Warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014 leo wameingia
siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina
asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hii wamefanya mazoezi katika chumba
maalum cha mazoezi ‘Gym’, ungana na mpigapicha wa Father Kidevu Blog
katika picha mbalimbali za warembo hao katika kambi yao.
Tuesday, September 16, 2014
4:47 AM
Unknown
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.Viongozi wa Kagera Sugar
Ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu msimu huu.
WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wakijifua kwenye Uwanja wa Kagera Sugar hivi karibuni tayari kwa Ligi kuu Vodacom sep 20 mwaka huu. Kagera Sugar wataanza ufunguzi wa Ligi kuu Vodacom Ugenini na timu ya Mgambo JKT mkwakwani Mjini Tanga wikiendi hii.
Kocha huyo alisema: “Tuna imani na vijana wetu kuwa wanaweza kutufikisha tunapotaka, japokuwa ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu, lakini tutajitahidi kupigana ili kuweza kushika nafasi za juu”.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.
Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20 mwaka huu.
Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi karibuni
4:35 AM
Unknown
Msanii mwingine anaekuja vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva aitwaye Kadja ambaye anatamba na wimbo wake wa Maumivu niache akiimba pamoja na Linah.
Mkali wa Bongo Hip Hop Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua vilivyo juu ya jukwaa na la Fiesta.
Msanii wa Bongofleva,Kadja akiimba wimbo wake wa Maumivu niache mbele ya maelfu ya wakazi wa Tabora (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
Ilikuwa buruuudani ya kusambaza upendo wa kweli kwa wakazi wa Tabora ndani ya tamasha la Fiesta
Palikuwa hapatoshi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora,ambapo tamasha la Fiesta lilirindima.
Wasanii chipukizi kutoka Tabora nao walionesha umahiri wao jukwaani
Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliofika kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Subscribe to:
Posts (Atom)