Tuesday, June 2, 2015


Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amekanusha habari hizo.
Katika Msimu wake wa kwanza na Chelsea ambao ulimalizika Majuzi, Costa alipiga Bao 20 za Ligi Kuu England na kuiwezesha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa.
Costa, ambae alijiunga na Chelsea mwanzoni mwa Msimu huu uliokwisha kwa Dau la Euro Milioni 40, hakucheza vizuri awamu ya pili ya Ligi baada ya kuundamwa na Majeruhi na Kifungo.
Akiongea hii Leo baada ya Chelsea kuifunga Sydney Bao 1-0, Mourinho alitamka: "Yeye ni Mtu anaefurahisha kwenye Timu yetu.
Ana furaha, anachekesha na anafurahia kila kitu. Kama hiyo ni kutokuwa na furaha Klabuni basi mie nasikia raha. Yeye hakufurahishwa na habari hizo."
Kwenye Mechi hiyo na Sydney FC huko Nchini Australia, Costa alicheza Dakika 40 za Kipindi cha Kwanza lakini bao pekee na la ushindi lilifungwa na Loic Remy.

Licha ya kufunga Bao 20 kwenye Ligi, Diego Costa hakufunga hata Bao moja kwenye Mashindano mengine ambayo Chelsea ilifika mpaka Fainali ya
Kombe la Ligi, Capital One Cup, na kutwaa Kombe na pia kucheza Mechi 7 za UEFA CHAMPIONS LIGI.


Klabu ya Manchester United inaamini iko katika nafasi nzuri ya kumsajili Dani Alves kutoka Barcelona iwapo kocha Louis Van Gaal anataka kumsajili beki huyo wa kulia.
Alves atakuwa hana mkataba mwishoni mwa msimu huu na Barcelona iko tayari kumwachilia beki huyo wa miaka 32 kuondoka baada ya mechi ya fainali ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Juventus siku ya jumamosi mjini Berlin.
Klabu ya PSG pia inamuania Alvez ijapokuwa kocha wake Laurent Blanc anaamini mchezaji huyo bado anataka kusalia Barcelona.
Lakini maoni ya Old Trafford ni kwamba Alvez hangependelea kujiunga na PSG.
Van Gaal anapanga kumsajili beki wa kulia.Licha ya umri wake mkubwa ukosefu wa fedha za uhamisho zinamfanya mchezaji huyo kuwa muhimu.

Mchezaji huyo wa Brazil anapokea kitita cha pauni 120,000 kwa wiki, fedha ambazo United inaweza kuzilipa bila kutoa jasho.


Sepp Blatter, ambae alikuwa Rais wa FIFA kwa Miaka 17, ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Uamuzi huu unafuatia Shirikisho hilo la Soka Duniani kuandamwa na kashfa ya rushwa ambayo ilipamba moto baada ya Marekani kufungua Mashitaka kwa Maafisa kadhaa wa juu wa FIFA.
Blatter amesema ataitisha haraka iwezekanavyo Kongresi ya FIFA ili kuchagua Rais mpya baada ya yeye kukiri hana sapoti ya kila Mtu kufuatia na kusakamwa na Skandali hiyo.

Akitangaza uamuzi huo, Blatter, ambae Ijumaa iliyopita alichaguliwa kwa Kipindi cha 5 cha kuwa tena Rais wa FIFA, alisema: "Nimefikiria sana kuhusu Urais wangu na Miaka 40 ya FIFA katika maisha yangu. Naipenda FIFA kupita kitu chochote na nataka kufanya vyema. Niliamua kusimama tena kupigania Urais kwa nia ya kuleta mambo mapema katika Soka. Lakini uchaguzi wangu unaelekea haungwi mkono na kila Mtu. Ndio maana nitaitisha KIkao cha Dharura ili kunibadili na sitagombea."

Hadi hapo Kikao hicho cha Dharura kitakapofanyika, Tarehe ambayo bado haijulikani, Blatter ataendelea kuwa Rais wa FIFA.
Kikao cha kawaida cha Kongresi ya FIFA kilitarajiwa kufanywa huko Mexico City, Mexico Mwakani Mei 16 lakini Blatter ametoboa hatafika wakati huo. 
Sepp Blatter



KWA MARA YA KWANZA SHOW YA AINA YAKE KATI YA WANA NDUGU WAWILI ALI NA ABDU KIBA ITAFANYIKA WASHINGTON DMV,JUMAMOSI HII PALE FIRE STATION 1, 8131,GEORGIA AVENUE,DOWN TOWN SILVER SPRING,VIP PACKAGE ZINAPATIKANA,FREE PARKING



Leo ni zamu ya Profesa Sospeter Muhongo kutangaza nia ya kuombwa kugombea urais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, kurithi mikoba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Profesa Muhongo anatangaza nia yake leo Mjini Musoma, kwenye Ukumbi wa Open University Hall, kuanzia saa 10 jioni.

MWILI WA MAREHEMU MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA WAPOKELEWA BUKOBA, MAJONZI YATANDA KWA WANABUKOBA.

Gari maalum kutoka Nchini Uganda lililobeba Mwili wa Mzee Samwel Ntambala Lwangisa ukiingia Bukoba. Picha na Innocent Rwezaula/Bukoba
Mwili wa Marehemu Samuel Ntambala Luangisa uliwasili usiku wa kumkia leo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Mauti yalimkuta akiwa Nchini Marekani na maziko yake itakuwa kesho jumatano june 3,2015. Wakati wa Uhai wake Marehe Samwel Luangisa aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kagera (ukiitwa ziwa magharibi), Aliwahi pia kuwa mbunge wa Bukoba Mjini, Meya wa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kitendaguro hadi mauti yalipomkuta.
Mtoto wa Marehemu Bi. Murungi
Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis KagashekiNi majonzi na huzuni





















waliotembelea blog