Friday, October 2, 2015
8:27 AM
Unknown
Kuchagua chuo sometimes inakuwa kazi
ngumu sana kwasababu unajikuta na maswali mengi sana baadhi yakiwa; je
campus unayoitaka ina mazingira mazuri ya kusomea, usafiri wa kufika
chuoni unapatikana, huduma za maduka je zipo? lakini swali kubwa kuliko
lote ni, je maisha ya mwanafunzi wa kawaida chuoni hapo yakoje!?
Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Time wa Marekani, wanafunzi waliomaliza High School yani A-level sasa hivi wameamua kutumia Instagram kuchagua vyuo vya kujiunga navyo! Yes Instagram mtu wangu, kwanini?
Kutokana na majibu ya utafiti
uliyofanyika, wanafunzi wengi wamelalamika kuwa wanapata shida kujua
vitu vidogo vidogo kuhusu vyuo wanavyofikiria kujiunga navyo, haswa
kujua hali halisi ya maisha ya wanafunzi wa kawaida vyuoni… Wengine
wamesema ‘vipeperushi’ vinavyotolewa na vyuo vingi havijibu maswali ya hali halisi ya maisha vyuoni na ndio maana wengi wameamua kutumia Instagram ili waweze kuchunguza wenyewe maisha ya kawaida ya kila siku vyuoni yakoje, kujua kama vyuo hivyo vitawafaa!
Utafiti uliofanyika umesema kuwa social network ya Instagram siku hizi ina nafasi kubwa sana ya kumshawishi mwanafunzi kujiunga au kutojiunga na chuo husika kutokana na picha zinazopostiwa kwenye account za wanafunzi wa vyuo mbalimbali, zikionyesha mazingira halisi ya campus hizo pamoja na uhalisia wa maisha ya kila siku kitu ambacho hakipatikani kwenye vipeperushi vya matangazo au kwenye websites za vyuo vingi.
>>>
“mimi binafsi nilichunguza account nyingi za watu kwenye Instagram ili
kuona tu maisha ya kawaida ya wanafunzi yakoje… ni kama kufanya tour ya
chuo husika bila wewe kwenda chuoni hapo na kutembelea kila sehemu yani
ofisini, madarasa, viwanja vya michezo na hata kupata picha ya maisha ya
kila siku … vyote navifanya kwenye Instagram sasa hivi! <<< Morgan Levy mwanafunzi.
>>> “kuna
chuo kimoja nilikifuatilia lakini nikagundua kuwa wanafunzi wengi wa
pale wanapenda sana starehe na party nyingi kitu ambacho sikukifurahia
sana…” <<< Morgan Levy.
Hii imekaa poa sana mtu wangu kwasababu ni rahisi na wala haina
gharama yoyote ile, au wewe unaonaje? Kitu hiki kitawafaa wanafunzi wetu
wa Tanzania!?
8:25 AM
Unknown
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amemwambia nahodha wa Timu hiyo Wayne Rooney kuwa hatasita kumuacha kwenye kikosi hicho endapo ataendelea kucheza chini ya kiwango.
Kauli hii ya Kocha Hodgson inakuja baada ya mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa Manchester United kuonesha kiwango duni ambapo ameshindwa kufunga bao lolote katika mechi kadhaa mpaka sasahivi .
Rooney
kwenye msimu huu amefunga jumla ya mabao manne kwenye mechi 10, sita
zikiwa mechi za ligi ambako amefunga bao moja na nne za ligi ya mabingwa
akiwa amefunga mabao matatu.
Katika mchezo wa juzi kwenye ligi ya mabingwa, Rooney alikosa bao la wazi baada ya kupaisha juu mpira uliopigwa na mshambuliaji Anthony Martial akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.
Hata hivyo Rooney atakuwa na nafasi ya kucheza kwenye mechi zinazofuata za England ambapo ataweza kuizidi rekodi ya gwiji Bobby Charlton kama mfungaji bora wa miaka yote wa timu ya taifa ya England.
2:20 AM
Unknown
Feneberhce
ya Uturuki imejitutumua ikiwa ugenini Glasgow na kufanikiwa kupata sare
ya mabao 2-2 katika michuano ya Kombe la Europa.
Ikiongozwa na Robin van Persie, Feneberhce ililazimika kusawazisha ikitoka chini kwa mabao 2-0 hadi kuwa 2-2.
Shuja alikuwa ni Fernandao ambaye alifunga mabao yote mawili ya kusawazisha katika dakika za 43 na 48.
2:17 AM
Unknown
TAIFA STARS |
Tanzania imepanda nafasi nne katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) lakini bado hali yake ni mbaya kwa jumla katika takwimu hizo
zilizotolewa jana Alhamisi.
Takwimu
hizo zinaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 136 ikiwa ndiyo nchi ya chini
kwa ubora kati ya zile zilizopo Afrika Mashariki katika chati hiyo.
Argentina
imeendelea kubaki namba moja ikifuatiwa na Ujerumani ambayo imepanda kwa nafasi
moja ikiishusha Ubelgiji iliyoshika nafasi ya tatu. Ureno imesogea mpaka nafasi
ya nne wakati kwa nchi za Afrika inayoongoza ni Algeria ikiwa nafasi ya 19.
Viwango
vya Fifa
1.
Argentina
2.
Ujerumani
3.
Ubelgiji
4. Ureno
5.
Colombia
6.
Hispania
7. Brazil
8. Wales
9. Chile
10.
England
93. Rwanda
75. Uganda
113.
Burundi
131. Kenya
136.
Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)