Mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Olimpia na Rangers ya Scotland ameuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa katika Parking za magari jijini La Ceiba Honduras, Arnold Peralta alikuwa likizo nyumbani kwao Honduras.
Kifo cha Arnold Peralta
ambaye anamudu kucheza nafasi ya kiungo kwa ufasaha kinachunguzwa na
maafisa usalama wa nchi hiyo, ila taarifa za awali zinaonesha kuwa Arnold Peralta alipigwa risasi sio na majambazi ila inasadikika ni watu wenye visasi lakini tukio bado linachunguzwa.
Headlines za kifo cha Arnold Peralta kupigwa risasi zinakuja ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka auwawe kwa risasi golikipa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa, ambaye nae alipigwa risasi na majambazi ambao walienda kufanya uharifu katika nyumba ya mpenzi wake.