Tuesday, August 5, 2014


BENDI mpya inayotamba kwa sasa hapa nchini na ambayo imechukuwa tuzo mbalimbali za muziki hapa nchini (MASHUJAA BAND) Alhamisi 14 inatarajia kushuka hapa Mjini Bukoba katika ukumbi wa LINA'S NIGHT CLUB kuwapa burudani wakazi wa Mji huu na vitongoji vyake.
Akiongea na Mwaandishi wa Bukobasports.com Mc Jerry kwa jina maarufu hapa Bukoba amesema Bendi hiyo itatua hapa Mjini kwa ajili Burudani ya Nguvu na pia alifafanua kuwa Tangu Bendi hii ianzishwe ni Onesho lao la kwanza hapa Bukoba hivyo anawataka Wakazi kuingia kwa wingi kushuhudia Bendi hiyo ikifanya mambo yake live Jukwaani.
Alisema kuwa bendi nzima ya Mashujaa inatarajiwa kutia timu mjini hapa wakiwa na wanamuziki wake wote ambapo aliwataja baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo kuwa ni pamoja na Chaz Baba.
Alifafanua zaidi kuwa Bendi hii imedhamiria ‘kufunika’ katika onyesho hilo na wamejipanga kufunika bendi zote ambazo zimeshawahi kufanya onyesho katika Mji huu wa Bukoba
kwani bendi hii ina historia nzuri katika muziki wa Tanzania haswa katika maonyesho yao mbalimbali ambayo wameshayafanya hapanchini.
Aidha Mc Jerry alisema kuwa ameamua kuwaletea wakazi hawa wa Mji wa Bukoba


bendi hii kwani bendi hii imekuwa inafanya vyema katika tasnia hii ya muziki wa dansi ambapo alifafanua kuwa kwa mwaka huu bendi hii ya Mashujaa inashikilia tuzo tano za muziki hapa nchini.

Alitaja kiingilio cha shindano hili ni shilingi10000 kwa kila mmoja huku akiwasihi wakazi wa mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi kuangalia bendi hii ambayo inawanamuziki wengi ambao wanajua kutawala jukwaa kwa kuimba pamoja na kucheza.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog