Tuesday, February 21, 2017



Kocha wa Man United Jose Mourinho kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Europa League dhidi ya St Etienne ya Ufaransa, ameulizwa maswali kuhusu hatma ya nahodha wa Man United Wayne Rooney kama ataondoka katika timu hiyo au atabaki.
Jose Mourinho ambaye inaaminika ndio anaweza akafanya Rooney aondoke mwisho wa msimu kama inavyoripotiwa au akabaki, ameshindwa kuweka wazi kama ataondoka staa huyo au atabaki, lakini amekiri kuwa hawezi kumlazimisha mchezaji kuhama.
“Kuhusu kuondoka unaweza kumuuliza mwenyewe kwa sababu hata mimi siwezi kukuhakikishia kama nitakuwa hapa wiki ijayo, sasa nawezaje kukuhakikishia kuwa mchezaji ataendelea kuwepo msimu ujao, kama Rooney ataamua kuondoka sio kwa sababu mimi nataka aondoke”

“Hicho ndio ninachoweza kukuhakikishia sitaweza kulazimisha legend wa Club hii kwenda sehemu nyingine, hivyo unaweza kumuuliza Rooney mwenyewe kama angependa kumaliza soka lake katika timu hii? lakini mimi nina furaha kuwa nae katika timu”

waliotembelea blog