Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini (NEC) imewataka wananchi kutosimama katika vituo vya kupigia kura mara baada ya kupiga kura oktoba 25 kufuatia viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuwataka Wananchi kukaa umbali wa mita 100 umbali unaokubalika kisheria baada ya kupiga kura ili wazilinde kura zao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alipokuwa akifungua mkutano wa tume na waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi nchini amesema kwamba haina haja ya wanachama kulinda kura kwa kuwa mawakala wa vyama vya siasa watakuwepo katika vituo vya kupigia kura ili kulinda maslahi ya chama pamoja na wagombea wao.
Jaji Lubuva amesema kuwa wajibu wa mawakala ni kuangalia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume zinazingatiwa katika mchakato mzima wa kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi ya chama au wagombea wao.
“Changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni pamoja na kuwapo na makundi ya vijana wanaohisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kuwatisha wapiga kura hasa wakinamama ili wasiende kupiga kura”
<a
href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&amp;cb=Math.random()'
target='_blank'><img
src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&amp;source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&amp;cb=Math.random()&amp;n=a08724c9'
border='0' alt='' /></a>
Mbali na hayo Jaji Lubuva amesema lengo la kushirikisha Jeshi la
polisi kwenye uchaguzi mkuu ni kutambua na kuhakikisha kuwepo kwa hali
ya usalama na amani wakati wa uchaguzi kwani uchaguzi huru na wa haki ni
lazima uendeshwe katika hali ya utulivu na amani.Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu amesema kuwa jukumu la jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, kuimarisha ulinzi katika vipindi vyote na haswa kipindi hiki cha uchaguzi, kulinda vifaa vya uchaguzi na kusimamia usalama katika vituo vya kupigia kura.