Thursday, June 12, 2014



Meneja wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, anatarajiwa kuutumia Mfumo wa 4-2-3-1 lakini hamna uhakika kama Kiungo wa Chelsea, Oscar, anaweza kuanza kutokana na fomu yake kuporomoka hivi karibuni.
Lakini asipocheza Oscar, Mchezaji mwingine wa Chelsea, Willian, huenda akajaza nafasi yake.

Croatia wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Mario Mandzukic ambae yuko Kifungoni baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi yao ya Mchujo dhidi ya Iceland Mwezi Novemba.
Hata hivyo, Croatia wanae Eduardo, Mzaliwa wa Brazil, ambae ameungama akiwepo huenda akaimba Nyimbo za Taifa zote mbili ambazo huimbwa kabla Mechi kuanza.

Mvuto mkubwa kwa Duniani nzima ni kutaka kumwona Supastaa mdogo wa Brazil, Neymar, atachezaje na kama ataweza kurithi mikoba ya Lejendari Pele kwa kuwika kwenye Kombe la Dunia na kuipa Nchi yake Taji.
Brazil v Croatia Preview

KOMBE LA DUNIA 2014: FIFA YATAJA MAREFA MECHI ZA JUMAMOSI! REFA BJORN KUIPERS KUCHEZESHA MCHEZO WA ENGLAND v ITALY JUMAMOSI HII...

FIFA imetangaza Marefa wa Mechi za Fainali za Kombe la Dunia za Jumamosi ikiwemo ile ya England v Italy ambayo amepewa Bjorn Kuipers wa Netherlands.
Colombia v Greece itasimamiwa na Refa wa USA Mark Geiger mwenye Miaka 39 ambae alianza Mechi za Kimataifa Mwaka 2008.

Refa Enrique Osses wa Chile, mwenye Miaka 40, atachezesha Mechi ya Côte d'Ivoire na Japan na alianza Mechi za Kimataifa Mwaka 2005

JUMAMOSI, JUNI 14, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
REFA
1900
Colombia v Greece
C
Estadio Mineirão
Mark Geiger [USA]
2200
Uruguay v Costa Rica
D
Estadio Castelão
Felix Brych [Germany]
0100
England v Italy
D
Arena Amazonia
Bjorn Kuipers [Holland]
0400
Ivory Coast v Japan
C
Arena Pernambuco
Enrique Osses [Chile]
Mtanange wa Uruguay v Costa Rica utakuwa chini ya Mjerumani Felix Brych, Miaka 38, ambae hivi Juzi tu alichezesha Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.
Refa wa England v Italy, Bjorn Kuipers, ni Mholanzi mwenye Miaka 41 ambae ni Mzoefu aliewahi kuchezesha Fainali 6 za Kimataifa ikiwemo ile ya Mwaka Jana ya Kombe la Mabara Uwanjani Maracana, Rio De Janeiro ambapo Brazil iliibonda Spain 3-0 na Mwezi uliopita ndie alikuwa Refa wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Lisbon, Ureno ambapo Real Madrid iliitwanga Atletico Madrid Bao 4-1.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog