Thursday, May 28, 2015


 Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa kukabidhiwa Matrekta kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
 Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink  akisalimiana mara baada ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino Komed, Isaya Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
  Mwigizaji wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa niaba ya waigizaji wa kundi la Origino Komedi  mara baada ya kukabidhiwa Funguo za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex Chalamila(Mackregani).
  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza na Vijana wa Kundi la Origino    Komedi mara baada ya kuwakabidhi funguo za Matrekta ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja waigizaji wa kundi la Origino  Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.



Chuck Blazer alikuwa mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA wakati alikuwa akifanya udukuzuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia Fifa kwa kipindi cha miaka miwili.

Kashfa za rushwa zinazoelezwa kwa kiasi kikubwa katika Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA, zilizotolewa Jumatano asubuhi wiki hii baada ya kukamatwa kwa maofisa saba wa Shirikisho hilo, ni za muda mrefu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, yote yalianza mwaka 2011, wakati Idara ya uchunguzi ya Marekani (FBI) ilifaulu kumshawishi Chuck Blazer kuwa afisa wake wa ujasusi. Chuck Blazer alikuwa mwanachama wa kamati tendaji ya FIFA tangu mwaka 1998 hadi mwaka 2013. Chuck Blazer alilitumikia Shirikisho la Concacaf, ambalo ni sawa ni Shirikisho la Soka Duniani FIFA.

Chuck Blazer alikuwa akifanya udukuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia FIFA kwa kipindi cha miaka miwili. Alikubali kuwafanyia kazi viongozi wa Marekani baada ya kugunduliwa na mamlaka ya kodi kwa kushindwa kulipa kodi kwa mamilioni ya fedha aliyopitisha mlango wa nyuma kwa kipindi cha miaka ishirini na moja akiwa kama Katibu mkuu mtendaji wa Concacaf, ambalo ni Shirikisho la Soka la Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean.

Kati ya mwaka 2011 na 2013, wakati alikua bado mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA, Chuck Blazer alikua akibebelea chombo kidogo cha kurekodi sauti ambaco alikua akikificha kwenye funguo zake gari. Chuck Blazer alirekodi mazungumzo zaidi ya mia moja, ambayo yote yaliwekwa kwenye faili iliyofunguliwa na Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki ya New York, Loretta Lynch, ambaye ni waziri wa sheria wa Marekani tangu Aprili 27.

Kwa sasa, maofisa tisa wa FIFA waliochaguliwa pamoja na wadau watano wa uongozi wa soka wameshtakiwa rasmi kwa tuhuma za kashfa ya rushwa, hasa kuhusiana na utoaji wa Kombe za Dunia, haki za masoko na televisheni. Jambo ambalo limezua hali ya sintofahamu, kwani Ijumaa wiki hii kutafanyika uchaguzi wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA. Uchaguzi utafanyika wakati ambapo rais wa sasa wa FIFA, Sepp Blatter, raia wa Uswisi anayemaliza muda wake, ambaye amekua akikosolewa mno, anatazamiwa kuwania muhula wa tano. Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limeomba uchaguzi huu uahirishwe.
Joseph Blatter
David Ginola withdrew from the FIFA presidency race two weeks after announcing he would stand
David Ginola alijiondoa kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi  FIFA wiki mbili zilizopita
Miongoni mwao 14 wako kwenye wasiwasi na sakata hilo

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Barcelona Luis Figo nae alijitoa


http://www.cokestudio.co.tz/en_TZ/season2/KUFUATIA mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Msimu wa Pili wa Coke Studio Africa, Kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya, inayo furaha kutangaza kuanza tena msimu wa tatu wa burudani ya muziki maarufu kwa jila la Coke Studio Africa. msimu huu utajumuisha wanamuziki wakali 26 barani Afrika huku nyimbo mpya 52 kutumbuizwa ikiambatana na maonyesho 9 ya wanamuziki wanaotamba hapa duniani.
Maonyesho hayo ya muziki ya Coke Studio Africa ni tofauti na mengine ya aina hiyo yanayolenga zaidi kupatikana mshindi. Badala yake, maonyesho haya yanalenga kujumuisha pamoja vipaji tofauti vya wanamuziki mbalimbali kutoka barani Afrika. Aidha, yanatoa fursa kwa wasanii wanaochipukia kufanya pamoja kazi zao na wanamuziki nguli wa ndani na wale wa ngazi za kimataifa.


Alikiba
Msimu huu unaozinduliwa utawakutanisha wanamuziki kutoka katika nchi za Tanzania, Msumbiji, Kenya, Uganda na Nigeria, na kwa mara ya kwanza wasanii hawa wataweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki kwa kushirikiana katika staili ya kipekee ijulikanayo kama mash-ups – ambayo inatawala kwa sasa katika tasnia ya muziki duniani. “Kufurahia muziki wa Kiafrika” ikiwa ndiyo kiini kikuu cha burudani hiyo, msimu huu mpya wa Coke Studio Africa utawakutanisha wasanii maarufu ambao wameonyesha mafanikio makubwa katika kazi zao, na pia maonyesho hayo yatawaleta pamoja wasanii nyota wanaochipukia katika ulimwengu wa muziki.

Chini ya ushirikiano huo mpya na Kampuni ya Coca-Cola, Shirika la Ndege la Kenya kwa upande wake litawasafirisha wasanii wote na waandaaji wa muziki wanaoshiriki katika Msimu wa Tatu wa Coke Studio Africa. Mpango huo wa ushirikiano wa makampuni haya makubwa unatokana na imani ya kwamba hatua hiyo itajenga msingi wa ubia muhimu wa kufanya kazi kwa pamoja.


Vanessa Mdee
Akizungumzia juu ya Coke Studio Africa Msimu wa Tatu, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema: “Lengo letu ni kuufanya na kuwezesha namna ambayo muziki unavyoweza kuchukua nafasi katika kukonga nyoyo za watu katika Bara letu. Coke Studio Msimu wa Tatu si kwa ajili ya kuwakutanisha tu wanamuziki wa Afrika, bali pia maonyesho haya yanatoa fursa ya pekee ya ushirikiano ambao ni imani yetu kuwa wateja wetu pamoja na umma kwa ujumla wangependa kuusikia.”


Straika wa Sevilla  Carlos Bacca akiifungia bao la Ushindi kipindi cha pili dakika ya 73

Juhudi binafsi za Bacca zilimfanya aifungie bao mbili na Kipa wa  Dnipro Denys Boyko Pamoja na kuwa kulilinda vyema lango lake hakuona ndani bao la mwisho la Bacca.

Bacca akishangilia

Carlos Bacca akiomba mara baada ya  kufunga bao mbele ya wapiga picha pembeni ya Uwanja
Mchezaji wa zamani wa  Blackburn Rovers  Kalinic alishangilia bao lake huko Warsaw, Poland

Kalinic akipongezwa na Wana Dnipro

Dnipro Mashabiki waliosafiri kwenda kuishangiliaTimu yao
Carlos Bacca  ndie aliyewafungia bao la Ushindi Sevilla na kufanya Timu hiyo kuibuka na Ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Dnopro. Ushindi huu unawafanya Sevilla kulibeba kombe hilo kwa mara ya nne.Carlos Bacca akishangilia moja ya bao lake usiku huu kwenye Fainali. Bacca kaifungia Sevilla bao 2 la pili na la tatu na kuipa Ushindi.Rotan wa Dnipro akishangilia ba la pili pamoja na Leo Matos
Bacca wa Sevilla akishangilia bao lake la pili huku Jose Antonio Reyes (kushoto) akimshangaa kwa ufundi wakeKocha wa Zamani wa Manchester United nae alikuwa moja ya watazamaji katika Fainali hii ya Europa Ligi
Balaa mpaka nyavuni!Dnipro vs. Sevilla


FIFA imesema Uchaguzi wa Rais wa Shirikisho hilo utaendelea Ijumaa licha ya Maafisa wao 7 kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya zaidi ya Dola 150 Milioni.
Ijumaa Kongresi ya FIFA inapiga Kura za Uchaguzi wa Rais ambapo Rais wa sasa, Sepp Blatter, anawania kiti hicho kwa mara ya 5 huku akikabiliwa na Mpinzani mmoja, Mwana wa Mfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Maafisa waliobambwa Leo kwa tuhuma za rushwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb, na Eduardo Li, Julio Rocha, Costas Takkas, Eugenio Figueredo, Rafael Esquivel na Jose Maria Marin.
Maafisa wa Polisi wa Uswisi waliivamia Hoteli ya Baur au Lac Mjini Zurich ambayo Wajumbe wa FIFA wamefikia kwa ajili ya Uchaguzi wa Ijumaa na kuwanasa Maafisa hao 7 kutokana na Mashitaka yaliyofunguliwa na Idara ya Sheria ya Marekani ambayo imefungua Mashitaka 47 kwa Watuhumiwa 14 wanaodaiwa kuhusika na rushwa na utakatishaji Fedha kwa kipindi cha Miaka 24.

Hata hivyo, Rais wa FIFA, Sepp Blatter, hajahusishwa na Mashitaka hayo.




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho.Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro).

YAMOTO BAND, MASHAUZI KUWASHA MOTO MANGO GARDEN 

KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden, ulioko Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kupitisha wikiendi bila burudani yoyote, leo usiku ‘utawaka moto’ wakati Yamoto Band na Mashauzi Classic zitakapotoa shoo kabambe hapo.
Wasanii wa yamoto band.

Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.

Kesho, Ijumaa,  Malaika Band ambao hupiga hapohapo Mango Garden, kila Ijumaa, watakuwa Arusha mjini wakitoa burudani.
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhani 'Isha Mashauzi'.

Vilevile,  Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, wasanii hao Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.  Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi
Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la Nyama Choma.

waliotembelea blog