Tuesday, July 7, 2015


Raia huyo wa Uingereza ambaye harakati za kuhamia Manchester City, zilitumbukia nyong'o amekadiriwa kuwa mwenye thamani ya pauni milioni 35 na kampuni ya utafiti ya Soccerex inayochapisha Orodha ya wachezaji wenye thamani ya juu ama 20 Football Value Index.
Manchester City ilikuwa imeweka dau la pauni milioni £40 lakini ombi lao likakataliwa na Liverpool.
Mlinzi wa Manchester United, Luke Shaw ameorodheshwa katika nafasi ya 9, John Stones wa Everton ameorodheshwa wa 16 huku kiungo wa Arsenal Calum Chambers akiorodheshwa katika nafasi ya 19.

Kampuni hiyo ya Soccerex imefanya utafiti huo miongoni mwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 wanaocheza katika ligi za bara ulaya.
Inatumia vipengee kama umri,nafasi wanayocheza uwanjani,Klabu,urefu wa Kandarasi,mechi walizochezea timu zao za taifa,mechi walizocheza,mabao waliofunga,majeraha na ubora wao kitalanta.

''tukiangalia kwa kina vipengee hivi vyote tunaweza kutathmini uwezo na thamani ya mchezaji.''
''Hivyo vyote ndivyo vilitusaidia kubaini kuwa Sterling ndiye mchezaji bora na mwenye thamani ya juu zaidi barani ulaya kwa sasa.'' alisema bwana Esteve Calzada
Mlinzi wa Paris St-Germain ya Ufaransa ambaye ni raia wa Brazil Marquinhos ameorodheshwa katika nafasi ya pili na thamani ya pauni milioni £27.8.
Mchezaji mpya wa Manchester United vilevile ye Uingereza Memphis Depay aliyegharimu kitita cha pauni milioni £31 ameorodheshwa katika nafasi ya tatu akiwa na thamani ya pauni milioni £23.8.

Calzada anasema kuwa sheria iliyowekwa na shirikisho la soka la Uingereza ambayo inazilazimisha vilabu vya Uingereza kuwa na takriban wachezaji 8 raia wa Uingereza imeongeza maradufu thamani ya wachezaji waingereza.
Wachezaji 4 katika orodha hiyo ni raia wa Uingereza huku 9 kati ya 20 bora wakitarajiwa kucheza katika ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.


RAHEEM STERLING AKILINGANISHWA NA WENGINE HAPA!

1. Raheem Sterling (Liverpool) £35m 7. Mateo Kovacic (Inter Milan) £18.5m
2. Marquinhos (Paris St-Germain) £27.8m 8. Jose Gaya (Valencia) £18.3m
3. Memphis Depay (Manchester United) £23.8m 9. Luke Shaw (Manchester United) £18m
4. Domenico Berardi (Sassuolo) £21.6m 10. Aymeric Laporte (Athletic Bilbao) £17m
5. Jose Gimenez (Atletico Madrid) £21.4m 16. John Stones (Everton) £12m
6. Hakan Calhanoglu (Bayer Leverkusen) £19.4m 19. Calum Chambers (Arsenal) £10.6m

Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei.
Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya dola lakimi mbili $200,000 kabla ya makataa aliyopewa ya tarehe 3 Julai. Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.

Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama mshikilizi wa taji hilo. Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei
Taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.
Yamkini Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao,angevua mataji yote ya vijana ilikuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.
Taarifa yao iliyochapishwa katika mtandao wa www.boxing.com umesema kuwa ''hatukukuwa na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu.kwa hivyo hatutamtambua mayweather kama mshikilizi wa ukanda huo wa Welter''
Hata hivyo Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20 kukata rufaa ya kauli hiyo.
Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba, japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.
Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la welter linalopangwa kufanyika tarehe 27 kati ya Bradley na Jessie Vargas.


Harold Mayne-Nicholls
Afisa wa shirikisho la soka duniani ,FIFA aliyesimamia jopo la kutathmini uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022 amepigwa marufuku ya miaka 7
FIFA imetangaza kuwa bwana Harold Mayne-Nicholls, 54 hataruhusiwa kushiriki maswala yeyote yanayohusiana na kandanda kwa kipindi cha miaka 7 ijayo.
Kamati ya maadili ya FIFA imesema kuwa itatangaza wazi madai dhidi yake pindi marufuku hiyo itakapoaanza kutekelezwa.
Bwana Mayne-Nicholls anapanga kukata rufaa ya madai dhidi yake.
Aidha bwana Mayne-Nicholls anahoji kwanini kauli hiyo imechukuliwa na kutangazwa wakati ambao FIFA inafahamu fika kuwa anaendelea kukata rufaa.

Mayne-Nicholls aliyekuwa wakati mmoja mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chile alitajwa miongoni mwa watu 5 ambao kamati ya maadili ya FIFA ilkuwa imeanzisha uchunguzi.Alikiri wakati wa uchunguzi kufanya mazungumzo ya kibinafsi na wakuu wa shirikisho la soka la Qatar akitaka jamaa wake waajiriwe katika chuo cha mafunzo ya kisoka ya Aspire .
Kulingana na barua pepe zilizodukuliwa huo ulikuwa ni ushahidi tosha wa kumchukulia hatua bwana Mayne-Nicholls. Harold Mayne-Nicholls, 54 hataruhusiwa kushiriki maswala yeyote yanayohusiana na kandanda kwa kipindi cha miaka 7 ijayo.
Mayne-Nicholls aliongoza kamati ya FIFA iliyokuwa na jukumu la kupiga msasa maombi ya uwenyeji wa fainali ya kombe la dunia mwaka wa 2018 na 2022.
Uwenyeji wa mashindano hayo ulipewa Urusi na Qatar mtawalia.
Katika ripoti yake aliyoichapisha mwaka wa 2010, bwana Mayne-Nicholls alielezea hofu kuwa haitawezekana Qatar, kuandaa kombe la dunia kwani viwango vya joto nchini humo hutimia hata nyuzi joto 50'C.

Maafisa 9 wa FIFA wanaendelea kuchunguzwa kufuatia madai ya utoaji hongo,ama utumiaji wa mamlaka yao vibaya.
Mayne-Nicholls ni miongoni mwa maafisa waliotaka ripoti kamili ya FIFA kuhusiana na uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022 kuchapishwa kikamilifu na wazi.
Mwezi desemba FIFA iliamua kuchapisha ''nakala halali kisheria'' iliyoandikwa na Mwanasheria kutoka Marekani Michael Garcia.
Bwana Garcia baadaye alijiuzulu akidai kuwa shirikisho hilo halikuwa tayari kuwa wazi kuhusiana na yaliyojiri katika utoaji zabuni wa mashindano hayo mawili ya kombe la dunia.
Wakati hayo yakijiri Maafisa 9 wa FIFA wanaendelea kuchunguzwa kufuatia madai ya utoaji hongo,ama utumiaji wa mamlaka yao vibaya.


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa amewashukuru watanzania wote waliowapa sapoti katika mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki jijini Kampala.
Mkwasa amesema kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo.
“Kiukweli japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa.
Aidha Mkwasa amesema kwa sasa wataomba kupata nafasi ya japo siku 10 kufanya mazoezi kwa pamoja kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu, na kuwaomba watanzania wote kuwaunga mkono katika maandilizi hayo.

.
.
Good news ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa msanii wa Bongo Fleva, H Baba ambaye ametangaza rasmi sasa hivi kurudi kwenye soka na kujiunga na timu ya Toto African.
‘Kupitia kwenye kipindi cha AMPLIFAYA cha Clouds FM july 7, 2015 alifunguka na kusema’Ni kweli kwamba mimi nina vipaji vingi sasa ubora wa vipaji ni kuvionesha kwasababu nilishawahi kucheza soka na hii ni timu ya nyumbani timu nyingi zilishawahi kunihitaji sema muda mwingi sana nilikua kwenye kazi zangu za muziki kwa hiyo kwasasa hivi najipanga kwa mambo mengi wasishangae nikafanya vitu tofauti’ H Baba
.
.
‘Hapana siwezi kuacha muziki siwezi kuacha mpira siwezi kuacha filamu ni vitu vyote ambayo ninavyovipenda na siwezi kuja kuviacha mimi umri wangu bado mdogo unaniruhusu kuingia kwenye soka kwasasa hivi mimi niko Toto African watu wajiandae tu wafahamu kuwa niko Toto ila bado tupo katika harakati kwamba tutakapokaa sawa kuzungumza yakifikia sasa maafikiano ila Yanga na Sima wajiandae’ H baba

CHADEMAAR 
Taarifa ilianza kuenea jioni ya July 07 2015 kwenye kuhusu ajali ya Helicopter iliyokua imebeba Wanachadema mbalimbali akiwemo mbunge Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
Kwenye ukurasa wa Twitter wa CHADEMA zimewekwa post kwamba Mbunge Joshua Nassari ndiye aliyepata ajali hiyo ya Helicopter, amepelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu pamoja na rubani na watu wengine ambao hawajatajwa, ni baada ya kunusurika.

waliotembelea blog