Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo
BAADA ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya
klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la
Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho
la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama
inaona haijajiandaa.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface
Wambura Mgoyo amezugumza na MPENJA BLOG
mchana huu na kueleza kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana
kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari
wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.
“Tunachosema ni kwamba klabu inapokuwa bingwa sio
kwamba kuna kanuni zinailazimisha kucheza mashindano. Kwahiyo ikiona kwamba
haijajipanga kwa mashindano, bado ina haki ya kutuandikia sisi kuwa hawapo
tayari kushiriki mashindano na tunatafuta timu nyingine inayokwenda kwenye
mashindano,” alifafanua Wambura.
Hata hivyo, Shirikisho la soka Tanzania limeichagua
Azam fc kwenda kushiriki mashindano hayo na tayari limeshawaandikia barua baada
ya mawasiliano ya pande zote kwenda barabara.
“Ni kweli , CECAFA waliwapa Yanga muda wa
kuthibitisha kikosi chao, lakini muda umekwisha, maana yake sasa CECAFA
wamefanya uamuzi wa kuwatoa katika michuano ya Kagame kwa uamuzi wa kupeleka
kikosi cha pili au mchanganyiko kinyume na kanuni za mashindano. Na hii ililenga
kupunguza hadhi ya mashindano,” alisema Wambura.
“Kwahiyo CECAFA wakaiondoa Yanga na badala yake
sisi tukawaomba watupe hiyo nafasi kwa kutafuta timu nyingine ambayo
itatuwakilisha kwa maana ya Tanzania bara, tukasema lazima tuwe na uwakilishi
kwenye mashindano hayo na tumewapa nafasi Azam.”
“Tumeshawaandikia barua baada ya kuzungumza nao na
ndio watatuwakilisha kwenye mashindano yanayotarajia kuanza Agosti 8
“Cha msingi cha kuelewa ni kwamba kila mashindano
yana kanuni zake na taratibu zake. Kila mashindano lazima uwe na sifa ya
kushiriki, ukishakuwa na sifa, unatakiwa kufuata kanuni kama zinavyoelezeka”
Aidha, Wambura alisema TFF hawahusiki kwa lolote
kuhusu maamuzi hayo kwasababu wao sio sehemu ya waandaaji wa mashindano.
“Sisi kama TFF hatupo kwenye hayo mashindano na waliohusika kuwatoa Yanga ni waandaji wa mashindano, kwahiyo sisi hatuna lingine la kufanya isipokuwa kuwakumbusha watu kuwa wanapokwenda kucheza mashindano wazingatie kanuni na wasitunge kanuni zao, wanatakiwa kufuata kanuni za waandaaji”.
0 maoni:
Post a Comment