Tuesday, July 5, 2016
6:52 AM
Unknown
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.
Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.
Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.
Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.
"Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
"Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi," alisema Chande.
Nae mlezi wa kituo hicho, Bi. Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.
Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande.
"Tangu walipotufahamu wamekuwa wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia," alisema Bi. Kuruthum.
Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao wanasoma.
Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande akimkabidhi Cherehani, mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf. Wa tatu kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu wakiwa na wafanyakazi wengine wa Multichoice Tanzania.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akimpongeza mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf baada ya kukabidhiwa misaada na Multichoice Tanzania.
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akiwaelekeza jambo watoto wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwonekano wa vitu vilivyotolewa na Multichoice Tanzania kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina.
6:43 AM
Unknown
DIRISHA la Uhamisho la Ligi Kuu England limefunguliwa rasmi Julai 1 na litafungwa Agosti 31.
Klabu kadhaa zimeshavamia Soko na kununua na pia kuuza Wachezaji.
PATA DILI ZILIZOKAMILIKA HADI SASA:
AFC Bournemouth
MPYA
Emerson Hyndman (Fulham) Bure
Nathan Ake (Chelsea) Mkopo
Lys Mousset (Le Havre) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Sylvain Distin (Ameachwa)
Tommy Elphick (Aston Villa) ADA HAIKUTAJWA
Matt Ritchie (Newcastle United) ADA HAIKUTAJWA
Arsenal
MPYA
Granit Xhaka (Borussia Monchengladbach) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Mikel Arteta (Ameachwa)
Tomas Rosicky (Ameachwa)
Mathieu Falmini (Ameachwa)
Daniel Crowley (Oxford United) Mkopo
Burnley
MPYA
Robbie Leitch (Motherwell) Bure
Jamie Thomas (Bolton Wanderers) Bure
Chelsea
MPYA
Meneja: Antonio Conte
NJE
Lewis Baker (Vitesse Arnhem) Mkopo
Nathan Ake (Bournemouth)
Crystal Palace
MPYA
Andros Townsend (Newcastle United) Pauni Milioni 13
NJE
Dwight Gayle (Newcastle United) Pauni Milioni 10
Everton (evertonfc.com)
MPYA
Meneja: Ronald Koeman
Bassala Sambou (Coventry City)
Chris Renshaw (Oldham Athletic) ADA HAIKUTAJWA
Maarten Stekelenburg (Fulham) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Steven Pienaar (Ameachwa)
Leon Osman (Ameachwa)
Tony Hibbert (Ameachwa)
Leicester City
MPYA
Ron-Robert Zieler (Hannover 96) ADA HAIKUTAJWA
Luis Hernandez (Sporting Gijon) Bure
Raul Uche Rubio (Valencia) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Andrej Kramaric (Hoffenheim) ADA HAIKUTAJWA
Klabu kadhaa zimeshavamia Soko na kununua na pia kuuza Wachezaji.
PATA DILI ZILIZOKAMILIKA HADI SASA:
AFC Bournemouth
MPYA
Emerson Hyndman (Fulham) Bure
Nathan Ake (Chelsea) Mkopo
Lys Mousset (Le Havre) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Sylvain Distin (Ameachwa)
Tommy Elphick (Aston Villa) ADA HAIKUTAJWA
Matt Ritchie (Newcastle United) ADA HAIKUTAJWA
Arsenal
MPYA
Granit Xhaka (Borussia Monchengladbach) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Mikel Arteta (Ameachwa)
Tomas Rosicky (Ameachwa)
Mathieu Falmini (Ameachwa)
Daniel Crowley (Oxford United) Mkopo
Burnley
MPYA
Robbie Leitch (Motherwell) Bure
Jamie Thomas (Bolton Wanderers) Bure
Chelsea
MPYA
Meneja: Antonio Conte
NJE
Lewis Baker (Vitesse Arnhem) Mkopo
Nathan Ake (Bournemouth)
Crystal Palace
MPYA
Andros Townsend (Newcastle United) Pauni Milioni 13
NJE
Dwight Gayle (Newcastle United) Pauni Milioni 10
Everton (evertonfc.com)
MPYA
Meneja: Ronald Koeman
Bassala Sambou (Coventry City)
Chris Renshaw (Oldham Athletic) ADA HAIKUTAJWA
Maarten Stekelenburg (Fulham) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Steven Pienaar (Ameachwa)
Leon Osman (Ameachwa)
Tony Hibbert (Ameachwa)
Leicester City
MPYA
Ron-Robert Zieler (Hannover 96) ADA HAIKUTAJWA
Luis Hernandez (Sporting Gijon) Bure
Raul Uche Rubio (Valencia) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Andrej Kramaric (Hoffenheim) ADA HAIKUTAJWA
3:51 AM
Unknown
Taarifa za
awali ambazo zimeripotiwa hivi punde ni kuhusu ajali
iliyohusisha mabasi mawili, Kamanda polisi mkoa wa Singida, Thobias
Sedoyeka amesema ajali ya basi namba T 531 BCE likitokea Dar es salaam
kwenda Kahama na T 247 lililokuwa linatoka kahama kwenda Dar es salaam
yote ya kampuni moja ya City Boys yamegongana uso kwa uso na kusababisha
vifo vya watu 24 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)