Thursday, December 17, 2015



Jumamosi Desemba 19

18:00 Chelsea v Sunderland
18:00 Everton v Leicester
18:00 Man United v Norwich
18:00 Southampton v Tottenham
18:00 Stoke v Crystal Palace
18:00 West Brom v Bournemouth
20:30 Newcastle v Aston Villa

Jumapili Desemba 20

16:30 Watford v Liverpool
19:00 Swansea v West Ham

Jumatatu Desemba 21

 23:00 Arsenal v Man City


Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich alikutana na bodi ya klabu hiyo kujadili hatima ya meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho na sasa kuamua kumtimua.
Hii ni baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo mabaya sana msimu huu, matokeo ya karibuni zaidi yakiwa kuchapwa 2-1 na Leicester ligini Jumatatu.
Hiyo ilikuwa mara ya tisa kwa Chelsea kushinda Ligi ya Premia katika mechi 16 na sasa wamo alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.

Mechi inayofuata kwa Chelsea ni Sunderland Jumamosi uwanjani Stamford Bridge.
Abramovich alitangaza kwamba bado alikuwa akimuunga mkono Mourinho Oktoba lakini matokeo hayajaimarika.
Abramovich na wenzake uongozini Chelsea wamekuwa wakimuunga mkono meneja huyo lakini kuna kizungumkuti cha matokeo mabaya na kuendelea kufanya vibaya Kwa Klabu hiyo kuimeifanya Imtimue Meneja wake na hii ni baada ya kutoimarika kwa Klabu hiyo.


Meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola na Diego Simeone Atletico Madrid bado wana majukumu kwa sasa. Hili limepelekea uvumi kwamba sasa huenda Chelsea ikarudi tena kwa Guus Hiddink kwa mkataba wa muda.Jose Mourinho hapa alioneka akiwa na Kikosi cha  Chelsea siku ya Jumanne wakifanya mazoezi na leo hii Alhamisi Kutimliwa.

Mourinho sasa kuuangalizia Mtanange wa Chelsea dhidi ya Sunderland kwenye Tv

Mourinho amekuwa kwenye kizungumkuti baada ya Msimu huu Kikosi Chake kutofanya Vyema


Kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa  Leicester jumatatu kiliongeza Machungu kwa Mmiliki na Wapenzi wa Soka wakiwemo Mashabiki wake.

Mourinho alisukumiza sababu kwa Wachezaji wake kuwa ndio waliosababisha katika Mechi hiyo lakini Mmiliki wa Klabu hiyo Bwana Roman Abramovich aliitisha Kikao na Sasa wameamua kumtimua Kiongozi huyo mwenye Makeke mengi na Majigambo mengi kwenye Soka.


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.

TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.

Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).

Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.

Pia TFF kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inaweza kumruhusu kwa kipindi maalum mchezaji mwenye dosari acheze kwa leseni ya muda (provisional license) hadi dosari hizo kati ya klabu na klabu zitakapomalizwa. Iwapo dosari hizo hazitakuwa zimemalizwa, mchezaji anaweza kuzuiwa kucheza na klabu husika kuadhibiwa.


Timu zote za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kufuatilia TFF kujua wachezaji ambao hawana pingamizi na leseni za wachezaji waliopitishwa wanaweza kuanza kutumika kuanzia kesho tarehe 18/12/2015 na kwenye michezo ya kombe la Shirikisho (FA Cup) kama hawakuwa wamecheza raundi ya kwanza kwenye vilabu vya zamani.

waliotembelea blog