Saturday, June 6, 2015


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.

Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera

Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA.



Luis Suarez, Neymar, Jordi Alba, Lionel Messi, Javier Mascherano na Gerard Pique kwenye mazoezi yao wiki hii wakijiandaa ya Mtanange wa Fainali ya Uefa Champions League kesho Jumamosi Juni 6, 2015.
Hii ni Fainali ya UEFA CHAMPIONS ambayo ama FC Barcelona ya Spain au Juventus ya Italy itatwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Bingwa huyo atakuwa ametwaa Trebo Msimu huu baada ya Timu zote mbili kutwaa Makombe mawili Nchini mwao yale ya Ubingwa na Kombe la Nchi.
Habari kubwa ya Fainali hii ni kukosekana kwa ule mvuto mkubwa wa kuwakutanisha tena kwa mara ya kwanza Beki wa Juventus Giorgio Chiellini na Fowadi wa Barcelona Luis Suarez baada ya Chiellini kuumia Jumatano.
Wachezaji hao walivaana huko Brazil Mwaka Jana wakizichezea Nchi zao kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Suarez kuadhibiwa kwa Kifungo kirefu kwa kumng'ata Meno Chiellini.

Messi kulia

Messi kwenye mazoezi akikabwa na  Dani Alves pamoja na  Adriano.


Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiwa katika mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaofanyika Juni 14, jijini Alexandria. (Picha kwa hisani ya TFF)

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza mazoezi katika uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.
Stars ambayo iliwasili jana jioni jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na 22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.
Akiongelea kuhusu kambi, kocha Nooij amesema kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda wa juu(mita 2000 kutoka usawa wa bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri kutokana na wachezaji kufanya mazoezi katika hali hiyo na kwenda kucheza katika ukanda wa kawaida.

Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo eneo la bahari ya Mediteranian.

waliotembelea blog