya Africa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN, nchini Ivory Coast.
Wakati inakwenda Ivory, Stars chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilionekana kufufuka na kulikuwa na morali kubwa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki kwa ujumla.
Baada ya kuondoka kwa Maximo mwaka 2010, TFF ilimteua Mdenish Jan Poulsen. Mzee huyu alikuwa na mipango mizuri, lakini ilionekana kushindikana kutokana na uharaka wa Watanzania.
Ni kweli Stars ilishuka kiwango ukilinganisha na kipindi cha Maximo, lakini Jan alikuwa na mipango ya muda mrefu, jambo ambalo ni adui wa Watanzania wengi.
Njia za mkato zinapenda kweli, eti leo hii mtu anatafakari kufuzu kombe la dunia au Afcon 2015, kwa mipango ipi?
Siku moja wakati anatoa kozi kwa makocha wa Tanzania alichora mchoro katika ubao.
Wote walioenda shule wanajua mbao za kuandikia wakati walimu wanafundisha zilivyo. Rudisha kumbukumbu.
Jan aliandika  pointi A chini kabisa ya ubao na akaandika pointi B juu kabisa ya ubao.
Akasema Tanzania ipo pointi A ambapo soka la Tanzania lipo. Hicho ni kiwango cha chini kabisa, lakini soka hilo linatakiwa kufikia pointi B, ngazi au kiwango ya juu kabisa.
Mdenish huyo aliuliza swali, tunafikaje pointi B?. Akafafanua kuwa ili kufika pointi B, hapa katikati kuna kitu kinaitwa mchakato ‘Process’.
Huu mchakato unajumuisha kuandaa mipango sahihi, mfumo sahihi wa soka, hususani soka la vijana.
Jan alieleza kuwa ili kufanikiwa kufika Pointi B, lazima kuwekeza muda na fedha za kutosha kuandaa timu za vijana, miundo mbinu ya soka, kuandaa makocha wenye ueledi wa juu na kuwa na viongozi sahihi katika nafasi sahihi.
Kim Poulsen alirithi mikoba ya Mdenish mwenzake, Jan Poulsen kuinoa Taifa Stars

Wakati anayasema hayo, alionekana kugundua matatizo ya wachezaji wa Tanzania. Alipoondoka na kumuachia Kim Poulsen, mambo yalionekana kuwa poa, lakini ghafla watu wakasitisha programu za kim na kumleta Mart Nooij.
Siku Kim anaaga pala TFF, aliongea vitu vingi, lakini nilishika zaidi kitu alichosema ‘Things Takes Time’ (TTT). Hapa kocha huyu alimaanisha vitu vinahitaji muda. Soka linahitaji muda.
Lazima kuwa na uvumilivu unapojenga timu. Kwa maana yake yeye, Kim alikuwa anajenga timu na alikuwa na program ya muda mrefu hasa katika soka la vijana, lakini kutokana na uchu wa kutaka kufuzu AFCON 2015 akamtimuliwa.
Viongozi wa juu wa TFF walikaririwa mara kadhaa wakisema kwa vyovyote vile, kwa kumwaga damu uwanjani, lazima Taifa Stars iende AFCON 2015.
Tayari Kim alisema mapema kuwa malengo yake yalikuwa AFCON 2015 nchini Morocco na sio kombe la dunia 2014 au CECAFA Senior Challenge Cup 2014 nchini Kenya, lakini watu wakata mafanikio ya haraka haraka.
Mpira haulazimishwi. Lazima mipango sahihi iweke na uvumilivu uwepo.
Busara za Kim na Jan Poulsen si za kuziacha hata kidogo. Walikuwa na maana kubwa, tena ile ile aliyonayo Mart Nooij. Sema namna viongozi wanavyochukuliwa mambo kwa haraka ndio matokeo ya kule Msumbiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Enzi za Marcio Maximo akiifundisha Taifa Stars (2006-2010)

TFF wamekuwa wakijitahidi kuiandaa timu, kwa mfano mwaka huu waliweka kambi Botswana kuiwinda Msumbiji na kufanya mpango wa maboresho ya Taifa Stars ingawa kwa asilimia 500 ‘umefeli’.
Lakini tatizo ni lile lile na viongozi wanalijua kuwa aina ya wachezaji waliopo sasa wamekosa vitu vingi vya kimbinu na kiufundi kwasababu wengi wao walikosa misingi ya mpira enzi za utoto wao.
Nadhini ni lazima turudi nyuma na kuwekeza katika soka la vijana.
Unajua kwa mara ya kwanza nafasi nzuri zaidi ambayo Tanzania ilishika katika viwango vya FIFA? Hii ni mwaka 1965 ambapo ilishika nafasi ya 65.
Wachezaji wengi wa timu ya 1965 ndio walioipeleka Taifa Stars michuano ya mataifa ya Afrika 1980 nchini Morocco.
Asubuhi njema!

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog