Monday, April 3, 2017



Moja kati ya majina yaliojipatia umaarufu na heshima kubwa katika soka ni Zinedine Zidane na Ronaldinho ambao uwezo wao umeifanya dunia ya soka kutokusahau mchango wao, Zidane ni mahiri katika kucheza mpira na kufanyia mbwembwe kama ilivyo kwa Ronaldinho.
Naomba nikusogezee video yao kila mmoja akionesha uwezo wake katika soka, mtu wangu wa nguvu naomba jikumbushe halafu usisahau kuacha comment yako nani unamkubali zaidi katika umahiri wa kuuchezea mpira.



Leo April 3 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM mtangazaji Soudy Brown katuletea U-heard inayomhusu msanii Nay wa Mitego kudaiwa kuvunja uchumba wa shabiki yake kutokana na shabiki huyo kuchora tatoo ya Nay wa Mitego. Ndugu wa mchumba aliyekuwa akitarajia kumuoa dada huyo walikataa baada ya kuona tatoo ya Nay wa Mitego kwake.

Soudy Brown alipiga story na Nay wa mitego na majibu yake yalikuwa haya.…..>>>“Mimi simfahamu na mimi napendwa na watu wengi sana wengine siwajui so inawezekana ni shabiki tu japo nashukuru maana amechora tatoo mpaka kufikia hatua ya kuachika lakini mimi simfahamu”:- Nay wa mitego

waliotembelea blog