Julio Grondora enzi za uhai wake
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia
salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio
Grondora.
Amesema
yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla
wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha
Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
Ameongeza
kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani
alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika
maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais
Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata
pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya
FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
cha msiba huo mzito.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
0 maoni:
Post a Comment