Sunday, August 3, 2014


Wanted: Javier Hernandez (left) is a target for Southampton who have £70million to spend this summer
Anawindwa: Javier Hernandez (kushoto) yupo katika rada za Southampton ambao wamepanga kutumia paundi milioni 70 majira haya ya kiangazi.

Southampton  wanapanga kutumia paundi milioni 70 siku chache zijazo ili kusajili wachezaji wataoziba nafasi za nyota wao walioondoka.
Saints wanatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji watakaoachwa na Manchester United wakati huu wanaoimarisha kikosi chao.
Klabu hiyo inamhitaji mshambuliaji wa Mexico, Javier Hernandez na Wilfried Zaha au Ashley Young kutegemeana na winga gani Louis Van Gaal atamuacha.
Bosi mpya wa Saints, Ronald Koeman pia anaziwinda saini za waholanzi wawili, Ron Vlaar wa Aston Villa na Virgil van Dijk wa Celtic, wakati huo huo kipa wa Celtic Fraser Forster naye yupo katika rada zake.
Tatizo la Southampton ni kwamba klabu nyingine zitawasumbua kwenye dau la uhamisho kwasababu zinajua timu hiyo imepata paundi milioni 100 baada ya kuuza wachezaji watano wa kikosi cha kwanza.
Target: Wilfried Zaha (right) is also attracting the attention of Southampton this pre-season
Kwenye rada: Wilfried Zaha (kulia) pia anawindwa na Southampton 


Great start: Joe Allen is congratulated by Rickie Lambert after his opener for Liverpool against AC Milan
Mwanzo mzuri: Joe Allen akipongezwa na Rickie Lambert baada ya kuifungia bao la kuongoza Liverpool dhidi ya AC Milan.

LIVERPOOL wametinga fainali ya mashindano ya kimataifa ya maandalizi ya msimu nchini Marekani na sasa watakabiliana na wapinzani wao wakubwa Manchester United siku ya jumatatu.
Hii inatokana na ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya AC Milani huko Charlotte.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Joe Allen na Suso na yaliwafanya Liverpool washinde mechi tatu kati ya tatu walizocheza kwenye mashindano hayo.
Majogoo hao wa jiji walikuwa na uhakika wa kumaliza katika nafasi ya juu ya kundi  lao kufuatia Manchester City kufungwa kwa penati 5-4 dhidi ya Olympiacos baada ya kutoka sare ya 2-2 katika dakika za kawaida.
Hata hivyo katika mchezo huo, Rickie Lambert alikosa mkwaju wa penalti.
Young star: Raheem Sterling looks to take the ball of Milan midfielder Michael Essien
Kinda nyota: Raheem Sterling akijaribu kuchukua m[ira dhidi ya kiungo wa AC Milan  Michael Essien
Spurned: Rickie Lambert missed a penalty for Liverpool, a great chance for an early goal in his Reds career

Rickie Lambert alikosa mkwaju wa penalti lciha ya Liverpool kushinda.


Kikosi cha LIVERPOOL: Mignolet, Kelly (Johnson 60), Toure (Sakho 60), Coates (Skrtel 60), Robinson Enrique 60), Lucas (Gerrard 60), Henderson (Suso 46), Allen (Can 60), Lambert (Peterson 60), Ibe (Coutinho 60), Sterling (Coady 46). 


Wafungaji wa magoli: Allen (17), Suso (89).

Kikosi cha AC MILAN: Abbiati (Gabriel 46), Abate (Zapate 80), Bonera, Rami (Mexes 66), De Sciglio, Essien (Cristante 66), Muntari (Poli 80), Saponara, Niang, Pazzini (Balotelli 46), El Shaarway (Honda 66).

Mwamuzi: David Gantar 


Miss Redd's Kagera 2014 Jackline Kimambo kwenye pozi ya picha baada ya Kutangazwa Mshindi usiku wa kuamkia leoMshindi wa Taji la Redd's Miss Kagera Jackline Kimambo(katikati) kwenye picha ya pamoja na mshindi wa  pili na watatu ambapo mshindi wa pili ni Nyangi Warioba na watatu ni Faudhia Haruna(kushoto).Babylove Kalala (kulia) akimvisha taji Miss Redd's Kagera 2014 Jacline Kimambo(katikati) shindano lililofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba Mjini.

Mshindi wa Miss Redd's mwaka 2012 Babylove Kalala ndie aliyemvalisha Taji Miss Redd's Kagera 2014
Picha za Pamoja zilipigwa za washindi

Jackline Kimambo(katikati) Mshindi wa Redd's Miss Kagera 2014, kulia ni mshindi wa pili Nyangi Warioba na (kushoto) ni Faudhia Haruna kwenye picha ya pamoja.
Warembo walipokuwa wakitoa burudani ya ufunguzi.
Jumla ya warembo nane walichuana
Warembo wakitoa Burudani yao ya Onesho la Ufunguzi Jukwaani.
 Mgeni Rasmi (kushoto) Bw. Amimu Kangezi-Mwenezi wa Chama cha mapinduzi Mkoa Kagera na (kulia) ni Kiongozi wa Utamaduni hapa Kagera
Warembo wakitoa Burudani ya Ufunguzi
Sharobaro Wakihaya kutoka kundi la Futuhi la (Star Tv) akipagawisha Wahaya wenzake katika Usiku wa Redd's Miss Kagera 2014
Ilikuwa Balaa sana!! Tajiri wa Kigoma nae alikuwepo!Kwa kuchekeshaa tuu!! Huu ndio mtambo wa kuchomoa mbavu na kuanika 32 nje!!

Vazi la Ufukweni

Mshiriki Miss Redd's Kagera 2014 Tete Augustine
Warembo wakionesha VaziUbunifu
Furaha kwa Mashabiki wao! Tabasamu
Baadhi ya Wapenzi wa Miss Redd's wakifuatilia kwa karibu Mchuano huu wa kmpata Mwakilishi wa Mkoa wa Kagera 2014
Majaji wakiumiza kichwa kutafuta tano bora, kutoka kushoto ni Jaji Abera Kamala, Mr. Jay Buberwa na kulia ni Jaji Lilian PeterWarembo wa Miss Redd's Kagera 2014 waliobahatika kuingia Tano Bora-"Top 5"
Baadhi ya Dadaz wakifuatilia nao kwa karibu wadogo zao wanavyo chuana jukwaaniWakina Dada wa Kundi la Dreams Girls kutoka Nchini Uganda walikuwepo kutoa Burudani naoKundi hili linataba sana na nyimbo mablimbali zikiwemo za Wine, Weekiend, Dance overnight, Wandekangawo na nyingine kibao.Hatari lakini salama!Kibao cha jigy jigy kikishambuliwa na wenyewe jukwaani!! Wadau wa Miss redd's wakichukua na Kumbukumbu na wengine furaha zipo 120, Vunjika mbavu!! Kutoka kwa Mwanahutuhi!Unaweza ukajizuia kuona hata kucheka!! Macho yoote ylikuwa mbele!Junior Mwemezi akichukua kumbukumbu za Video kwenye Ukumbi wa Lina's Night Club, Usiku wa Redd's Miss Kagera 2014.Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi (kushoto) Bw. Amimu Kangezi-Mwenezi wa Chama cha mapinduzi Mkoa Kagera.


Packed to the rafters: 109,00 spectators watched the match unfold at Michigan Stadium in Ann Arbor
Nyomi ya hatari: Mashabiki 109,00 waliitazama mechi kwenye uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor.

Louis van Gaal amekiri kuwa alikuwa na hofu ya ukubwa wa Manchester United baada ya kuwafunga Real Madrid mbele ya mashabiki 109,000 jana usiku nchini Marekani.
Van Gaal alisema: 'Tumecheza mbele ya mashabiki 300,00  kwenye ziara hii na watakuwa wengi zaidi katika mechi ya fainali mjini Miami (dhidi ya Liverpool jumatatu).
'Inashangaza sana na athari ya mashindano haya imekuwa kubwa mno zaidi ya nilivyowahi kuona katika maandalizi ya msimu nikiwa Ujerumani au Uholanzi.'
Full: The Michigan Stadium was jam-packed for United's exciting win against the European champions
Umefurika: Uwanja wa Michigan ulifurika mashabiki walioshuhudia United ikiwatandika mabingwa wa Ulaya.
Having a good time: Two United fans cheer on their team during the Guinness International Champions Cup
Furaha imerudi: Mashabiki wawili wa United walikishangalia kwa furaha wakati wa mechi ya kombe la kimataifa la  Guinness .

Van Gaal anaweza kushinda kombe la kwanza akiwa na United, ikiwa ni wiki tatu tu tangu aanze kazi na alisema: 'Huwezi kusema upo tayari kwa kuangalia mechi za maandalizi, lakini kiukweli ni matokeo mazuri na yanakufanya ujiamini'.
'Nilibalilisha wachezaji wengi kipindi cha pili na licha ya hivyo tulifunga tena.'
Alipoambiwa Liverpool ndio wapinzani wake wanaofuata, aliongeza: 'Nadhani ni jambo zuri kwa mpira wa Uingereza kuwa na timu mbili katika mechi ya fainali'
'Mechi hii dhidi ya Real ilikuwa kama si ya kirafiki, nilihisi Madrid hawakutaka kupoteza na ndio maana walimuingiza Ronaldo mwishoni tofauti na walivyopanga'
Louis van Gaal amejipa nafasi ya kutwaa kombe la kwanza akiwa Manchester United ikiwa ni wiki tatu tu tangu aanze kazi.
Kushindi kombe la kimataifa la maandalizi ya msimu nchini Marekani sio sababu ya kusema Man United itakuwa kali na kufuta machungu ya miezi 12 ya David Moyes, lakini utakuwa mwanzo mzuri kwa Mholanzi huyo katika dimba la Old Trafford kama timu yake itashinda fainali siku ya jumatatu mjini Miami.
Man United jana usiku imefanikiwa kuifunga Real Madrid  mabao 3-1, huku Cristiano Ronaldo akianzia benchi dhidi ya timu yake ya zamani.
Bao la kwanza la Man United lilifungwa na Ashley Young katika dakika 20. Katika dakika ya 27, Real Madrid walisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti uliotiwa kambani na Gareth Bale.
Katika dakika ya 37 kipindi hicho cha kwanza, Young aliifungia United bao la kuongoza na katika dakika ya 80, Javier Hernandez 'Chicharito' akaifungia United bao la tatu.
United's hero: Ashley Young struck twice to help his side beat the reigning European champions Real Madrid
Shujaa wa United: Ashley Young alifunga mawili katika ushindi wa 3-1
Packed to the rafters: 109,00 spectators watched the match unfold at Michigan Stadium in Ann Arbor
Watazamaji 109,00 waliitazama mechi kwenye uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor

MATCH FACTS

KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED (3-4-1-2): De Gea 7; Keane 5.5, Jones 7, Evans 6 (Blackett 45mins 6); Valencia 5.5 (Lingard 61mins 6.5), Herrera 7 (Cleverley 45mins 6), Fletcher 7.5, Young 7 (Shaw 45mins 6.5); Mata 6.5 (Kagawa 61mins 6.5); Welbeck (Zaha 41mins 5.5), Rooney 6 (Hernandez 61mins 7).

Mfungaji wa magoli: Young 20, 37, Hernandez 80.

KIKOSI CHA REAL MADRID (4-1-4-1): Casillas 6; Arbeloa 6 (Ronaldo 73mins 6), Pepe 6, Ramos 6.5, Fernandez 7; Alonso 7(De Tomas 55mins 7.5); Carvajal 6.5, Illarramend 6, Modric 6, Bale 7; Isco 6.

Mfungaji: Bale (pen) 27.

Kadi ya njano: Arbeloa, Isco.

Mwamuzi: Hilario Grajeda 7.
Breaking the deadlock: Young opened the scoring for United with a crisp finish past Casillas
Alivunja ngome: Young alimtungua kwa umakini mkubwa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas


other


MALAWI wamefuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kuifunga Benin kwa mikwaju 4-3 ya penalti.
Mechi iliyopita mjini Cotonou, Malawi walifungwa bao 1-0 na leo wakiwa nyumbani wamepata ushindi wa aina hiyo, hivyo sheria ya mikwaju ya penalti kutumika kuamua mshindi.
Bao pekee la ushindi kwa Malawi liligungwa na John Banda katika dakika ya 13.
 Malawi ambao wapo nafasi ya 16 kwa nchi za Afrika katika viwango vya FIFA walitawala mchezo kwa muda mrefu, lakini walishindwa kupata mabao mpaka penalti zikaamua.
Benin ndio walikuwa wa kwanza kulishambulia lango la Malawi, lakini nyota wake Stephane Sessegnon alikosa nafasi kadhaa na kuipa Malawi kupata faida ya ushindi kwa penalti.
Baada ya ushindi huo, Malawi watakabiliana na nchi za Mali, Ethiopia na Algeria kwenye kundi B.
Wakati huo huo, Rwanda nao wamefuzu hatua ya makundi kwa mikwaju ya penalti baada ya kufuta kipigo cha mabao 2-0 walichopata ugenini dhidi ya Congo-Brazzavile.
Mabao mawili ya Rwanda yalifungwa kipindi cha pili kupitia kwa Ndahinduka Michel katika dakika 55 na Meddy Kagere katika dakika ya 60 na kuipa nchi hiyo ushindi.

Rwanda walishinda penati 4-3 na Patrick Sibomana alifunga penati ya ushindi na sasa wanaungana na mabingwa watetezi Nigeria, Afrika kusini na Sudan katika kundi A.


In trouble: 21 West Ham and Newcastle fans were arrested for fighting in Dusseldorf (not pictured)
 Mashabiki 21 wa Westham na Newcastle wamekamatwa na polisi mjini Dusseldorf (picha ya juu haihusiani na tukio).
POLISI nchini Ujerumani wamewatia mbaroni mashabiki 21 wa klabu za Westham na Newcastle baada ya kuanzishaji fujo na kuzichapa 'kavukavu' huko Dusseldorf.
Mapigano hayo yalizuku baina ya mashabiki hao hasimu jana mchana na polisi 100 walipelekwa eneo la tukio kutuliza ghasia.
Timu hizo mbili zitachuana katika kombe la Schalke 04 mwishoni mwa wiki hii huko  Gelsenkirchen.
Msemaji wa polisi wa Polizeipräsidium Düsseldorf alisema: 
"Kulikuwa na mashabiki 300 wa Uingereza katikati ya mji".
"Mashabiki kutoka klabu zote walikutana na awali ya yote walikuwa na bia na walipokutana walianza kurushiana maneno na baadaye kuamua kupigana".
"Tulituma polisi 100 katikati ya mji ili kutuliza mambo na zoezi hilo lilifanikiwa haraka na kwa muda mfupi tuliwatia mbaroni mashabiki 21",
Abroad: Newcastle and West Ham are competing in the Schalke 04 Cup this weekend
Mwishoni mwa wiki hii klabu za Newcastle na West Ham zinachuana katika kombe la  Schalke 04 




Keita compares Garcia to Guardiola


SEYDOU Keita amemfananisha kocha wa Roma, Rudi Garcio na kocha wake wa zamani akiwa Barcelona, Pep Guardiola.

Kiungo huyo wa zamani wa Barca alijiunga na timu hiyo ya Seria A kwa mkataba wa mwaka mmoja majira haya ya kiangazi kufuatia kumalizana na Valencia.
 Nyota huyo mwenye miaka 34 anajiimarisha ili kutafuta nafasi chini ya Garcia na amezifananisha mbinu za Mfaransa huyo na Guardiola ambaye alicheza chini yake katika dimba la Camp Nou.

Keita ameliambia La Gazzetta dello Sport:  “Nimekuja katika kikosi kikubwa na kuungana na wachezaji wazuri”.
“Kucheza na wachezaji kama Francesco Totti, Daniel De Rossii, Morgan De Sanctis, Mehdi Benatia, Miralem Pjanic na nina uhakika ninawasahau wengine, tuna kila kitu na tunachosubiria ni msimu mzuri,”
“Pep alikuwa ananisema sana nikiwa Barcelona kwasababu siku zote alikuwa anatambua mchango wangu kwa klabu. Garcia ni sawa na yeye na ananikumbusha enzi za Pep, anatamani kuona timu yake inacheza mpira wa kuvutia na kumiliki”.

“Wana mbinu sawa sawa: matokeo yanapatikana kupitia mpira mzuri”.

waliotembelea blog