Thursday, April 23, 2015


Ijumaa Aprili 24 Mchana huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu yao, UEFA itaendesha Droo maalum za kupanga Mechi za Nusu Fainali za Mashindano yao makubwa kwa Klabu za Ulaya yale ya UEFA CHAMPIONS LIGI na EUROPA LIGI.
Jana UEFA CHAMPIONS LIGI ilikamilisha Mechi zao za Marudiano za Robo Famili na Timu 4 zimetinga Nusu Fainali.
Timu hizo 4 ni Mabingwa Watetezi Real Madrid na wenzao wa Spain, FC Barcelona, Mabingwa wa Italy, Juventus na Mabingwa wa Germany, Bayern Munich.
Droo hii ni huru ikimaanisha Timu yeyote inaweza kupangwa na yeyote na hivyo upo uwezekano wa hata kupata El Clasico lile pambano kabambe kati ya Real Madrid na Barcelona.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Mei 5 na 6 na Marudiano ni Mei 12 na 13.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog