Wamekutana: Cristiano Ronaldo na James Rodriguez wakitoa dole kuashiria mambo 'supa' wakati wa mazoezi ya Real Madrid.
MWANASOKA BORA wa dunia, Cristiano Ronaldo amekutana na kijana mpya wa Real Madrid James Rodriguez katika mazoezi ya klabu hiyo mjini Madrid nchini Hispania.
Rodriguez alijiunga na mabingwa hao wa
Ulaya kutokea klabu ya Monaco kwa dau la paundi milioni 60 baada ya
kuonesha kiwango kikubwa katika fainali za kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu na kutwaa kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa
mashindano.
Baada ya mapumziko akitokea kombe la
dunia kuiwakilisha Colombia, nyota huyo aliripoti katika uwanja wa
mazoezi wa klabu hiyo wa Valdebebas HQ ambapo aliungana na wenzake.
Ronaldo akifanya mazoezi katika uwanja wa Valdebebas
Ona kitu hicho: Nyota wa Real (kutoka
kushoto) Ronaldo, Karim Benzema, Rodriguez na Raphael Varane wakati wa
mazoezi ya Real Madrid
0 maoni:
Post a Comment