Monday, April 13, 2015


LEO Jumanne Usiku Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI zitaanza kwa Mechi mbili na moja ikiwa huko Jiji la Madrid, Spain ndani ya Estadio Vicente Calderon wakati Atletico Madrid watakapokuwa Wenyeji wa Mahasimu wao Real Madrid.Mechi hii, Dabi ya Madrid, maarufu kama El Derbi Madrileño, ni Marudio ya Fainali ya Msimu uliopita ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo Real Madrid waliinyuka Atletico Madrid Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.

Mechi nyingine ya Jumanne Usiku itachezwa huko Jiji la Turin Nchini Italy wakati Wenyeji Juventus watakapoivaa AS Monaco ya France.

Real watatinga kwa maadui zao Vicente Calderon wakiwa na Kikosi kamili kwa mara ya kwanza katika Miezi Mitano.
James Rodriguez na Toni Kroos, ambao waliikosa Mechi ya La Liga ya Jumamosi walipoifunga Eibar 3-0 baada ya kuwa Kifungoni, wanarejea dimbani.

Nao Atletico wana habari njema ya kurejea dimbani baada ya kuzikosa Mechi mbili akijiuguza Enka kwa Straika wao Mario Mandzukic ambae tangu ahamie Atletico akitoka Bayern Munich mwanzoni mwa Msimu amepachika Bao 20 zikiwemo Bao 2 katika Gemu mbili dhidi ya Real Uwanjani Vicente Calderon.
Jumatano pia zipo mechi mbili nyingine za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kati ya PSG na Barcelona huko Mjini Paris na nyingine itachezwa huko Ureno kati ya FC Porto na Bayern Munich.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Robo Fainali-Mechi za Kwanza
Jumanne Aprili 14

Atlético Madrid vs Real Madrid
Refa: Milorad Mažić (Serbia)

Uwanja: Estadio Vicente Calderón, Madrid, Spain
Juventus vs AS Monaco
Refa: Pavel Královec (Czech Republic)

Uwanja: Juventus Stadium, Turin, Italy

Jumatano Aprili 15
Paris Saint-Germain vs Barcelona

Uwanja: Parc des Princes, Paris, France
FC Porto vs Bayern Munich
Uwanja: Estádio do Dragão, Porto, Portugal


Fernando Torres akiwa na wenzake kwenye mazoezi huko  Vicente Calderon wakijiandaa na kipute cha UEFA leo Jumanne Usiku.

Fundi...! Meneja  Diego Simeone nae kwenye mazoezi

Simeone akiteta na Vijana wake wakati wa Mazoezi leo wakijiandaa vyema kuwakabili ndugu zao  Real Madrid leo Jumanne kwenye UEFA.

 Diego Godin, Arda Turan, Cristian Ansaldi, Antoine Griezmann na Torres wamejumuika leo kwenye zoezi

Simeone na Vijana wake hawajapoteza kwao Atletico Madrid kwenye mitanange sita tangu  2014 Champions League na leo wanaangalia kubaki na pointi
Wakiendelea na Mazoezi Vijana wa Klabu ya Atletico Madrid

Tiago na  Godin  nao kwenye mazoezi.



Wanachama ACT wazalendo la wananchi wa jimbo la Morogoro mjini wakiwa katika mkutano wa ACT wazalendo leo

viongozi wa kitaifa wa ACT wazalendo wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza mkutano wa hadhara jimbo la Morogoro mjini leo

Wanachama wa ACT wazalendo wakiimba wimbo wa Taifa leo


Wananchi wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa leo

Afande Selle akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro mjini kupitia ACT Wazalendo leo


Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Bw Samson Mwigamba akieleza sera ya chama hicho leo

Mwenyekiti wa Taifa wa ACT wazalendo Anna Mngwira akiwahutubia wananchi wa jimbo la Morogoro mjini leo


Zitto Kabwe kushoto na afande Selle wakionyesha alama ya ACT wazalendo

viongozi wa ACT wazalendo wakijumuika kucheza wimbo mpya wa ACT wazalendo



kiongozi wa ACT wazalendo Zitto Kabwe akihutubia katika mkutano wa chama hicho jimbo la Morogoro mjini leo












 

Raheem Sterling akishangilia bao lake la dakika ya 9 kipindi cha kwanza baada ya kuwa butu katika baadhi ya mechi na kuhusishwa kutaka kuondoka Liverpool..leo hii usiku kawaamsha mashabiki kwenye viti kushangilia bao lake, Newcastle United mtanange huu wameumaliza pungufu uwanjani kwao baada ya mwenzao Sissoko kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mbaya Lucas.

Liverpool Ushindi huu umewasimaisha nafasi ya tano wakiwa na pointi 57 wakiwa nyuma ya City wenye pointi 61 wakiwa nafasi ya nne kwenye Ligi Hiyo pendwa Duniani ya EPL huko England. Newcastle United wameachwa nafasi ya 13 wakiwa na pointi 35 nyuma ya Everton wenye pointi 38.Joe Allen dakika ya 70 kipindi cha pili aliwapachikia Liverpool bao la pili na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Newcastle United. Raheem Sterling dakika ya 9 anaipachikia bao Liverpool na kufanya 1-0 dhidi ya Newcastle United. 
Hadi mapumziko Liverpool walikuwa wanaongoza kwa bao hilo la Raheem Sterling.
VIKOSI:
Liverpool Wanaoanza:
Mignolet, Johnson, Can, Lovren, Moreno, Allen, Lucas, Henderson, Ibe, Coutinho, Sterling
Liverpool Akiba: Jones, Toure, Lambert, Manquillo, Borini, Brannagan, Markovic
Newcastle United Wanaoanza: Krul, R.Taylor, Janmaat, Williamson, Colback, Anita, Abeid, Sissoko, Cabella, Obertan, Perez.
Newcastle Akiba: Elliot, Sterry, Gouffran, Gutierrez, Ameobi, Armstong, Riviere


Baada ya ushindi wa magoli 4-2 iliyoupata Manchester United mwishoni mwa wiki uliyopita dhidi ya majirani zao Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya England, meneja wa mashetani wekundu Louis van Gaal amesema ushindi huo ni zawadi tosha kwa mashabiki wa timu hiyo. Katika mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wa timu zote mbili, wageni Man City ndio waliokuwa wa kwanza kundika bao kupitia mchezaji wake Kun Aguero ambaye ndiye mfungaji wa magoli yote kwa upande wa City, goli la Ashley Young, Marouane Fellaini, Juan Mata na Chris Smalling yalitosha kabisa kuikusanyia Manchester Utd point tatu muhimu.Ligi hiyo inaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa pale Liverpool itakapowakaribisha Newcastle Utd. Chelsea bado inaendelea kushika usukani wa ligi hiyo wakiwa na point 73, wakifuatiwa na Arsenal yenye point 66. Manchester Utd wanashika nafasi ya tatu kwa jumla ya point 65, wakati Manchester City wakibaki nafasi ya nne wakiwa na pointi 61.City hoi baada ya kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Man United.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Aprili 11, 2015. Kulia kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe.

Mtoto Tobias Kallaghe ambaye ni mtanzania anayeishi na wazazi wake nchini Uingereza akisamasasoti nyumbani kwao, eneo la High gate London Aprili 11, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe na Binti wa Balozi huyo, Rebecca (katikati) kwenye makazi ya Balozi huyo eneo la Highgate, Londondoni Aprili 11, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Binti wa Balozi wa Tanzainia nchini Uingereza, Rebecca Kallaghe kwenye makazi ya Balozi huyo eneo la Highgate, London Aprili 11, 2015.

waliotembelea blog