Nyomi ya hatari: Mashabiki 109,00 waliitazama mechi kwenye uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor.
Louis van Gaal amekiri kuwa alikuwa na
hofu ya ukubwa wa Manchester United baada ya kuwafunga Real Madrid mbele
ya mashabiki 109,000 jana usiku nchini Marekani.
Van Gaal alisema: 'Tumecheza mbele ya
mashabiki 300,00 kwenye ziara hii na watakuwa wengi zaidi katika mechi
ya fainali mjini Miami (dhidi ya Liverpool jumatatu).
'Inashangaza sana na athari ya
mashindano haya imekuwa kubwa mno zaidi ya nilivyowahi kuona katika
maandalizi ya msimu nikiwa Ujerumani au Uholanzi.'
Umefurika: Uwanja wa Michigan ulifurika mashabiki walioshuhudia United ikiwatandika mabingwa wa Ulaya.
Furaha imerudi: Mashabiki wawili wa United walikishangalia kwa furaha wakati wa mechi ya kombe la kimataifa la Guinness .
Van Gaal anaweza kushinda kombe la
kwanza akiwa na United, ikiwa ni wiki tatu tu tangu aanze kazi na
alisema: 'Huwezi kusema upo tayari kwa kuangalia mechi za maandalizi,
lakini kiukweli ni matokeo mazuri na yanakufanya ujiamini'.
'Nilibalilisha wachezaji wengi kipindi cha pili na licha ya hivyo tulifunga tena.'
Alipoambiwa Liverpool ndio wapinzani
wake wanaofuata, aliongeza: 'Nadhani ni jambo zuri kwa mpira wa
Uingereza kuwa na timu mbili katika mechi ya fainali'
'Mechi hii dhidi ya Real ilikuwa kama si
ya kirafiki, nilihisi Madrid hawakutaka kupoteza na ndio maana
walimuingiza Ronaldo mwishoni tofauti na walivyopanga'
0 maoni:
Post a Comment