Thursday, June 12, 2014


WENYEJI, Brazil, baada ya Sherehe ya Ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia iliyofana sana,walijikita Uwanjani na kucheza Mechi ya Ufunguzi kwa kuichapa Croatia Bao 3-1.
Croatia ndio waliotangulia kupata Bao kwenye Dakika ya 11 baada ya Krosi ya chini kutoka Winga ya Kushoto kumkuta Fulbeki wa Kushoto wa Brazil Marcelo ambae alitumbukiza Mpira wavuni bila kutegemea.
Aminia!!!! Oscar
Supastaa Neymar aliamsha sherehe Uwanja mzima na Nchi nzima ya Brazil baada ya kusawazisha kwenye Dakika ya 29 kwa Shuti la chinichini la Mguu wa Kushoto.

Kipindi cha Pili, Brazil walipewa Penati baada ya Beki wa Croatia, Lovren, kumwangusha Fred na Neymar kupiga Bao la Pili.
Huku Dakika zikiyoyoma na Croatia kujikakamua kutaka kusawazisha, kaunta ataki ya Brazil ilizaa Bao la Tatu kwa kazi njema na ya ufundi ya Oscar.
Neymar akipewa kadi ya njanoNeymar akifanyiwa ndivyo sivyo na Vedran wa CroatiaHapa ndipo palizaa penati, mkwaju uliopigwa na NeymarNeymar akifunga mkwaju wa penatiNeymar (kulia) akishangilia bao lake la pili na kufanya 2-1
Hakunaga! Neymar akishangilia...huku macho yote ya Brazil yakiwa kwake.......Oscar akimpelekesha VedranOscar akifunga bao la tatu katika dakika za lala salama3-1 Croatia wakijionea wenyewe 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog