Tuesday, September 16, 2014


Msanii mwingine anaekuja vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva aitwaye Kadja ambaye anatamba na wimbo wake wa Maumivu niache akiimba pamoja na Linah.

Mkali wa Bongo Hip Hop Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua vilivyo juu ya jukwaa na la Fiesta.

Msanii wa Bongofleva,Kadja akiimba wimbo wake wa Maumivu niache mbele ya maelfu ya wakazi wa Tabora (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.

Ilikuwa buruuudani ya kusambaza upendo wa kweli kwa wakazi wa Tabora ndani ya tamasha la Fiesta

Palikuwa hapatoshi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora,ambapo tamasha la Fiesta lilirindima.

Wasanii chipukizi kutoka Tabora nao walionesha umahiri wao jukwaani

Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliofika kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog