Thursday, April 23, 2015


Usiku huu EUROPA LIGI watakamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo Fainali na Timu 4 Washindi zitaingizwa kwenye Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali ambayo pia ni huru bila kujali Utaifa.
Mechi za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Mei 7 na 14 ni Marudiano.

Kocha wa Napoli Rafael Benítez akiteta na Gökhan Inler

Mazoezini


Kocha wa Napoli Rafael Benítez
Kocha wa Napoli Rafael Benítez(kulia) akiongea na Waandishi wa habari ( Hawapo Pichani) juu ya Mtanange wao wa leo Usiku dhidi ya Wolfsburg.

EUROPA LIGI
ROBO FAINALI
Mechi zote kuanza Saa 22:05

Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Alhamisi Aprili 23
Dnipro vs Club Brugge (0-0)
Fiorentina vs Dynamo Kiev (1-1)
Napoli vs VfL Wolfsburg (4-1)
Zenit St Petersburg vs Sevilla (1-2)


Ijumaa Aprili 24 Mchana huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu yao, UEFA itaendesha Droo maalum za kupanga Mechi za Nusu Fainali za Mashindano yao makubwa kwa Klabu za Ulaya yale ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Jana UEFA CHAMPIONS LIGI ilikamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo Famili na Timu 4 zimetinga Nusu Fainali.
Timu hizo 4 ni Mabingwa Watetezi Real Madrid na wenzao wa Spain, FC Barcelona, Mabingwa wa Italy, Juventus na Mabingwa wa Germany, Bayern Munich.
Droo hii ni huru ikimaanisha Timu yeyote inaweza kupangwa na yeyote na hivyo upo uwezekano wa hata kupata El Clasico lile pambano kabambe kati ya Real Madrid na Barcelona.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13.



Wachezaji wa Simba wakishangailia baada ya kupata bao.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akipokea mpira kutoka kwa mwamuzi, Jacob Odongo kutoka Mkoa wa Mara baada ya kufunga 'hat trick' katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Mgambo Shooting mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Mgambo Shooting, Bashiru Chanache katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanya wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 4-0.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Mgambo Shooting, Bashiru Chanache katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanya wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 4-0.

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic akitoa maelekezo kwa Mohamed Hussein.
Mashabiki wa Simba wakifurahia matokeo ya 4-0 baada ya timu yao kuifunga Mgambo Shooting.

Mashabiki wa Simba wakimpongeza Okwi.

waliotembelea blog