Tuesday, February 17, 2015



LEO Jumatano Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI Real Madrid wanarudi tena Veltins-Arena, Mjini Gelsenkirchen huko Germany ambako Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliwanyuka Wenyeji wao Schalke 6-1.
Hata hivyo safari hii Schalke wako chini ya Meneja wa zamani wa Chelsea aliewabebesha Kombe hili Mwaka 2012 Roberto Di Matteo lakini wana kibarua kigumu kwani pia atawakosa Nyota wake Majeruhi Julian Draxler, Leon Goretzka na Jefferson Farfan.
Lakini pia Real, chini ya Meneja Carlo Ancelotti wana Majeruhi ambao ni pamoja na Viungo wao muhimu James Rodriguez na Luca Modric na Beki Sergio Ramos ingawa Beki mwingine, Pepe, amepona na huenda akacheza.
Katika Mechi nyingine ya Jumatano, Mabingwa wa Uswisi FC Basel, ambao waliwapiku na kuwatupa nje ya Mashindano haya Liverpool katika hatua za Makundi, wanaivaa Porto ya Ureno ambayo haikufungwa hata Mechi kwenye hatua hiyo ya Makundi.

RATIBA LEO JUMATANO
Jumatano 18 Februari 2015

Schalke 04 vs Real Madrid CF
FC Basel 1893 vs FC Porto
Jumanne 24 Februari 2015
Juventus FC vs BV Borussia Dortmund
Manchester City vs FC Barcelona
Jumatano 25 Februari 2015
Arsenal FC vs AS Monaco FC Bayer 04 

Leverkusen vs Atletico de Madrid


Kipindi chs pili dakika ya 54 Edinson Cavani aliisawazishia bao PSG kwa kichwa baada ya kupokea krosi kutoka kwa Blaise Matuidi kama kona na kuweza kusawazisha bao kwa kichwa na kufanya 1-1. Mchezo huu utaendelea kwenye marudiano huko Stamford Bridge Chelsea watakapoikaribisha na wao PSG ili kuamua ni Timu gani inasonga hatua inayofuata ya Robo Fainali.Dakika ya 36 Branislav Ivanovic anaifungia bao Chelsea 1-0 dhidi ya PSG bao la kichwa baada ya kusogezewa pasi ya kisigino na Gary Cahill. Mpaka mapumziko Chelsea ndio walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.Kukabana" hakuna kupeana nafasi...Patashika..Kipindi cha kwanza.Wamekutana...David Beckham  akipeana neno na Kocha wake wa Zamani Man United Mzee Sir Alex Ferguson leo wakati wa Mchezo wa PSG na Chelsea. David Beckham  alistaafu soka akiwa katika timu hiyo ya PSG msimu wa 2012-13 Ligue 1.David Beckham and Sir Alex Ferguson (right) watch on as PSG face Chelsea in the Champions LeagueMtanange ukiendelea..David Beckham akiwa anatazama kipute kati ya PSG vs Chelsea huko Ufaransa.Kikosi kilichoanza cha Chelsea dhidi ya PSG
VIKOSI:
Paris Saint Germain Wanaoanza:
Sirigu, Van der Wiel, Silva, Marquinhos, Maxwell, David Luiz, Verratti, Matuidi, Lavezzi, Ibrahimovic, Cavani
PSG Akiba: Douchez, Camara, Bahebeck, Digne, Rabiot, Pastore, Kimpembe
Chelsea wanaoanza: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Fabregas, Hazard, Diego Costa
Chelsea FC Akiba: Cech, Filipe Luis, Zouma, Oscar, Cuadrado, Drogba, Remy

Refa: Cuneyt Cakir


www.bukobasports.comUEFA CHAMPIONS LIGI inarudi tena dimbani Jumanne Februari 17 kwa Mechi mbili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine watakapokuwa Wenyeji wa Bayern Munich na Paris Saint-Germain kuikaribisha Chelsea ndani ya Parc des Princes Jijini Paris Nchini France.
Jumatano Raundi ya Mtoano ya Timu 16 pia itaendelea kwa Mechi mbili ambapo Mabingwa Watetezi Real Madrid watakuwa Wageni wa Schalke huko Ujerumani.
Mechi nyingine Siku hiyo ni ile ya kule Uswisi kati ya Wenyeji FC Basel 1893 na FC Porto ya Portugal.
Mechi nyingine 4 zilizobakia za Raundi hii zitachezwa Wiki ijayo.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza.
Mechi kati ya FC Shakhtar Donetsk na Bayern Munich huko Nchini Ukraine imehamishwa toka Mji wa Nyumbani wa FC Shakhtar, Donetsk, kwenda Lviv kwa sababu Mji huo umeshikiliwa na Wapinzani katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe Nchini humo.
Jumatano Mabingwa Real wanacheza Nyumbani kwa Schalke ambako Msimu uliopita Uwanjani hapo hapo kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliinyuka Schalke 6-1.
Msimu huu, kwenye hatua ya Makundi, Schalke pia walidundwa Bao 5-0 na Chelsea hapo hapo kwao na kupenya toka hatua hiyo baada ya kuifunga Sporting Lisbon 4-3 wakati Mabingwa Watetezi Real walivuka hatua ya Makundi kwa kushinda Mechi zao zote 6.
Katika Mechi nyingine ya Jumatano, Mabingwa wa Uswisi FC Basel, ambao waliwapiku na kuwatupa nje ya Mashindano haya Liverpool katika hatua za Makundi, wanaivaa Porto ya Ureno ambayo haikufungwa hata Mechi kwenye hatua hiyo ya Makundi.
Baadhi ya Mechi nyingine za mvuto za Wiki ijayo za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni ile ya Uwanja wa Etihad kati ya Manchester City na Barcelona hapo Februari 24 ikiwa pia ni Marudio ya Raundi kama hii ya Msimu uliopita ambayo Barcelona walishinda kwa Jumla ya Bao 4-1 katika Mechi mbili.
Siku hiyo hiyo, Mabingwa wa Italy na Vinara wa Ligi Serie A, Juventus watakuwa Wenyeji wa Borussia Dortmund iliyoanguka vibaya huko kwao kwenye Bundesliga.
Jumatano Februari 25, Arsenal ya Arsene Wenger itaivaa AS Monaco ya France ikiwa ni mara ya kwanza kwa Wenger kucheza na Klabu yake ya zamani katika Mashindano rasmi.
Mechi ya Pili ya Jumatano hiyo hiyo, ambayo itakamilisha Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni kati ya Bayer Leverkusen na Atletico Madrid ambao ndio Washindi wa Pili wa UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA:

Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku leo
Jumanne 17 Februari 2015
FC Shakhtar Donetsk vs Bayern Munich
Paris Saint-Germain vs Chelsea FC

Jumatano 18 Februari 2015
Schalke 04 vs Real Madrid CF
FC Basel 1893 vs FC Porto 

waliotembelea blog