Friday, October 2, 2015


TAIFA STARS
Tanzania imepanda nafasi nne katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lakini bado hali yake ni mbaya kwa jumla katika takwimu hizo zilizotolewa jana Alhamisi.


Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 136 ikiwa ndiyo nchi ya chini kwa ubora kati ya zile zilizopo Afrika Mashariki katika chati hiyo.

Argentina imeendelea kubaki namba moja ikifuatiwa na Ujerumani ambayo imepanda kwa nafasi moja ikiishusha Ubelgiji iliyoshika nafasi ya tatu. Ureno imesogea mpaka nafasi ya nne wakati kwa nchi za Afrika inayoongoza ni Algeria ikiwa nafasi ya 19.

Viwango vya Fifa
1. Argentina
2. Ujerumani
3. Ubelgiji
4. Ureno
5. Colombia
6. Hispania
7. Brazil
8. Wales
9. Chile
10. England
93. Rwanda
75. Uganda
113. Burundi
131. Kenya
136. Tanzania

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog