MCHEZAJI
BORA DUNIANI Cristiano Ronaldo amerudi kwao huko Mji wa Funchat kwenye
Kisiwa cha Himaya ya Ureno cha Madeira hii Leo Jumapili kuhudhuria
uzinduzi maalum wa Sanamu yake ya kumuenzi kwa mafanikio yake.
Mara baada ya Jana kuisaidia Klabu yake Real Madrid kutwaa Kombe la Dunia kwa Klabu baada ya kuichapa San Lorenzo ya Argentina Bao 2-0 huko Marrakech, Nchini Morocco, Ronaldo aliruka moja kwa moja kwenda Madeira.
Akiongea kwenye uzinduzi huo wa Sanamu yake huku akizungukwa na Familia yake pamoja na Maelfu ya Mashabiki, Ronaldo, ambae alijawa hisia, alitamka: “Huu ni wakati spesho kwangu, kuweka Sanamu yangu!”
Nae Mama yake Mzazi Ronaldo, Dolores Aveiro, alisema: “Ronaldo hajasahau asili yake.”
Sanamu hiyo yenye Urefu wa Mita 3.4 ni sehemu ya mkusanyiko wa Mataji na Tuzo mbalimbali ambazo Ronaldo amezitwaa katika maisha yake ya Soka na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho yake maalum hapo Kisiwani Madeira zikiwemo Ballon d'Or mbili huku akiwekewa matumaini makubwaya kutwa ya tatu ifikapo Januari 12.