Sunday, June 8, 2014





Share on facebookShare on twitterShare on linkedinShare on pinterest_shareShare on google_plusone_share
2014 FIFA World Cup Brazil. 
Group A Brazil Croatia Cameroon Mexico
Group A: Brazil, Croatia, Cameroon, Mexico
Group B Australia Chile Netherlands Spain
Group B: Australia, Chile, Netherlands, Spain
Group C Colombia Côte d’Ivoire Greece Japan
Group C: Colombia, Côte d’Ivoire, Greece, Japan
Group D Costa-Rica England Italy Uruguay
Group D: Costa-Rica, England, Italy, Uruguay
 Group E Ecuador France Honduras Switzerland
Group E: Ecuador, France, Honduras, Switzerland
Group F Argentina Iran Bosnia and Herzegovina Nigeria
Group F: Argentina, Iran, Bosnia and Herzegovina, Nigeria
Group G Germany Ghana Portugal USA
Group G: Germany, Ghana, Portugal, USA
Group H Algeria Belgium Russia South Korea
Group H: Algeria, Belgium, Russia, South Korea

 MWONEKANO WA STAGE NA JINSI  KAHAMA WALIVYOKUWA WANASHANGWESHEKA.
 HAPO SASA NDIPO SHOKA ILIPOUNGUA MPINI UKABAKI.


Bia ya bure mlangoni baada ya kuingia ndani BIA BUREEEEEEEE KWA GETI UKIINGIA TU.
KAZI NA DAWA
Mashabiki wakifurahia Kili baada ya kuingia ndani JAMAA WASHADAKA ZAO MAPEMAAA

Kama ilivyo kwa tuzo zozote maarufu duniani, mara nyingi ma’MC wa show hizo huwa wanapenda kumwaga maneno mengi sana ya utani, ila hii ni kali zaidi, bila kujijua mwenyewe wakati akiwa anaendelea kutangaza, alitokea kuwaponda watu maarufu duniani, akiwemo Kim Kardashian ambaye anajulikana kama ni mwanamke mwenye umbo zuri zaidi, “I’ve seen beautiful women here with butts that make kimkardashian‘s look like Miley Cyrus.(“nimekuja hapa nimeona wanawake wenye maumbo mazuri, yanavyomfanya Kim Kardashian aonekane kama Myle Cyrus”) – alitamka wazi wazi MC wa tuzo hizo za MTV MAMA.

Watu wenye maumbo kama Wema Sepetu na wanawake wengi wa huko nchini South Africa achilia mbali wageni waaalikwa kutoka nchi mbali mbali za africa, kwa jinsi walivyo umbika kwa asili ya maumbo yao ya ki-africa, yalimfanya hadi MC ambaye ndiye mchekeshaji muigizaji maarufu huko hollywood maarufu kama Marlon Wayans, ashundwe kujizuia na kutamka maneno kama hayo hadharani.

MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI,SAID NGAMBA MAARUFU KWA JILA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU.

AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL,MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.

MIPANGO INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA NA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA TUTAENDELEA KUJULISHANA.

NI PIGO LINGINE TENA KWENYE TASNIA YA SANAA BAADA YA KUONDOKEWA NA WASANII KADHAA MAJUMA YALIYOPITA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA,NA INAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.

-AMIN.



Msafara wa gari chache majira ya saa 2:30 ulianza safari katika viwanja vya Usa-River ambako gari za maharusi zilikuwa zikipambwa mdogo mdogo zikapanda Kilima zikiwa na maharusi Joshua Nassari na Anande Nnko safari ilikuwa ni kanisa la Kipentekoste la Kilinga,Meru tayari kwa ajili ya Ndoa.


Hatimaye Bw Harusi Joshua Nassari anateremka katika usafiri wake aina ya Range Rover muda mfupi baada ya kufika katika viwanja vya kanisala la Kilinga maarufu kama kwa Mchungaji Babu.


Wageni mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ya ndoa mmoja wapo ni huyu ,Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai(katikati)

Bibi Harusi Anande Nnko alikuwa ni mwenye furaha kila wakati ,"Full Tabasamu."

Wenyeji katika shughuli hiyo akiwemo mzee Samweli Nassari ,baba mzazi wa Jishu walikuwa wamevalia mavazi nadhifu aina ya suti wakingojea ugeni uliokuwa ukiwasili katika kanisa la Kilinga.

Hataimaye Bw Harusi Joshua Nassari akaingia kanisani yeye na wapambe wake na hapa anaye ngojewa ni Bibi Harusi Anande Nko.


Bi Harusi Anande Nko akashuka katika gari alilokuja nalo aina ya Land Cruser VX.

Bwaa Harusi Joshua Nassari akamvisha pete mkewe Anande Nnko.

Bibi Harusi Anande Nnko akamvisha pete mumewe Joshua Nassari

Kisha Maharusi wakapongezana.

Maharusi wa wakawekewa mikono na Maskofu wakiongozwa na Askofu mkuu wa kanisa la Pentekoste Tanzania (PCT) David Batenzi.

Maharusi wakiwasalimia waumini waliohudhuria ibada hiyo (hawapo pichani)

Maharusi wakionesha pete zao za ndoa muda mfupi baada ya kuvishana.


Uthibitsho wa ndoa ni vyeti vya ndoa ,na hapa maharusi wakitia saini katika vyeti vyao.

Wagebi mbalimbali walihudhuria ibada hiyo ,na hapa ni mbunge wa Viti maalum Lucy Owenya (wa kwanza)

"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.

Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.

Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.

Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka.

Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.


Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia kuwa wasomi wa vyuo wanatakiwa kuchangia mawazo yao kwenye chama ambayo yatasaidia kuleta mabadiliko hasa ya kiuchumi ,alisema ni vyema kuja na mikakati ya kuonyesha uchumi umepanda kwa mwananchi kuliko huu wa sasa ambao unaonyesha uchumi umepanda lakini ni uchumi wa kwenye makaratasi.Uongozi Tawi la SAUT Kambarage ulimualika Katibu wa Itikadi na Uenezi kuja kushuhudia makabidhiano ya Uongozi na tathmini ya Tawi kwa miaka minane sasa.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi katika Chuo cha SAUT Mwanza Ndugu Dova Mcheshi akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhiana Uongozi wa Tawi la SAUT Kambarage ambapo aliwaambia wanachama wa CCM katika Chuo cha SAUT kuwa kuanzia sasa chama kinajiimarisha zaidi kwenye Chuo cha SAUT.Dova laiyekuwa CHADEMA lakini sasa amejiunga na CCM .
Wadada wakiwa wamependeza na Sare yao ya Chama.Viongozi wa CCM mkoani Mwanza na Viongozi wa Serikali ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.
Wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage,Mwanza.


Diamond na Wema wakipiga picha za Red Carpet katika tuzo za MTV zinazoendelea usiku huu mjini Durban South Afrika, wadau wamempongeza designer wao kwa mavazi mazuri yaliyo match vizuri, kuanzia nguo hadi saa na bangili za mkono.
NI SUPERB!…

Diamond na Wema wakipiga picha za Red Carpet katika tuzo za MTV zinazoendelea usiku huu mjini Durban South Afrika, wadau wamempongeza designer wao kwa mavazi mazuri yaliyo match vizuri, kuanzia nguo hadi saa na bangili za mkono. NI SUPERB!

Diamond na Wema wakipiga picha za Red Carpet katika tuzo za MTV zinazoendelea usiku huu mjini Durban South Afrika, wadau wamempongeza designer wao kwa mavazi mazuri yaliyo match vizuri, kuanzia nguo hadi saa na bangili za mkono. NI SUPERB!

waliotembelea blog