Wednesday, August 26, 2015

 
Wachezaji wa Yanga SC wakisherehekea na Ngao ya Jamii wiki iliyopita baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 8-7 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA 

Septemba 12, 2015
Ndanda FC Vs Mgambo JKT
African Sports Vs Simba SC
Majimaji FC Vs JKT Ruvu
Azam FC Vs Prisons
Stand United Vs Mtibwa Sugar
Toto Africans Vs Mwadui
Mbeya City Vs Kagera Sugar
Septemba 13, 2015
Yanga SC Vs Coastal Union
Septemba 16, 2015
Yanga SC Vs Prisons
Mgambo JKT Vs Simba SC
Majimaji FC Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Azam FC
Toto Africans Vs Mtibwa Sugar
Ndanda FC Vs Coastal Union
Septemba 17, 2015
Mwadui FC Vs African Sports
Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo JKT Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo JKT
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015
African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC wanatarajiwa kuweka kambi ya wiki moja visiwani Zanzibar kuanzia Septemba 6, kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayoanza wiki itakayofuatia.
Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amesema kwamba kwa sasa kikosi kipo Dar es Salaam kikiendelea na mazoezi chini ya kocha Hans van der Pluijm.
“Mazoezi yanaendelea Dar es Salaam kwa sasa, kama unavyojua, wachezaji wetu wengi wamekwenda kuzitumikia timu zao za taifa, hivyo waliobaki wanaendelea na mazoezi,”amesema Dk. Tiboroha.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, watafungua dimba na Coastal Union ya Tanga Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wiki iliyopita, Yanga SC ilifungua pazia la Ligi Kuu kwa ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo, kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ alipangua penalti mbili za beki raia wa Ivory Coast, Serge Wawa Pascal na mshambuliaji Ame Ali ‘Zungu’, wakati kipa wa Azam FC, Aishi Manula naye alicheza penalti ya Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.
Penalti za Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondan aliyepiga ya mwisho.
Penalti za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Nahodha John Raphael Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomary Kapombe. 
Ushindi huo ni sawa na kisasi baada ya Yanga SC kufungwa kwa penalti 5-3 katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Julai 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa, baada ya sare ya 0-0. 
Ni mara ya tano sasa Yanga SC kutwaa Ngao ya Jamii ikiwa ni rekodi, baada ya kuifunga Simba SC mara mbili, mwaka 2001 mabao 2-1 na 2010 kwa penalti 3-1 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika ya 90, kabla ya kuifunga Azam FC miaka mitatu mfululizo, 2013 bao 1-0 na 2014 mabao 3-0.
Inafuatia Simba SC iliyotwaa Ngao mara mbili, mwaka 2011 wakiifunga Yanga SC 2-0 na 2012 wakiifunga Azam FC 3-2, wakati Mtibwa Sugar ni timu nyingine iliyowahi kutwaa Ngao mwaka 2009 ikiifunga 1-0 Yanga SC.


WINGA Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ usiku huu amefunga bao lake la kwanza Azam FC ikilazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, walianza kupata bao kupitia kwa Singano ‘Messi’ kabla ya Bakari Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. 
Hilo linakuwa bao la tatu kwa Azam FC kufungwa kufungwa ndania ya mechi 15 ilizocheza tangu kurejea kwa kocha Muingereza, Stewart John Hall Juni mwaka huu.
Awali ya hapo, ni Friends Rangers pekee walioweza kuupenya ukuta wa Azam FC ya Stewart na kufunga mara mbili wakilala 4-2 katika mchezo wake wa kwanza kabisa wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Baada ya hapo, Azam FC ilishinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Chamazi, 1-0 dhidi ya African Sports Tanga, 1-0 dhidi ya Coastal Union Tanga, zote zikiwa mechi za kirafiki kabla ya kuingia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na kushinda mechi zote hadi kutwaa ubingwa.
Ilianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya KCCA kabla ya kuzifunga 2-0 Malakia ya Sudan Kusini, 5-0 Adama City ya Ethiopia na baadaye kushinda kwa penalti 5-3 dhidi ya Yanga SC baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika Nusu Fainali, Azam FC iliichapa tena 1-0 KCCA kabla ya kumaliza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya 2-0 Gor Mahia ya Kenya katika Fainali na kutwaa Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza.
Kutoka hapo, Azam FC ikashinda mechi tatu mfululizo za kirafiki visiwani Zanzibar 1-0 dhidi ya KMKM, 3-0 dhidi ya Mafunzo na 2-0 dhdi ya JKU kabla ya sare ya 0-0 na Yanga SC katika mechi ya Ngao- ambayo mwishowe walifungwa kwa penalti 8-7.
Kipa wa Azam FC, Aishi Manula alicheza penalti ya kwanza ya Yanga SC iliyopigwa na Nahodha wao, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ lakini Serge Wawa akaenda kukosa kabla ya Ame Ally pia kukosa.
Penalti za Yanga SC zilifungwa na Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Amissi Tambwe, Andrey Coutinho, Godfrey Mwashiuya, Thabani Kamusoko, Mbuyu Twite na Kelvin Yondan aliyepiga ya mwisho.
Penalti za Azam FC zilifungwa na Kipre Herman Tchetche, Nahodha John Raphael Bocco, Himid Mao Mkami, Aggrey Morris, Jean Baptiste Mugiraneza, Erasto Nyoni na Shomary Kapombe.


Wayne Rooney akiondoka na mpira wake Uwanjani baada ya kupiga hat-trickAnder akishangilia bao lake la nne kwa man unitedAnder Herrera alifunga bao lake dakika ya 63 kipindi cha pili na kufanya 4-0 huku matokeo jumla yakiongezeka na kuwa (1-7). Dakika ya 81 Chicharito aliteleza na kukosa mkwaju wa penati kwa kupiga mpira vibaya kwa nje.
Rooney anaondoa ukame wa mabao katika Mtanange huu wa marudiano anatupia bao tatu kwa mpigo.. Hat-trick!
Chicharito alikosa nafasi ya wazi hapaNa hapa akiwa chini baada ya kukosa penati Hernandez akiwa chini akijiuliza baada ya kukosa penatiChicharito aliteleza wakati wa upigaji penati kipindi cha pili mwishoniMweleka!Balaa! Ander akishangilia bao
Wayne Rooney alipiga hat-trick kwa kufunga bao la tatu dakika ya 57 kipindi cha pili na kufanya 3-0.Dakika ya 49 kipindi cha pili Wayne Rooney aliipatia bao la pili Man United na kufanya 2-0 dhidi ya Club Brugge.Rooney akishangilia moja ya bao lake usiku huu.Wayne Rooney akishangilia bao lake mapema kipindi cha kwanza dakika ya 20 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Depay. Kipindi cha kwanza kilimalizika United wakiwa mbele ya bao 1-0, (Agg 1-4).
Rooney na Depay wakipongezanaDakika ya 20 kipindi cha kwanza Wayne Rooney aliwafungia bao la kuongoza Man United kwa kufanya 1-0 dhidi ya Timu ya Club Brugge Nchini Ubelgiji.Kikosi cha Man UnitedSehemu ya Mashabiki wa Man UnitedSir Bobby na Mwenyekiti Ed W. ndani huko Belgium.Wakipasha kabla ya Mechi
VIKOSI:
Club Bruges:
Bolat, De Fauw, Castelletto, Duarte, De Bock, Claudemir, Vormer, Vazquez, Bolingoli Mbombo, De Sutter, Diaby.
Akiba: Bruzzese, Meunier, Vanaken, Cools, De Smul, Dierckx, Oulare.
Man Utd: Romero, Darmian, Smalling, Blind, Shaw, Ander Herrera, Carrick, Mata, Januzaj, Depay, Rooney. 

Akiba: Johnstone, Hernandez, Young, Fellaini, Schneiderlin, Schweinsteiger, McNair.
Refa: Antonio Miguel Mateu Lahoz (Spain)

aina
Moja ya safari zinazokufanya uwe huru zaidi ni pamoja na usafiri wa ndege.
Zipo ndege za aina mbalimbali na gharama zake hutegemea na umbali wa safari ya mtu..lakini pia watalam wa ndege wameweza kutengeneza hizi ndege ambazo unapoipanga inakufanya ujione ni sawa na upo nyumbani kutokana na vitu vinavyopatikana ndani yake.
Nimekuwekea hizi Pichaz 15 za aina mbalimbali za ndege ambazo ni za kifahari zaidi duniani
singapo
1. Singapore Airlines

singapo2
2. Etihad Diamond First

singapo3
3. Emirates First Class Suites

4
4. ANA First Square

5
5. Qatar Airways

66
6. Virgin Atlantic
7
7. Air France

8
8. JetBlue Mint

9
9. American Airlines Flagship

10
10. Thai Royal First

11
11. Transaero Imperial Class

12
12. Korean Air Kosmo Suite

13
13. Oman Air First Class

14
14. British Airways First Class

15
15. Lufthansa First Class
August 25 ni siku ambayo mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli ambaye alikuwa akiichezea Liverpool ya Uingereza  athibitishwe kujiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkopo wa muda mrefu. Balotelli alijiunga na AC Milan ikiwa ni msimu mmoja umepita toka ahamie Liverpool akitokea klabu ya AC Milan
2BABE7BA00000578-0-image-a-54_1440581954477
Sasa August 26 zimetoka taarifa mpya kuhusu vipengele vilivyomo ndani ya mkataba wa Mario Balotelli wa kujiunga na AC Milan, imethibitishwa kuwa, kuna kipengele ambacho kinamzuia kuweka Style za nywele za ajabu kuvuta sigara ili kulinda afya yake, afike mazoezini kwa wakati, kunywa pombe na kwenda Club bila mpangilio.
2BABE79600000578-0-image-m-53_1440581945151
Kwa mujibu wa gazeti la dello Sport linaeleza kuwa afisa mtendaji mkuu wa klabu ya AC Milan Adriano Galliani ameeleza kuhusiana na kipengele hicho kuwemo kwenye mkataba, Balotelli amewahi kukutwa na muhudumu wa treni akivuta sigara katika choo cha treni.
2BABD8B100000578-0-image-a-38_1440581288448
Haya ni baadhi ya makosa ambayo Balotelli aliwahi kufanya na faini alizolipa
1 2

Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Uingereza na Ligi Kuu Hispania mashirikisho ya soka ya nchi husika huwa wanatangaza aina ya mpira utakaotumika katika msimu husika, tayari tumeshaona mpira unaotumika katika Ligi mbalimbali barani Ulaya.
News-Picture-UEFA
August 26 umetangazwa mpira utakaotumika katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu huu, licha ya kuwa ulitumika katika mechi ya kwanza ya mchujo katika ya Manchester United dhidi ya Bruges lakini August 27 ni siku ambayo utazinduliwa rasmi mpira huo katika mji wa Marseille Ufaransa.
Uzinduzi huo utapambwa na uwepo wa wachezaji wa vilabu vya Man United, Real Madrid, AC Milan, Bayern Munich, Chelsea na Juventus lakini ni siku ambayo droo ya makundi ya klabu Bingwa Ulaya itachezeshwa.
Hizi ni picha za mpira huo


Adidas-Finale-15-Champions-League-Official-Match-Ball (1)

.
.
Wakati Ukawa wakiwa wamezuiliwa kutumia uwanja wa Jangwani uliopo Dar es Salaam kwenye shughuli za kampeni uchaguzi 2015, sasa hapa nina picha ambazo zikimuonesha mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara zake huko Mikoani ikiwemo, Tunduma, Sumbawanga, Rukwa.
.
.Mhe. Magufuli katika Kampeni za Uchaguzi 2015 mkoani Sumbawanga.
.
.Mhe John Pombe Magufuli akihotubia Wananchi wa Tunduma, asema atashulikia matatizo yao.

waliotembelea blog