LEO Jumatano Mabingwa Watetezi wa UEFA CHAMPIONS LIGI Real Madrid wanarudi tena Veltins-Arena, Mjini Gelsenkirchen huko Germany ambako Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliwanyuka Wenyeji wao Schalke 6-1.
Hata hivyo safari hii Schalke wako chini ya Meneja wa zamani wa Chelsea aliewabebesha Kombe hili Mwaka 2012 Roberto Di Matteo lakini wana kibarua kigumu kwani pia atawakosa Nyota wake Majeruhi Julian Draxler, Leon Goretzka na Jefferson Farfan.
Lakini pia Real, chini ya Meneja Carlo Ancelotti wana Majeruhi ambao ni pamoja na Viungo wao muhimu James Rodriguez na Luca Modric na Beki Sergio Ramos ingawa Beki mwingine, Pepe, amepona na huenda akacheza.
Katika Mechi nyingine ya Jumatano, Mabingwa wa Uswisi FC Basel, ambao waliwapiku na kuwatupa nje ya Mashindano haya Liverpool katika hatua za Makundi, wanaivaa Porto ya Ureno ambayo haikufungwa hata Mechi kwenye hatua hiyo ya Makundi.
RATIBA LEO JUMATANO
Jumatano 18 Februari 2015
Schalke 04 vs Real Madrid CF
FC Basel 1893 vs FC Porto
Jumanne 24 Februari 2015
Juventus FC vs BV Borussia Dortmund
Manchester City vs FC Barcelona
Jumatano 25 Februari 2015
Arsenal FC vs AS Monaco FC Bayer 04
Leverkusen vs Atletico de Madrid
0 maoni:
Post a Comment