FC Barcelona walisafiri kuelekea Madrid tayari wakiwa wanamkosa mchezaji wao wa kimataifa wa Brazil Neymar kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, licha ya kumkosa Neymar safu ya ushambuliaji ya Barcelona bado ilikuwa imara na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-2.
Lionel Messi ndio ameonekana kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22 katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea Lionel Messi faulo dakika ya 77, Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 33 na 90 baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.
Wakati magoli ya Real Madrid yalifungwa na Casemiro dakika ya 28 na James Rodriguez dakika ya 85 akitokea benchi, ushindi huo wa FC Barcelona unavunja rekodi yaa Real Madrid ambao walikuwa wamecheza mechi 22 bila kufungwa katika uwanja Santiago Bernabeu toka February 27 2016.