Friday, March 7, 2014
4:01 AM
Unknown
Klabu
ya Arsenal imeshangazwa na kitendo cha benchi la ufundi la England
kuendelea kumchezesha Wilshere akiwa majeruhi kwenye mechi ya kirafiki
kati ya England na Denmark. Taarifa hii ya Arsenal imetolewa na
madaktari wa timu baada ya kumfanyia vipimo mchezaji huyu na kugundua
majeraha makubwa kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kuchezewa rafu
mbaya na beki wa Denmark, Daniel Agger. Wilshere alifanyiwa rafu dakika
ya 12 ya mchezo lakini alitolewa nje dakika ya 59. Madakatri wa Arsenal
wamesema benchi la ufundi la England lilitakiwa kuangalia uzito wa faulo
aliyofanyiwa Wilshere na kumfanyia uchunguzi mdogo kabla ya kuamua
kuendelea kumchezesha. Matokeo ya kuendelea kumchezesha yamesababisha
kukua kwa majeraha na mchezaji huyu anatarajiwa kukosa mechi zilizobakia
za ligi na anaweza pia kukosa kombe la dunia.
Subscribe to:
Posts (Atom)