Sunday, July 27, 2014

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AM 
Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann Center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambaye pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo hizo
Habari njema za  ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja wake Babu Tale ambaye nae kahudhuria tuzo hizi Marekani ala ametuma ujumbe mfupi wa simu  akisema Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.
Diamond akihojiwa muda mfupi baada ya kushinda tuzo AFRIMMA
Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.01 AM 
lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.33 AM
Endelea kufuatilia  millardayo.com  ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.Habari hii ni  kwa hisani ya

Majaji wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa washiriki wa kundi hilo
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katikati wakiwasikiliza washiriki wa kundi la kwanza wanavyojielezea kabla ya filamu fupi waliyochezwa kuonyeshwa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wiki iliyopita
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiangalia filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa makumbusho kabla ya kuanza kutoa hukumu kwa washiriki ni nani anatoka na nani anabaki.
Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
  Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
 Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
 Mshiriki Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
 Washiriki walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
 Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka
 Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
 Hatimaye Mshiriki Isalito Isaya Akaweza kurudi ndani ya Mjengo wa TMT kutokana na Kura zake kumzidi Mshiriki mwenzie Pendo ambaye aliweza kuaga mashindano hayo kutokana na kura kuwa chache
Baadhi ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati) ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa chache.Picha Zote na Josephat Lukaza

Na Josephat Lukaza – Proin Promotions Limited – Dar Es Salaam.

Hatua ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake na uzuri wake pia.

Mshiriki mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza  kuchomwa na jua la utosi lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.

Shindao la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini zaidi.
Hatimaye wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki kwa kutumia simu zao za mkononi.

Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno “TMT” ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678



DSC_0145
Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba akitoka kukagua jukwaa lenye hadhi ya kimataifa la Ebony FM kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viunga vya Samora mkoani Iringa.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
DSC_0455
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga wakiwasili kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio inayowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 iliyozinduliwa rasmi jana mkoani humo.
DSC_0514
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari wakiwemo Shule ya wasichana Iringa wakiendelea kumiminika kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
DSC_0179
Stella Shubi kutoka Clouds Media (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika kwenye viwanja Samora mjini Iringa.
DSC_0835MC wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio B 12 kutoka Clouds FM Redio ambao ndio waratibu wa uzinduzi wa kampeni hiyo akiwa na mtoto aliyeashangaza umati wa vijana waliofurika kwenye uzinduzi huo baada ya kujibu swali ambalo hawakutegemea angelijibu kutokana na umri wake.
DSC_0591 
Meza Kuu, Kutoka kulia ni Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu pamoja na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu.
DSC_0596 
Baadhi ya Mameneja wa Redio 10 za Jamii zitakazokuwa zikirusha vipindi vya SHUGA Redio vitakavyoanza kurushwa rasmi tarehe 2 Agosti mwaka huu wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
DSC_0348 
Kikundi cha Wazalendo a.k.a Makhirikhiri wa Bongo kutoka Mtwivila Iringa wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
DSC_0368Mohamed Omari kwa jina la usanii Sam wa Wazalendo Group kutoka mjini Iringa akito burudani za nyimbo za Makhirikhiri kwa staili ya aina yake huku akiwa na Nyoka mdomo kwenye sherehe za uzinduzi huo.
DSC_0485Mwanafunzi Calist Hermet wa kidato cha Sita kutoka shule ya Sekondari Tosamaganga akiimba wimbo wenye kuhamasisha matumizi ya Kondomu na upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa vijana huku akipewa sapoti na baadhi ya wanafunzi wenzake katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0482Kutoka kushoto B Dozen a.k.a B12, Shadee pamoja na Stella Shubi wakiwakilisha Clouds FM Redio ikiwa ni miongoni mwa Redio zitakazokuwa zikirusha vipindi vya kampeni ya SHUGA Redio kupitia kipindi cha Bongo Fleva kinachopendwa kusikilizwa na vijana wengi katika Redio hiyo.
DSC_0535Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye uzinduzi huo.
DSC_0541Afisa Programu kutoka UNESCO, Courtney Ivins (kushoto) na Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu wakiwa kwenye jukwaa kuu ndani ya viwanja vya Samora mjini Iringa.
DSC_0609Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhiria uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0520Mwanadada Shadee kutoka CLOUDS Media akipata picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi Calist Hermet wa shule ya Sekondari Tosamaganga.
DSC_0426Kwenye moja na mbili alihusika DJ Zero kutoka CLOUDS FM Redio.
DSC_0398Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi na mashirika mbalimbali walijumuika kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0381Baadhi ya watoto wa mjini Iringa waliokusanyika uwanjani hapo kushushudia uzinduzi huo.
DSC_0418
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari mkoani Iringa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0602
DSC_0741Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akizindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio ambapo amewaasa Vijana kuzingatia matumizi sahihi ya Kondomu na upimaji wa VVU ili kuzitambua afya zao mapema na kuepukana na maambukizi mapya ya VVU.
DSC_0757Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amesema Lengo kuu la kampeni ni kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana wa umri wa kubalehe kupitia vyombo vya habari na kuwafikia kwa ujumbe mahususi kuhusu upimaji wa hiari na ushauri nasaha na ngono salama. Kampeni inakusudiwa kuchochea vijana walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi waweze kutafuta na kuziendea huduma zilizopo.
Bi. Jenkins aliongeza kuwa kutakuwa na mfululizo wa vipindi 12 vya kuigiza wenye muda wa dakika nane umeelezea maisha ya vijana wanne (Sofia, Fally, Amina na Kavis) kuwakilisha vijana wa umri wa miaka 15 – 24. Simulizi iliyopo inahusu ndoto, chaguzi, marafiki, mapambano ya changamoto za kimaisha katika Dunia, ambayo UKIMWI ni tishio kubwa.Simulizi hizi kwa ujumla wake zinajikita kwenye somo la mbinu za upimaji wa VVU na ushauri nasaha, matumizi ya kondomu katika mahusiano ya muda mrefu , Kinga, unyanyasaji wa kijinsia na kingono, unywaji pombe na athari za kuwa na wapenzi wengi zinazopelekea kupata maambukizi ya UKIMWI.
DSC_0765Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akimpongeza Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins (kulia) kwa risala nzuri wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu.
DSC_0694Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Iringa, Bw. Owen Wimbo miongoni mwa wadhamini wa kampeni hiyo akizungumza machache na wakazi wa Iringa, Vijana na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
DSC_0706 
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu, akizungumza na vijana waliohudhuria uzinduzi huo ambapo aliwaasa kutouza mechi kusubiri muda muafaka na kuzingatia zaidi masomo sanjari na kuepuka kufanya ngono zembe.
DSC_0707 
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu akisikiliza majibu kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za sekondari mkoani Iirnga waliopata nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huo.
DSC_0770Mgeni rasmi akiwa ameungana na wasanii wa Bongo Flava pamoja na meza kuu kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0774 
Sasa imezinduliwa rasmi…..!
DSC_0778
DSC_0619 
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari mkoani Iringa wakitumia mbio kutoka kwenye majukwaa yao kusogea uwanja kushuhudia burudani za wasanii wa Bongo Flava Izo Business na Ben Paul waliopamba uzinduzi wa mradi huo jana mkoani Iringa.
DSC_0653
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Ben Paul akitoa burudani ya aina yake iliyoambatana na ujumbe mahususi wa kuhamasisha vijana kupima afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio ulioanyika jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
DSC_0931
DSC_0679 
Umati wa vijana na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Iringa wakishuhudia burudani za wasanii maarufu wa Bongo Flava waliosinfdikiza uzinduzi huo.
DSC_0685
DSC_0793 
Pichani juu na chini ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini anayejulikana kama Izo Business akitoa burudani kwa Vijana na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
DSC_0815
DSC_0829George Magesa kutoka UNICEF (katikati) akipata ukodak na Msanii wa Bongo Fleva nchini Ben Paul pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM Redio B Dozen a.k.a B 12.
DSC_0268Baadhi ya wanafunzi wa Kituo cha Upendo mjini Iringa wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye chumba maalum kwa ajili kupima Virusi vya Ukimwi bure wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Radio uliofanyika kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
DSC_0274Mtaalamu kutoka AMREF akichukua vipimo vya damu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa kituo cha Upendo mjini Iringa aliyejitolea kupima kwa hiari Virusi vya Ukimwi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) sambamba na Redio Jamii 10 nchini Tanzania wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
DSC_0175 
Vijana wa kiume nao walihamasika kupima afya zao bure bila malipo.

waliotembelea blog