Thursday, June 12, 2014

Alama ya chaki ya kupulizia (spray) ni moja ya ingizo jipya kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Tayari refa ameshaitumia mara ya kwanza kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia usiku wa kuamkia leo, pale refa alipochora kwa kupulizia na kuweka alama wapi wachezaji wasimame wakati wa kupigwa mpira wa adhabu (pichani chini), ili kuthibiti zogo la wachezaji, ama wapi mpira uwekwe kabla ya kupigwa. Chaki hiyo, ambayo huyeyuka baada ya dakika chache, ilianza kutumika mwaka jana kwenye kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ambapo huko Argentina na Brazil ilitumika kwa Misimu kadhaa iliyopita.


WENYEJI, Brazil, baada ya Sherehe ya Ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia iliyofana sana,walijikita Uwanjani na kucheza Mechi ya Ufunguzi kwa kuichapa Croatia Bao 3-1.
Croatia ndio waliotangulia kupata Bao kwenye Dakika ya 11 baada ya Krosi ya chini kutoka Winga ya Kushoto kumkuta Fulbeki wa Kushoto wa Brazil Marcelo ambae alitumbukiza Mpira wavuni bila kutegemea.
Aminia!!!! Oscar
Supastaa Neymar aliamsha sherehe Uwanja mzima na Nchi nzima ya Brazil baada ya kusawazisha kwenye Dakika ya 29 kwa Shuti la chinichini la Mguu wa Kushoto.

Kipindi cha Pili, Brazil walipewa Penati baada ya Beki wa Croatia, Lovren, kumwangusha Fred na Neymar kupiga Bao la Pili.
Huku Dakika zikiyoyoma na Croatia kujikakamua kutaka kusawazisha, kaunta ataki ya Brazil ilizaa Bao la Tatu kwa kazi njema na ya ufundi ya Oscar.
Neymar akipewa kadi ya njanoNeymar akifanyiwa ndivyo sivyo na Vedran wa CroatiaHapa ndipo palizaa penati, mkwaju uliopigwa na NeymarNeymar akifunga mkwaju wa penatiNeymar (kulia) akishangilia bao lake la pili na kufanya 2-1
Hakunaga! Neymar akishangilia...huku macho yote ya Brazil yakiwa kwake.......Oscar akimpelekesha VedranOscar akifunga bao la tatu katika dakika za lala salama3-1 Croatia wakijionea wenyewe 


Bao la pili la Brazil limefungwa tena na Neymar kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Croatia Dejan Lovren kumvuta jezi kwenye eneo hatari na Neymar kuachia mkwaju huo na kipa wa Croatia kuupangulia ndani lango lake na kufanya 2-1 dhidi ya Croatia.
Bao la tatu lilifungwa na Oscar katika daika za majeruhi kwenye dakika ya za nyongeza 90+1, Baada ya kupewa pasi na zikiwa zimeongezwa dakika 4. Na mpira kumalizika kwa Wenyeji  Brazil wakiwa washindi wa bao 3-1 dhidi ya Croatia. Brazil ndio walianza kujifunga bao mapema dakika ya 11 kupitia kwa Marcelo kujifunga bahati mbaya kwenye eneo hatari la kipa na Baadae dakika 29 Staa Neymar aliyekuwa ameisha pewa kadi ya njano, Dakika ya 29 aliwachomoka mabeki wa Croatia na kuisawazishia bao timu yake ya Brazil na kufanya 1-1 kwa kupewa pasi nzuri na Oscar.Wachezaji wa Brazil wakishangilia baada ya mchezaji wao nyota Neymar kusawazisha bao kwa kufanya 1-1.Mchezaji wa Croatia Vedran Corluka akishangilia bao lao la kwanza walilojifunga Brazil mapema dakika ya 11.Neymar scores the equaliser for Brazil
Bao la pili la Brazil limefungwa tena na Neymar kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Croatia Dejan Lovren kumvuta jezi kwenye eneo hatari na Neymar kuachia mkwaju huo na kipa wa Croatia kuupangulia ndani lango lake na kufanya 2-1 dhidi ya Croatia.Patashika za hapa na pale
Timu zote mbili Katikati ya Uwanja zikiwa tayari kwa kipute..Kombe la Dunia Brazil 2014 usiku huu.Mchezaji wa  Brazil David Luiz wakishikana vikali na mchezaji wa Croatia  Ivica Olic kwenye mchezo wa kwanza kundi  A unaondelea usiku huu...
Mashabiki wa Brazil kwenye uwanja wa  Sao Paulo Arena wakiishangilia timu yaoWachezaji wa Brazil wakiwa tayari kwa Wimbo wa Taifa

VIKOSI:
Brazil:
Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho, Gustavo, Hulk, Oscar, Neymar, Fred.
Subs: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.

Goal:Neymar 29  71pen, Oscar 90+1.

Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Lovren, Vrsaljko, Modric, Rakitic, Perisic, Kovacic, Olic, Jelavic.
Subs: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Brozovic, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.

Goal: Marcelo 11og.
Referee: Yuichi Nishimura (Japan)


You might also like:



Singer Jennifer Lopez, rapper Pitbull and Brazilian popstar Claudia Leitte bounced around the giant stage as they sang the official World Cup song 'We Are One (Ola Ola)' during the opening ceremony

Popstar Jennifer Lopez and rapper Pitbull performed to thousands of people at the Arena de Sao Paulo in Brazil this evening as the opening ceremony of the World Cup got underway

Superstar Jennifer Lopez sizzled in a sparkly green number as she performed to thousands of people at the official World Cup opening ceremony

Jennifer Lopez performed with rapper Pitbull ahead of the group A match between Brazil and Croatia, which is the opening game of the 2014 tournament
Jennifer Lopez wore a sparkling leotard as she sang the official FIFA World Cup song 'We Are One (Ole Ola)' alongside Pitbull and Claudia Leitte

J-Lo wows as she performs during the opening ceremony of the 2014 World Cup prior to the Group A match between Brazil and Croatia

Singer Jennifer Lopez was joined by rapper Pitbull and Brazilian pop star Claudia Leitte as the world's biggest football tournament commenced in Brazil this evening
Thousands of fans have gathered in the Arena de Sao Paulo in Brazil as the World Cup opening ceremony gets underway this evening ahead of the tournament's first match, which will be between Brazil and Croatia

Brazilian fans cheer during the World Cup opening ceremony



Meneja wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, anatarajiwa kuutumia Mfumo wa 4-2-3-1 lakini hamna uhakika kama Kiungo wa Chelsea, Oscar, anaweza kuanza kutokana na fomu yake kuporomoka hivi karibuni.
Lakini asipocheza Oscar, Mchezaji mwingine wa Chelsea, Willian, huenda akajaza nafasi yake.

Croatia wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Mario Mandzukic ambae yuko Kifungoni baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi yao ya Mchujo dhidi ya Iceland Mwezi Novemba.
Hata hivyo, Croatia wanae Eduardo, Mzaliwa wa Brazil, ambae ameungama akiwepo huenda akaimba Nyimbo za Taifa zote mbili ambazo huimbwa kabla Mechi kuanza.

Mvuto mkubwa kwa Duniani nzima ni kutaka kumwona Supastaa mdogo wa Brazil, Neymar, atachezaje na kama ataweza kurithi mikoba ya Lejendari Pele kwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na kuipa Nchi yake Taji.
Brazil v Croatia Preview

KOMBE LA DUNIA 2014: FIFA YATAJA MAREFA MECHI ZA JUMAMOSI! REFA BJORN KUIPERS KUCHEZESHA MCHEZO WA ENGLAND v ITALY JUMAMOSI HII...

FIFA imetangaza Marefa wa Mechi za Fainali za Kombe la Dunia za Jumamosi ikiwemo ile ya England v Italy ambayo amepewa Bjorn Kuipers wa Netherlands.
Colombia v Greece itasimamiwa na Refa wa USA Mark Geiger mwenye Miaka 39 ambae alianza Mechi za Kimataifa Mwaka 2008.

Refa Enrique Osses wa Chile, mwenye Miaka 40, atachezesha Mechi ya Côte d'Ivoire na Japan na alianza Mechi za Kimataifa Mwaka 2005

JUMAMOSI, JUNI 14, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
REFA
1900
Colombia v Greece
C
Estadio Mineirão
Mark Geiger [USA]
2200
Uruguay v Costa Rica
D
Estadio Castelão
Felix Brych [Germany]
0100
England v Italy
D
Arena Amazonia
Bjorn Kuipers [Holland]
0400
Ivory Coast v Japan
C
Arena Pernambuco
Enrique Osses [Chile]
Mtanange wa Uruguay v Costa Rica utakuwa chini ya Mjerumani Felix Brych, Miaka 38, ambae hivi Juzi tu alichezesha Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.
Refa wa England v Italy, Bjorn Kuipers, ni Mholanzi mwenye Miaka 41 ambae ni Mzoefu aliewahi kuchezesha Fainali 6 za Kimataifa ikiwemo ile ya Mwaka Jana ya Kombe la Mabara Uwanjani Maracana, Rio De Janeiro ambapo Brazil iliibonda Spain 3-0 na Mwezi uliopita ndie alikuwa Refa wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Lisbon, Ureno ambapo Real Madrid iliitwanga Atletico Madrid Bao 4-1.

waliotembelea blog