Thursday, October 8, 2015




Yale yake unaweza kusema hivyo baada ya mchezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Afrika Kusini kumng’ata mwenzake.


Kupitia picha iliyopigwa na Kevin Quigley, inaonyesha mchezaji wa Afrika Kusini ‘Springboks’, Frans Malherbe akididimiza meno yake kwneye bega la Matt Trouville wa timu ya taifa ya Marekani wakati wakiwania mpira.

Usisahau, siku chache zilizopita kumekuwa na gumzo la beki wa Mbeya City, Juma Nyosso kumtomasa makalio nahodha wa Azam FC, John Bocco. Tayari Nyosso amekumbana na adhabu ya kufungiwa miaka miwili na faini ya Sh milioni 2.

Hata hivyo, kitu kizuri zaidi, Trouville ambaye aling’atwa amewaeleza waamuzi kwamba hakumbuki kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa alikuwa amevaa kifaa maalum cha kulinda mabega ambacho huvaliwa an wachezaji wa mchezo huo.

Bado haijajulikana kama Malherbe atakumbana na adhabu, au suala la muhusika yaani aliyeumwa kusema hakumbuki, linaweza kumuokoa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog