Friday, July 12, 2013
















msanni Prezzo wa Kenya  atakuwa amepata sample ya majibu ya baadhi ya fans wake ambao wengi ni wakenya baada ya kumdiss Diamond Platinumz wa Tanzania kupitia akaunti yake ya twitter July 10.


Sample ya majibu hayo inaweza kuonekana kupitia comments zote za fans kwenye habari iliyowekwa na mtandao wa ghafla wa nchini Kenya, ambapo asilimia 99 wameonesha kutokubaliana na alichokifanya.



Edwin Mwashegwa  : ah, Diamond achana na huyu mbulula, wewe unda hela!, bifu za kisenge hazifai.



Top Commenter: Prezzo umepita hiyo age ya beef za kishenzi. Ingia studio utoe kitu, otherwise kwa musiki diamond ako juu. I feel you bro! anything to remain relevant and grab some headlines.



Bellah Ongachi : aaarggh Diamond is waaayy better.. n am sure by the time he hits the years prezzo has stayed in the entertainment scene he'll be miles ahead..so your thing diamond.



Caroline Karijo : Mhhhhh who even listens to to him Jaguar and Diamond r much better than him n we all knw,,,,,,, he can continue playing women who stoops low for him.



Yvonne De Cole : Prezzo ni wivu nini,,,, leave the highest paid musician in East Africa alone,,, ana mulla en he is still simple doesn floss,,,, prezzo inherits yet flosses



De Sheriff : Diamond, silence is the best weapon. let the baby throw tantrums. Prezzo, its tym to mature up.

Katika umri wa miaka 76 amekuwa jina linatamba na nyota wa kurasa za mbele za majarida.
Lakini Papa Francis kwa sasa anapambana kwa nguvu zote kuepuka kuwa mtu maarufu - ameamuru kuondolewa kwa sanamu yake  kwenye kanisa kuu la mjini Buenos Aires.
Tangu kusimikwa kwake waumini wamekuwa wakitembelea sanamu hiyo iliyoko katika bustani ya kanisa kutoa heshima kuu kwa baba mtakatifu huyo, wakati watalii wamekuwa wakipiga picha kando yake.


Lakini Papa Francis, Askofu wa zamani wa mji mkuu huo wa Argentina, aliripotiwa kutishwa na habari hizo.
Alipiga simu moja kwa moja na kutoa maneno makali kwa padri huyo aliyehusika akimweleza: "Angusha hicho kitu, haraka", gazeti la Argentina la Clarin liliripoti.
Vyanzo vya kanisa vililieleza gazeti hilo kwamba Papa Francis amedhamiria kuepuka kutengeneza 'upendo wa ubinafsi' kama ule aliofurahia Papa John Paul II.
Tangu alipochaguliwa mwezi Machi, Papa Francis amefika mbali kuonekana kama asiyetaka makuu, akionesha uvumilivu kidogo kwa ufahari na msukosuko unaokuja na nafasi yake kama kiongozi wa Wakatoliki bilioni 1.2 kote duniani.
Mara chache huvaa joho na mapambo ya kitamaduni maalumu kwa Papa huyo, na kuendelea badala yake kuvalia kanzu ya kawaida nyeupe na msalaba wa chuma.
Amegoma kuhamia kwenye makazi ya kifahari ya Papa, akisema ni makubwa mno, na kupenda kuishi badala yake katika nyumba ya kawaida ya wageni kwa ajili ya watawa wanaokuja kutembelea Vatican., ambao pamoja nao hula chakula na kuendesha misa kila siku asubuhi.
Lakini umaarufu wake mpya hauepukiki - hasa kuondoshwa kwa sanamu hiyo kugongana na kutajwa kwa Francis kama Mwanaume Bora wa Mwaka na jarida la Vanity Fair lililochapishwa Italia.
Jarida hilo lilisema:
"Siku zake 100 tayari zimemweka kwenye kundi la viongozi wa dunia walioweka historia. Lakini mapinduzi yanaendelea..."
Sanamu hiyo, iliyosimikwa siku kumi zilizopita, ilikuwa ni mtazamao wa mchongaji Fernando Pugliese, ambaye pia alitengeneza sanamu bustani ya wazo Katoliki inayoitwa Holy Land (Ardhi Takatifu) nchini Argentina. Hapo awali alishawahi kutengeneza sanamu za Papa John Paul II na Mama Teresa.
Inasubiriwa kuona kama makumbusho ya Papa Francis kwenye eneo hilo, yaliyotangazwa wiki mbili zilizopita, nayo yatapigwa marufuku na Papa huyo.


 


Mm ni kijana wa miaka 23 sasa nililelewa na wajomba mkoani Kagera, nilipokuwa na umri wa miaka 17 niliwahi kulawitiwa na mjomba angu kwa kipindi cha mwaka mzima na nikivuta kumbukumbu zangu nadhani ilifikia zaidi ya mara nane. Nilipomaliza for 4 nikaondoka huko Kagera na kuja kuishi Dar kwa dada yangu ili niweze kujiendeleza maana matokeo yangu hayakuwa mazuri.
Nilipofika Dar nimesomea course mbili ambazo ndo zimenisaidia kumudu maisha yangu mjini na kipindi nimeingia Dar tayari nilikuwa nishazoea guys sexual yani nilitamani sana maana nilikuwa namkumbuka mjomba kwa jinsi alivyokuwa akinifanya na nikatamani kupata tena hilo tendo.

mwaka baada ya kumaliza course yangu nilipata kazi sehemu na nikawa nafanya hiyo kazi nilipofikisha umri wa miaka 20 nikapata tena mtu mwingine wa kufanya nae, ki ukweli nilikuwa nafurahia ilo jambo kwa sana na nikaona ni zuri kwangu.

sasa toka kufanya na mjomba nimeshafanya na watu zaidi ya wanne.

Sasa nataka kwenda nyumbani kusalimia maana nina muda sijaenda kuwasalimia kitu kinachoniumiza kichwa ni mjomba na yeye ameshaowa na naogopa anaweza akataka tena.

Je mnanishaurije wana jamii wenzangu?





 



MAAJABU YA MBEYA HEBU SOMA HII KWA MAKINI KABISA.
  Huyu mzee alifika katika studio za Kyela FM, anasema yeye anahitaji Msaada anataka kwenda kumfufua Mwl. Julius
Kambarage Nyerere baba wa Taifa aliyefariki Miaka 15 iliyopita,Na huo ufunguo ameushika mkononi ndiyo wa kumfufulia! Madai yake mzee huyu
anasema anaenda kumfufuana Mwalim ndiye atakuja kusimamia uchaguzi wa mwaka 2015.Na pia anaibashiria CCM kuwa mshindi atatoka katika chama cha CCM.
STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel juzikati alifunguka na kuweka wazi juu ya mipangilio yake ya ndoa kuwa anatarajia kubeba ujauzito siku chache zijazo kwani ana kiu kubwa ya kuitwa mama. 

Akichonga na paparazi wetu Julai 9, mwaka huu nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kuwa anajutia sana kukaa kwa muda wote bila kuiruhusu mimba iingie ila siku si nyingi mambo yatakuwa yametiki.
Nina mpango wa kubeba mimba na nizae siku chache zijazo kwani sina sababu tena ya kunifanya nisipate mtoto kwa wakati huu ambao niko ndani ya ndoa na naamini itaimarika zaidi nikiitwa mama huku pembeni akiwepo baba wa mtoto wangu,” alisema Aunt Ezekiel.




















Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, jana, kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya Shingo

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na matatizo ya shingo.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye wodi ya uchunguzi ya Sewahaji, Lwakatare alisema kuwa anakabiliwa na matatizo ya pingili za shingo na jopo la madaktari linakutana leo kuamua kama afanyiwe upasuaji ama la.

“Nilifanyiwa uchunguzi kwa x-ray na madaktari walisema hakuna jinsi zaidi ya upasuaji na kesho (leo) jopo la madaktari linasoma picha za x-ray kuamua aina ya upasuaji...nimegundulika kuharibika pingili ya sita na saba
















Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi Wanafanya maandamano makubwa mjini Cairo mchana huu, huku waumini wa dini ya Kiislamu wakiadhimisha Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadan.
Wafuasi wa Bwana Morsi wanatarajia kuwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo, wataendelea kuunga mkono wito wao wa kutaka Bwana Morsi kurejeshwa madarakani.
Wapinzani wa rais huyo wa zamani ambao waliandamana hadi rais huyo akaondolewa madarakani na jeshi watakusanyika katika medani ya Tahrir.
Watu kadhaa wameuawa kwenye ghasia zilizotokea tangu Morsi alipoondolewa.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo, Jim Muir anasema vuguvugu la Muslim Brotherhood huenda liliwatenga raia wengi wakati wa utawala wa Morsi, lakini bado raia wengi wa nchi hiyo hawataki jeshi kuingilia masuala ya siasa.

Marekani kutuma ndege za kivita Misri

Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani, ilitoa wito kwa utawala mpya wa Misri, kusitisha harakati zake za kuwakamata wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood na kuonya dhidi ya kulenga kundi lolote.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon vile vile ameonya utawala huo wa Misri kutotenga chama chochote cha kisiasa katika harakati za kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo.

Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney amesema, utawala wa Washington hauamini kuwa ni lazima isitishe misaada yake ya Misri.

Marekani inatarajiwa kupeleka ndege nne za kivita aina ya F-16 nchini Misri, lakini haijathibitisha kuwa msaada huo utatolewa lini.

Serikali ya Marekani imesema, inachunguza ikiwa aumuzi huo wa jeshi la Misri kumuondoa madarakani rais Morsi ni mapinduzi ya Kijeshi kwa kuwa sheria za Marekani inazuia serikali kutoa misaada kwa nchi yoyote ambayo kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia ataondolewa kupitia mapinduzi.

Wafuasi wa rais Morsi wamekuwa wakiandamana wiki nzima karibu na kambi ya kijeshi iliyoko Mashariki mwa mji mkuu wa Cairo, ambako wanaamini kuwa kiongozi wao anazuiliwa na maafisa wa kijeshi tangu alipoondolewa madarakani







 


SERIKALI ya Tanzania imeipa onyo kali nchi ya Rwanda ikiitaka isijaribu kuota ndoto za kuishambulia kijeshi, vinginevyo itajibu mapigo kwa nguvu zote na kuhakikisha kuwa imeichakaza.


Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.


Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.


Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.


Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao na kumchapa.


Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri majadiliano….majadiliano?”


Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’.

“Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga kumtisha Rais Kikwete.


Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya; “Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.”


Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi za Maziwa Makuu.


Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na SADC.

“Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema Mkumbwa.


Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake.

Chanzo cha mzozo
Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC.

Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”.  


Hata hivyo, matamshi hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa tamko bungeni.


Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi. 

Akaongeza kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho.

Kauli ya Zitto
Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli, dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete.
 
Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa Rwanda pia kufanya hivyo.

“Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno ya nini tena? Hutaki ushauri basi. 

Maneno ya kila siku ya nini? Tangu Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili ya nini?


Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994 na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,” alisema Zitto.

Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu wake na si vita ya mtutu wa bunduki.

Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana yoyote,” alisema.

Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na mikoa ya mpakani ya Rwanda.


Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima harakati za kujenga demokrasia nchini.  Busara itumike tu,” alisema Zitto.


.

Jay Msangi ambae anaonekana katikati ameshawahi kucheza ngumi akiwa anaishi Marekani.
Taarifa ikufikie kwamba yule bondia mkongwe ambae ni mmoja kati ya waliowahi kumiliki headlines za dunia sana Evander Holyfield anatarajiwa kuja Tanzania. PromotaMtanzania Jay Msangi kutoka Hall of Fame Boxing and Promotions Company  ameongea na jovinbachwa na kumwambia hiyo game imepangwa kuchezwa Uwanja wa Taifa April 27 2014 Uwanja wa Taifa ambapo Evander atapigana na Francois Botha wa South Africa aliewahi kuwa bingwa mara mbili.





.
Evander na Francois
Jay amesema haijawa ngumu kumpata Evander kwa ajili ya pambano kwa sababu kampuni yake ina uzoefu wa miaka mingi na imeshaandaa mapambano zaidi 30 kwenye jimbo la Ohio Marekani, ni kampuni ambayo iko Marekani na hapa Tanzania. Hata hivyo kwa mara ya kwanza hii kampuni August 30 2013 itamkutanisha bondia Francis Cheka na Mmarekani Derrick atakaekua bondia wa kwanza Mmarekani kuja kupigana Tanzania. Siku hiyohiyo ya August 30 pia mabondia Mada Maugo na Thomas Mashari watashuhudiwa wakizichapa live.
 .


Maskini Irene Uwoya wetu...!!!! Inatia huzuni sana, soma hapa alichokiandika, daaah!


Kufuatia kuripotiwa kwa habari "kali" sana iliyopewa kichwa "DIAMOND AFICHUA KISA CHA KULALA NA UWOYA!" leo kuhusu mwanadada Irene uwoya na Msanii wa kizazi kipya Diamond platnumz leo na mtandao wa Global publishers, hatimaye Irene Uwoya alichukua dakika kadhaa kuandika hichi alichokiandika hapa chini....
“Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better”
MCHUNGUZI wa mambo anasema maneno hayo ni kutokana na kile alichokiona kama ni usaliti wa namna fulani toka kwa rafiki yake wa karibu (Jina kapuni) kuamua kumuanika hadharani mdada huyo wa bongo movies
Kama hukupata nafasi ya kuisona habari hiyo toka kwenye mtandao wa global publishers basi isome hapa kama tulivyoinukuu toka mtandao huo....

""SIRI nje! Lile skendo la Rais wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kudaiwa kulala na mwigizaji Irene Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ limevuja.
KISA KAMILI
Huku akijua kabisa kuwa ataibua zogo kwa kuwa Uwoya ni mke wa ndoa wa mtu, kwa mara ya kwanza, Diamond ameamua kuanika kisa kilichomfanya kujiweka kwa muda kwa Uwoya.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha gazeti hili, kilichomfanya Diamond kufikia hatua ya kumtongoza na kutoka naye kimapenzi, ni kitendo cha Uwoya kutoa  maneno ya kumponda huku akionesha waziwazi hali ya kumchukia kila walipokutana.

UWOYA ALIKUWA HAMPENDI DIAMOND
“Unajua Irene (Uwoya) alikuwa hampendi Diamond hata siku moja na mara nyingi alikuwa kila akimuona lazima amponde. Habari hizo zilikuwa zikimfikia mwanamuziki huyo kupitia mashoga wa mwigizaji huyo ambazo ndiyo zilichochea.
“Kufuatia hali hiyo, Diamond naye kila alipofikishiwa taarifa na mashosti wa Uwoya, alikuwa akijisikia vibaya mno ndiyo maana ‘Sukari ya Warembo’ alilazimika kumvizia Uwoya kwa hali na mali ili kumfanya ampende.

CHIKOKA ATAJWA
“Nakumbuka kwa mara ya kwanza Diamond alimtuma (Juma) Chikoka ‘Chopa’ kwa Uwoya ili amfikishie ujumbe wa yeye kumtaka.
“Chikoka hakufikisha taarifa hizo, kitendo ambacho kilimuuma sana lakini siku moja Diamond alikutana na Uwoya akiwa na Chikoka, maeneo ya Sinza-Mori (Dar), akamuomba tena Chikoka namba, akampa, hapo ndipo uhusiano ulipoanzia.
 “Siku mbili baadaye Diamond alizungumza vizuri na Uwoya.

GLOBAL NOMA
“Diamond aliomba ahadi ya kukutana na mwigizaji huyo, bila kuchelewa, Uwoya aliiva na kukubali ambapo walikutana kwenye ile hoteli mliyoandika (Global) kule Mbezi Beach (Dar) wakamalizana.
“Unajua Diamond alifanya hivyo kwa sababu ya kupondwa na washikaji zake kuwa anatamba kutembea na mastaa lakini hamuwezi Uwoya.
“Kwa hiyo utagundua chanzo cha yote ni mdomo wa Uwoya kutangaza kutompenda Diamond kwani alikuwa akimsema vibaya sana kwa watu wake wa karibu,” kilidai chanzo chetu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
Baada ya kujazwa habari hizo, mwanahabari wetu alilazimika kumtafuta Diamond ili kuhakikisha kama alichoelezwa kina ukweli ndani yake ambapo bila kinyongo, mkali huyo wa wimbo wa Kesho alifunguka:
“Dah! Japo yalishapita ila ni kweli Uwoya nilikuwaga nikipata taarifa kutoka kwa marafiki zangu kuwa alikuwa ananichukia sana.
“Nilikuwa nikijiuliza sababu za yeye kunichukia lakini nikawa sizipati hata kidogo na hata nilipochunguza niligundua kweli alikuwa hanipendi kabisa.
“Sipendi sana kuzungumzia ishu hiyo ila naweza kukubali kweli kuwa marafiki zake na wangu ndiyo walionichochea sana kukutana na Uwoya na sasa hatuna tatizo na tunaishi kwa amani na upendo ingawa mengi yamepita na yaliyosemwa sina sababu ya kuyashikilia, kikubwa tumuombe Mungu.”

KAMA KAWA UWOYA HAPOKEI SIMU
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimwendea hewani Uwoya lakini kama kawaida, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

TUJIKUMBUSHE
Miezi kadhaa iliyopita, gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda liliripoti habari ya Uwoya na Diamond kunaswa usiku katika moja ya vyumba vya hoteli maarufu kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi huko Mbezi Beach, Dar ambapo habari hiyo iliibua maneno lakini sasa mwanamuziki huyo amemaliza utata kwani nguzo na sifa kuu ya Global Publishers ni kuandika ukweli siku zote....""

http://4.bp.blogspot.com/-uWuH_yP6DAA/Ud-rDUX3WOI/AAAAAAAAi7o/JnALffiLZB4/s1600/1.png


 SERIKALI imesisitiza kuwa itatoza Sh 1,000 kwa kila kadi ya simu inayotumika lakini pia inaangalia utaratibu wa kufanya makato hayo kwa njia ambayo haitamuumiza mtumiaji wa simu.


Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa alisema kuwa kupitia tozo hizo wanatarajia kukusanya Sh bilioni 160 kwa mwaka.

“Kupitia wawakilishi wenu na sisi serikali kuwa sikivu, tulishauriwa na ikaonekana kwamba kuna uwezekano wa kupata chanzo kingine cha mapato kupitia kadi za simu”alisema.



Alisema katika mapendekezo yaliyokuwa yametolewa serikali ilishauriwa kutoza Sh 1,450 katika kila kadi ya simu lakini baada ya kukaa na kushauriana serikali iliona ni vyema ikatoza Sh 1,000 ili kila mwananchi aweze kumudu gharama ambapo kwa mwaka kila mmiliki wa kadi ya simu atatozwa sh 12,000.


Alisema baadae serikali ilipokea mapendekezo mbalimbali ili kuangalia kama hilo linaweza kutekelezeka na walipita ngazi zote kabla halijapelekwa katika kamati za Bunge na kushauriwa kwamba tozo hilo linaweza kufanyika kwa lengo la kukuza uchumi hasa maeneo ya vijijini.

 
“Tathmini zote zimefanyika kikamilifu na baadae suala hilo likafikishwa Bungeni ambapo pia napo lilikubalika... inawezekana watu wanalalamika lakini ngazi zote suala hilo lilipopita lilikubalika na ikaonekana ni sawa kutozwa sh 1,000 kwa kila kadi ya simu” alisema.



Alisema kutokana na hilo kwa kutwa nzima kadi ya simu itatozwa Sh 33.35 au Sh 100 kwa siku tatu ambapo serikali inaangalia utaratibu mzuri ambao hautamuumiza mtumiaji wa simu.


Dk Mgimwa alisema fedha hizo zitakazokusanywa zitaongeza upatikanaji wa maji vijijini, umeme pamoja na kuboresha miundombinu katika maeneo ya vijijini.

 
HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi.
Kwa mujibu wa habari ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:
Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”
 

KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea. 

 
 Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.
Sauti: Haloo, mimi Masogange.     
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.
“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”

Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?
Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
Habari hii imeandikwa na Imelda Mtema, Haruni Sanchawa na Musa Mateja.

 
 






 
 
Kuna saa najiuliza kwanin ukimwamin mtu ndio anageuka...kwanin ukiwa muwaz watu wanakuchukulia vbaya? Leo nimeumia sanaaa kuliko skuzote...sijaamini mtu niliye mwamini kumuona kama rafiki yangu anaweza kuongea shit kuhusu mim...au najiuliza siruhusiwi kuwa na rafik wa kiume? Lakin sa nyingine nakaa chin nasema God ...u know me better” alifunguka Uwoya. Sababu kubwa iliyodaiwa kumfanya Diamond atembee na Uwoya ni kitendo cha muigizaji huyo kudaiwa kumponda mara kwa mara na alikuwa hampendi Diamond ambaye alikuwa anafikishiwa habari hizo na marafiki zake Irine.

  
Emmily Omari akiwa selo.


 MREMBO mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo.

Emmily ambaye amekuwa akiwatesa askari polisi ambao wamekuwa wakimkamata mara kwa mara na kumfikisha mahakamani lakini haachi tabia hiyo, alipandishwa katika Mahakama ya Jiji na kusomewa mashtaka yake.
Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.
Pilato huyo baada ya kumuona tena Emmily mbele yake akikabiliwa na shitaka lilelile, alimuuliza alikuwa na tatizo gani lililosababisha mara kwa mara afikishwe mahakamani hapo, mrembo huyo hakujibu chochote.
“We Emmily sasa unatuletea utani, kila siku unaletwa hapa tunakupiga faini unalipa unatoka na kwenda kurudia hiyo biashara yako… sasa tunaona kama unatufanyia masihara  sasa leo hakuna cha faini wala dhamana uende Segerea ukale dona la bure labda utajifunza,” alisema Hakimu Lyon na kuwaamuru askari wampandishe kwenye Karandinga kwa ajili ya safari ya gerezani.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.






























Dar es Salaam. Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.
Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.
Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.
“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.
Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.
Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.
Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati.  Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.
Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.

waliotembelea blog